Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,185
- 7,491
Wakuu salaam,
Ki msingi mtu unapokuwa na biashara kubwa hasa inayofanya kazi kwenye mfumo wa kampuni, pamoja na mambo mengine unatakiwa uwe na vitu (3) ili ufanikiwe.
1. Mtaji (2) Maono (Vission) na (3) Rasilimali watu ya kufaa.
Utafiti wangu wa kina unaonesha kuwa watu wengi wanaoanzisha biashara Tanzania hawafanikiwi ipasavyo au wanafeli kabisa kwa sababu ya rasilimali watu isiyoridhisha na hivyo biashara kuwa na usimamizi duni au usiofaa kabisa hivyo wengine kuishia kufilisika na wengine kuogopa kuwekeza. Haina maana kwamba hakuna watu au wasomi! lahasha! wapo wengi tu na unapotangaza kazi wanaomba kwa maelfu lakini kwa sasa ni vigumu sana kupata mtu ambaye ana Elimu/uelewa wa kutosha, uzoefu wa kutosha, uwezo wa kusimamia Biashara na Rasilimali Watu na kubwa kupita yote na ambalo ndio changamoto kubwa kupita yote ni kupata mtu Mwaminifu ambaye haingiwi na tamaa ya kukuibia (kuibia kampuni)na anajijenga na kuwajenga wafanyakazi wengine kujihisi ni sehemu ya kampuni, hivyo mafanikio ya kampuni ni mafanikio yao vile vile. Watu wenye biashara kubwa kubwa watakuwa wananielewa vizuri hapa!.
Kama una biashara kubwa/kampuni au unatarajia kuanzisha biashara kubwa au kampuni, na unatafuta "Meneja wa Biashara", nakuomba uwasiliane nami na nakuhakikishia hutojutia kwani Mwenyezi Mungu akipenda biashara yako itakwenda vizuri kuliko hata ulivyokuwa umwekusudia. Biashara yako itakuwa inaendeshwa kwa faida na itakuwa haikupasui kichwa ( Hakuna haja ya mtu kuwekeza hela yako kwenye biashara halafu ukageuka kuwa mtumwa wa hela yako mwenyewe hata usingizi haupati kwa sababu ya wasimamizi wasio waaminifu).
Baadhi ya sifa nilizo nazo ni kama ifuatavyo:
Nina uzoefu wa kusimamia Rasilimali watu kwenye Taasisi yenye wafanyakazi zaidi ya 1500 kwa zaidi ya miaka 4.
Nina uzoefu wa kufanya kazi za kiutawala kwenye taasisi kubwa yenye wafanyakazi zaidi ya 1500 kwa zaidi ya miaka 4.
Nina uwezo mzuri na uzoefu kwenye masuala ya kiuongozi na nimekuwa nikiongoza na kushauri wengi kwenye masuala ya kiuongozi.
Ninatoa huduma bora sana "Customer service" kwa wateja ambao nimekuwa nikiwahudumia kwa kipindi chote kiasi kwamba wateja wamekuwa wakinipa zawadi ya vitu mbalimbali kutokana na huduma bora ninayowapatia Ikiwemo fedha tasilim. Aidha, nimekuwa nikiikabidhi kwenye taasisi zawadi hizo kwa kuwa nimekuwa nikizipata kwa jina na mgongo wa ofisi .
Kuna mengi ya kuyazungumza ila kama kuna mtu ana au anataka kuwekeza kwenye kuanzisha biashara kubwa na anatafuta msimamizi wa biashara hiyo asisite kuwasiliana nami kwa mazungumzo zaidi na kama akiridhika tunaweza kufanya kazi na hatojutia!. Nasema biashara kubwa kwa sababu wakati wote napenda kufanya vitu ambavyo ni "challenging" kwa sababu naamini kwamba kwa jinsi mtu unavyotumia akili ndivyo uwezo wa kufikiri unavyoongezeka!
Kwa anayetaka kujua chochote zaidi tuwasliane tafadhali ila ni vizuri kuwa serious!.Kwa pamoja tukuze uchumi wetu!
Betlehem.