Kama unafanya mambo haya basi haujaelimika

DELETED ACCOUNT

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2010
Posts
9,805
Reaction score
15,470
Wengi wana mtazamo kuwa elimu au kuelimika maana yake inaishia kwenye kuelewa, kufikiri au kujadili mambo.

Lakini kuna mambo muhimu katika maisha ambayo mtu mwenye elimu au aliye elimika inamsaidia na kumfanya tofauti na yule ambaye hajaelimika.

Kukosa nidhamu - Ukipitia shule na kweli ukaelimika unajifunza kuwa na nidhamu ya muda, kazi na mali za wengine. Mazingira na mahitaji ya shule yanakufundisha kuheshimu hivyo vitu kiasi kuwa ukihitimu elimu yako yale mazoea yanabaki na wewe.

Kusahau mambo - Mtu aliye elimika hauhitaji kumkumbusha mambo mara kwa mara. Shule inakujengea mazoea ya kukumbuka vitu, hivi hivi inakula kwako.

Kutokuwa Mkweli - Shule inakufundisha kusema ukweli na kufanya mambo yenye maadili. Ndiyo maana mimi naamini kudanganya katika mitihani ni jambo ambalo taifa na hata wanafunzi wenyewe inabidi waliepuke sana kwa sababu linaacha doa lisilofutika kwenye kujiamini na roho ya mtu. Watu walioelimika hawafanyi mambo kwa vificho wala hawahitaji kusimamiwa ili wafanye mambo kwa usahihi.

Nakumbuka wakati nakaribia kufanya mitihani yangu ya Form 4, bro wangu aliniuliza kama anitafutie papers zilizovuja mimi nikakataa. Kwenye mtihani nilipasua vile vile na nadhani 'ningechungulia' ingeniathiri sana kisaikolojia mpaka leo.

Hitimisho: Baada ya kusema hayo utaona kuwa kuna ambao wamepitia shule lakini kiukweli hawajaelimika.

Kuanzia sasa, ukiacha kuangalia tu uwezo wa mtu kuelewa na kuchanganua mambo unaweza pia kutumia vigezo hivyo kutambua mtu aliye elimika na ambaye bado.
 
Hapo kwenye ukweli hapo mmmmh maana wakati mwingine inatulazimu kuongopa ili mambo yaende
 
Wengi wana mtazamo kuwa elimu au kuelimika maana yake inaishia kwenye kuelewa, kufikiri au kujadili mambo.

Lakini kuna mambo muhimu katika maisha ambayo mtu mwenye elimu au aliye elimika inamsaidia na kumfanya tofauti na yule ambaye hajaelimika.

Kukosa nidhamu - Ukipitia shule na kweli ukaelimika unajifunza kuwa na nidhamu ya muda, kazi na mali za wengine. Mazingira na mahitaji ya shule yanakufundisha kuheshimu hivyo vitu kiasi kuwa ukihitimu elimu yako yale mazoea yanabaki na wewe.

Kusahau mambo - Mtu aliye elimika hauhitaji kumkumbusha mambo mara kwa mara. Shule inakujengea mazoea ya kukumbuka, vitu hivi hivi inakula kwako.

Kutokuwa Mkweli - Shule inakufundisha kusema ukweli na kufanya mambo yenye maadili. Ndiyo maana mimi naamini kudanganya katika mitihani ni jambo ambalo taifa na hata wanafunzi wenyewe inabidi waliepuke sana kwa sababu linaacha doa lisilofutika kwenye kujiamini na roho ya mtu. Watu walioelimika hawafanyi mambo kwa vificho wala hawahitaji kusimamiwa ili wafanye mambo kwa usahihi.

Nakumbuka wakati nakaribia kufanya mitihani yangu ya Form 4, bro wangu aliniuliza kama anitafutie papers zilizovuja mimi nikakataa. Kwenye mtihani nilipasua vile vile na nadhani 'ningechungulia' ingeniathiri sana kisaikolojia mpaka leo.

Hitimisho: Baada ya kusema hayo utaona kuwa kuna ambao wamepitia shule lakini kiukweli hawajaelimika.

Kuanzia sasa, ukiacha kuangalia tu uwezo wa mtu kuelewa na kuchanganua mambo unaweza pia kutumia vigezo hivyo kutambua mtu aliye elimika na ambaye bado.
Upo sahihi kabisa mtoa uzi, maana ni kweli mtu anayeitwa msomi lazima aishi kulingana na mafundisho (kuiishi elimu yake) kinyume na hapo huyo atakuwwa hajaelimika. Thumbs up to you!!
 
Back
Top Bottom