Bernard bakari
JF-Expert Member
- Mar 30, 2016
- 407
- 781
Ndoa ni Tamu sana tena Tamu kuliko kitu chochote ndani ya hii Dunia. Utamu wa ndoa utaushuhudia na kuuona pale tu ambapo wana ndoa watakuwa wamoja, wenye furaha na Amani. Kuwepo kwa migogoro kwa wana ndoa huweza kufanya ndoa kuwa chungu zaidi ya pilipili.
Katika vitu vinavyofanya ndoa iwe chungu, iwe na migogoro ya mara kwa mara ni USALITI. Usaliti ukianza kwa mmoja wa wanandoa kunafanya ndoa iwe chungu sana iwe mwenza kagundua au hajagundua kama anasalitiwa Na mpenzi wake.
Ukisaliti ndoa huko unakoenda unaweza pata vitu 2 kwanza unaweza kutana na mambo matamu kuliko ya mwenza wako au ukakutana na mambo mabaya yasikufurahishe kabisa. Ukikutana na mambo mabaya ndo pona yako lakini ukikutana na mambo mazuri na matamu utamsahau mwenza wako na kumwona si kitu, hana chochote, Anakera , Anaboa, Hukuchagua chaguo sahihi na mambo mengine kibao.
Mapenzi ni sanaa, kila mtu anastyle yake, ufundi wake na ujuzi wake wa kuishi na mpenzi wake. Hivyo mmoja wenu akijiingiza kwenye usaliti basi ombea akutane na mambo mabaya akikutana na tamtam ndoa itayumba kila siku.
Ili ndo iwe ya Aman, Upendo na Furaha jambo kumwa la kufanya ni kuepuka kujihusiaha na michepuko, hiyo ndiyo nguzo kubwa na silaha kubwa kwa wanandoa mtakuta ndoa yenu kila siku ina furaha na Amani. Jitahidini kumfanya mwenzako asiwe na wazo la kusaliti ndoa kwa kumwonesha mapenzi ya kweli na kumfanya mda wote afurahie penzi lako. NDOA BILA MICHEPUKO INAWEZEKANA.