Kama Unatafuta "Business Manager" Tuwasiliane!

Azizi Mussa

JF-Expert Member
May 9, 2012
9,172
7,427
Wakuu salaam,

Ki msingi mtu unapokuwa na biashara kubwa hasa inayofanya kazi kwenye mfumo wa kampuni, pamoja na mambo mengine unatakiwa uwe na vitu (3) ili ufanikiwe.

1. Mtaji (2) Maono (Vission) na (3) Rasilimali watu ya kufaa.

Utafiti wangu wa kina unaonesha kuwa watu wengi wanaoanzisha biashara Tanzania hawafanikiwi ipasavyo au wanafeli kabisa kwa sababu ya rasilimali watu isiyoridhisha na hivyo biashara kuwa na usimamizi duni au usiofaa kabisa hivyo wengine kuishia kufilisika na wengine kuogopa kuwekeza. Haina maana kwamba hakuna watu au wasomi! lahasha! wapo wengi tu na unapotangaza kazi wanaomba kwa maelfu lakini kwa sasa ni vigumu sana kupata mtu ambaye ana Elimu/uelewa wa kutosha, uzoefu wa kutosha, uwezo wa kusimamia Biashara na Rasilimali Watu na kubwa kupita yote na ambalo ndio changamoto kubwa kupita yote ni kupata mtu Mwaminifu ambaye haingiwi na tamaa ya kukuibia (kuibia kampuni)na anajijenga na kuwajenga wafanyakazi wengine kujihisi ni sehemu ya kampuni, hivyo mafanikio ya kampuni ni mafanikio yao vile vile. Watu wenye biashara kubwa kubwa watakuwa wananielewa vizuri hapa!.

Kama una biashara kubwa/kampuni au unatarajia kuanzisha biashara kubwa au kampuni, na unatafuta "Meneja wa Biashara", nakuomba uwasiliane nami na nakuhakikishia hutojutia kwani Mwenyezi Mungu akipenda biashara yako itakwenda vizuri kuliko hata ulivyokuwa umwekusudia. Biashara yako itakuwa inaendeshwa kwa faida na itakuwa haikupasui kichwa ( Hakuna haja ya mtu kuwekeza hela yako kwenye biashara halafu ukageuka kuwa mtumwa wa hela yako mwenyewe hata usingizi haupati kwa sababu ya wasimamizi wasio waaminifu).

Baadhi ya sifa nilizo nazo ni kama ifuatavyo:
Nina uzoefu wa kusimamia Rasilimali watu kwenye Taasisi yenye wafanyakazi zaidi ya 1500 kwa zaidi ya miaka 4.
Nina uzoefu wa kufanya kazi za kiutawala kwenye taasisi kubwa yenye wafanyakazi zaidi ya 1500 kwa zaidi ya miaka 4.

Nina uwezo mzuri na uzoefu kwenye masuala ya kiuongozi na nimekuwa nikiongoza na kushauri wengi kwenye masuala ya kiuongozi.

Ninatoa huduma bora sana "Customer service" kwa wateja ambao nimekuwa nikiwahudumia kwa kipindi chote kiasi kwamba wateja wamekuwa wakinipa zawadi ya vitu mbalimbali kutokana na huduma bora ninayowapatia Ikiwemo fedha tasilim. Aidha, nimekuwa nikiikabidhi kwenye taasisi zawadi hizo kwa kuwa nimekuwa nikizipata kwa jina na mgongo wa ofisi .

Kuna mengi ya kuyazungumza ila kama kuna mtu ana au anataka kuwekeza kwenye kuanzisha biashara kubwa na anatafuta msimamizi wa biashara hiyo asisite kuwasiliana nami kwa mazungumzo zaidi na kama akiridhika tunaweza kufanya kazi na hatojutia!. Nasema biashara kubwa kwa sababu wakati wote napenda kufanya vitu ambavyo ni "challenging" kwa sababu naamini kwamba kwa jinsi mtu unavyotumia akili ndivyo uwezo wa kufikiri unavyoongezeka!

Kwa anayetaka kujua chochote zaidi tuwasliane tafadhali ila ni vizuri kuwa serious!.Kwa pamoja tukuze uchumi wetu!

Betlehem.
 
ok samahan kwa swali langu kama litakuboa, kwasasa unajishugulisha na nini??
Mkuu kwanza ifahamike kuwa nina kazi kwa sasa, sio kwamba nipo tu! kama nilivyosema nasimamia Rasilimali watu na masuala ya utawala kwenye Taasisi moja kubwa ambayo siwezi kuitaja humu (ila haifanyi biashara). Aidha pia nina biashara binafsi lakini ndogondogo kulingana na mtaji wangu bado haujakuwa. Kwa hiyo ieleweke vizuri kuwa sio kwamba ni jobless! lahasha! bali naamini sana katika uzalishajimali, uwekezaji, biashara na mchango wa sekta bnafsi katika maendeleo ya mtu mmoja mmoja na taifa.

Pia naelewa ni kwa jinsi gani kampuni moja tu iliyostawi inaweza kutoa ajira na kuwasaidia watu wengi kimaisha ila sasa shida ni kwamba haiwezi kustawi bila "Strong Management" na strong management ni pamoja na kupata msimamizi mwenye uwezo na uaminifu, na watu hao kwa sasa ni wachache sana.
 
asante sana kwa kunijibu nilivyokuwa nategemea, ningependa kujua mifano ya makampuni ambyo unaona yako ndani ya uwezo wako kiusimamizi yanayo fahamika hapa tz. samahn pia
 
asante sana kwa kunijibu nilivyokuwa nategemea, ningependa kujua mifano ya makampuni ambyo unaona yako ndani ya uwezo wako kiusimamizi yanayo fahamika hapa tz. samahn pia
Napendelea zaidi iwe mpya ili kuijenga. Sio vizuri sana kupendelea ambavyo walishajenga wenzako.
 
Napendelea zaidi iwe mpya ili kuijenga. Sio vizuri sana kupendelea ambavyo walishajenga wenzako.
sawa ndugu.mimi napenda sana mwongozo endelevu wa kibiashara lakn kwa tz naona kama changamoto kwasababu ya mambo mengi yanayo tuzunguka ususan wafanya bishara wadogo kwailo unalizungumziaje
 
sawa ndugu.mimi napenda sana mwongozo endelevu wa kibiashara lakn kwa tz naona kama changamoto kwasababu ya mambo mengi yanayo tuzunguka ususan wafanya bishara wadogo kwailo unalizungumziaje
Mkuu, Tanzania kuna fursa nyingi sana, tatizo uaminifu wa watu. Nakuhakikishia kama ukipata wasimamizi wa biashara waaminifu na wabunifu na ukawa na customer service nzuri unatajirika mkuu. Kwa mfano tunaagiza bidhaa Japani na China wanatuletea licha ya kuwa hatuwajui na hatuwajui na hata wakiamua kutuibia hatuna la kuwafanya.Wewe hebu vuta Picha unatuma mamilioni ya hela Japan uletewe gari kwa imani tu na wanakuletea kweli.Sasa kama mfano wewe uko dar, tuma milioni mbili Mbeya uletewe mchele uone kama utakuja! Nunua daladala bila kufuatilia kama mwandawazimu uone kama hesabu itakuja! sana sana utarudishiwa gari injini imeshakufa dereva kala hela ya oil uliyompa, kisha anaendesha coaster mpya bila oil kisa tamaa ya hela ya oil elfu 80, mwezi gari unapaki!.

Nishashuhudia mtu anapewa semi la mzigo kupeleka nchi jirani akifika njiani anauza mzigo wote WA MIL 20 anatoroka huku wateja wanasubiria mzigo wao nchi jirani, au mtu anapewa tanki la mafuta anafika njiani anayauza (KILA LITA SH 400) gari analichoma moto anampigia mwenye gari "Boss gari imeungua moto, mimi nimenusurika! " ni hatari sana!
 
uhaminifu umekuwa tatizio na nimiongoni mwa changamoto zinazo tuludisha nyuma kiuchumi pamoja na umimi
Uko sahihi sana mkuu, yaani unaweza ukawekeza mwishowe fedha yako ikakupa presha na sukari, baadae uka paralyze kutokana na pesa yako mwenyewe. Inahitaji umakini sana.
 
Mm napenda kuwa na meneja hadi mhasibu kwasababu biashara yangu imefikia ivyo ila naogopa sana na sijuhi watu waaminifu kwa Tanzania hii wanapatikana wapi kwaiyo kuna watu nawakodi kwa kuandaa returns kwenda TRA
 
Mm napenda kuwa na meneja hadi mhasibu kwasababu biashara yangu imefikia ivyo ila naogopa sana na sijuhi watu waaminifu kwa Tanzania hii wanapatikana wapi kwaiyo kuna watu nawakodi kwa kuandaa returns kwenda TRA
Upo wapi mkuu
 
ACT wazalendo hakijaeleweka? nauliza tu
Ili mtu uweze kuendelea ni lazima ufikiri nje ya box, na ili ufikiri nje ya box, lazima kwanza awepo mtu wa kukuchorea hilo box ili ufikiri nje yake.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom