Boss Man
JF-Expert Member
- Feb 10, 2022
- 458
- 991
Wakubwa ebu leo tujichallange kidogo, tusiishie kukosoa tu huku tukiwa benchi ebu Leo tujipe madaraka ya Urais na kila mtu aseme kwa nafasi yake kama ungekuwa Rais ungefanya Nini? au ungeboresha kitu gani? pengine baadhi ya maoni yanaweza kuchukuliwa hapa na kufanyiwa kazi
Binafsi kama Mimi ndio namba One, ningeboresha kwenye swala la usafiri wa umma na ningepiga marufuku matumizi ya magari binafsi siku za kazi (weekdays) na ningeyaruhusu siku za weekends tu, hata wafanyakazi wa taasisi mbalimbali za serikali wangekuwa na mabasi yao pamoja na wabunge, mambo ya V8 kuendea jimboni kwako tu
Kwanza kabisa hii ingesaidia kupunguza foleni na kufika kazini kwa wakati, na mafuta yangekuwa bei rahisi, matabaka yangepungua kwa kiasi kikubwa, pia ingesaidia kupunguza ulimbukeni wa vijana kukimbilia kumiliki magari bila sababu za msingi
Kitu kingine ningechukua vijana wote waliokosa kazi na kuwapeleka semina za kilimo baada ya nawaimgiza maporini huko kwenye mashamba pembejeo Kila kitu Bure, ukishavuna serikali inakula asilimia 60% ya mavuno kwa misimu 3 mfululizo baada ya hapo unaachwa undelee mwenyewe, na uamuzi ni wako kuendelea na kilimo au kufanya Biashara nyingine
Hii itasaidia nchi kuwa na chakula Cha kutosha, hvyo hata bei za vyakula masokoni itakuwa ni rafiki kwa mwananchi wa kawaida na pia tutakuwa tumepunguza vijana wengi wasio na Kazi na kujipatia mitaji kwa style hiyo
Hayo ni machache kati ya mengi ambayo ningeyafanya au natamani serikali ingeyafanya, siwezi kueleza yote nimewaachia na nyie Uwanja
NB: Ni ruksa kukosoa mawazo ya mtu ila kwa hoja, hata Mimi unaweza kunikosoa hayo mawazo yangu kwa hoja
Je wewe ungefanya/boresha nini?