Mchokoo
JF-Expert Member
- Jul 28, 2015
- 1,179
- 1,579
Wanabodi nimewaza sana kuhusu ajira hii ya Urais, ambayo huko nyuma hayati baba wa taifa aliwahi kukiri kuwa kwa mtu mwaminifu kazi hii ni mzigo mzito!
Ingawa katika mada hii mahali nilipojikita mimi siko alikosemea mwalimu wakati ule.
Mwee!
Ndugu zangu nami niseme urais si kazi rahisi kama vile wengi wanavyodhani.
Kwa mfano wengi ni mashahidi wa jinsi rais wetu wa awamu hii anavyosemwa kwenye vijiwe au pengine katika mitandao ya kijamii, iwe kwa ukweli au kwa uwongo, hakika nimekubali kwamba kazi hii haipatani kabisa na mtu asiyeitawala hasira yake!
Naomba nieleweke vizuri; natumia neno mtu asiyeitawala hasira yake, na si mtu asiye na hasira kabisa!
Hii ni kwa sababu kimaumbile; hakuna mtu asiye na hasira, na ukikuta mtu wa aina hiyo elewa kuwa hicho ni kilema na si hali ya kawaida.
Ifahamike kuwa hasira ni kitu chema kama ulivyo upendo, ilimradi tu itumike mahali pake na kwa wakati wake. Na kwa sehemu kubwa hapa ndiyo zao la hasara au faida ya hasira linapobainika ndani ya mtu yeyote!
Kwa maendeleo ya nchi yetu taifa linamuhitaji kiongozi mwenye upendo ingawa vilevile tunamuhitaji kiongozi mwenye hasira iliyodhibitiwa, au tuseme kutawaliwa.
Kwa maana nyingine namaanisha hivi baba akiiendesha hasira yake nyumbani wengi watatamani kuishi hapo, lakini ikitokea hasira inamuendesha baba hilo ni tatizo kubwa na watu wa nyumba hiyo wanapaswa kuhamia kwa ndugu na majirani.
Sasa basi kwa nature ya kazi ya uongozi usio wa kifalme kama huu tulionao. Endapo kuna mtu ana njozi za kuwa rais katika siku za usoni basi ni vizuri huyo mtu aanze sasa mazoezi ya kuitawala hasira yake mwenyewe.
Akifaulu mtihani huo hapo ndipo aje ili tumkabidhi kazi hii ya Uamirijeshi mkuu!
Naam mwenye zana zote za kivita lakini ambaye hatatumia uwezo huo dhidi ya wakosoaji wake!
Jamani mbona kazi hii imekaa kimtego-mtego hivi?
Unasemwa na watu unaoweza kuwashughulikia!
Ukiwashughurikia kwa hasira isiyotawaliwa unaboronga zaidi, hasa pale atakapoamua kufuatilia kila jambo linalosemwa!
Ama kweli haka kamchezo hakataki hasira!
Sent from my itel_it1701 using JamiiForums mobile app