Kama umepitia jandoni Pitia hapa tuwasimulie vijana Dar

Hayo mambo ya ki analojia tupilia mbali sasa hivi ni kidigitali...unaenda hospitali wanakupiga ganzi wanakata bila hata maumivu..unashonwa unarudi home wala supu kwa sana unajenga mwili..mwishon unaenda kutoa nyuzi kitu nale nale
Siku hizi hakuna nyuzi. Wanatumia ring
 
Hayo mambo ya ki analojia tupilia mbali sasa hivi ni kidigitali...unaenda hospitali wanakupiga ganzi wanakata bila hata maumivu..unashonwa unarudi home wala supu kwa sana unajenga mwili..mwishon unaenda kutoa nyuzi kitu nale nale
C ndio maana vijana wengi wanagongwa cku hiz wamelegea Kama Mlenda wanachojua ni kwenda kuoshwa miguu tu saloon
 
Sasa hapo kipya kipi??? Yote hayo yakawaida saana......watu wa mkoani mnakosa usingizi Kwa ajili ya dar,.....vip Shem atakuja dar likizo??
Sizungumziii kitu kipya nazungumzia vya ambavyo sisi tulivukuta
 
Swali kubwa kwake ni "Alijuaje??"

Mwanaume anayefuatilia maisha ya mwanamme mwenzie anakuwa na chembechembe zote za u"Elton John"
Ulienda jando?
Afu msiwe mnakata bila ridhaa yetu jamani sisi si ndo watumiaji au?
 
Kwanza natanguliza salaamu kwenu.

Katika vitu ambavyo siwezi kuvisahau katika maisha yangu ni Jando, hii inapelekea nikiona damu tu nakumbuka.

Kwanza nilitahiriwa kipindi najua mema na mabaya,
pili nilitahiriwa bila ganzi,
tatu nilitahiriwa polini,
nne sijawai kubembelezwa pindi tu nilipotahiliwa, maneno ambayo nilikuwa Nayasikia, acha kulia mwanaume wewe, na maneno mengine.

JAmani jandoni si mchezo nilikaa mwezi mmoja na nusu, nikiuguza kidonda polini, unalazimishwa kutoa bandeji bila ya ganzi, unapewa athabu ngumu bila Sababu za M singi, unanyimwa chakula ambacho wazazi wako wamempa mtu unayekaa nae, ye akipewa anakula chakula mbele yako na unaambiwa nenda katafute, unaenda kuchimba mizizi na kuua wanyama wadogo kama sungura ndio chakula chako.

Jandoni tunafundishwa jinsi ya kuishi na mwanamke, ndio mana ni Mara chache kumsikia mtu aliyepitia jandoni analalamika juu ya wanawake,

Tunafundishwa Heshima, tunafundishwa kujitegemea na kusimama kama mwanaume sehemu yoyote,
Tunafundishwa kuwa Msiri, (hata hapa nimevunja sheria ya jando)

na mambo mengine mengi zikiambata na adhabu

Hebu tiririka kitu usichokisahau jandoni, vijana wetu Wajue
Jando ni shiiiida ila ndo umahirii unapo patikanaa
 
Hongera Sana mkuu umenikumbusha ciku hiyo tulichomolewa mida ya alfajiri kuelekea kwa Nkariba.,,,,,,,,,,, ciwez kusimulia yote ila tulirudi hom tunachechemea ambapo kilichofuata ni kuishi kwa babu na kuhudhuria nyimbo za jando kila jioni kwa takriban ciku 30,,,,,,,,,,ni mengi ila naomba kutia nanga. Asante kwa uzi mzuri
 
Karibu tena mkuu

Sent from my SM-J110H using JamiiForums mobile app
 
Nakumbuka tulipokuwa darasa nne tulitoroka shule tukielelekea polini kuvizia ili tuchungulie kwenye kambi ya jando, tulipokaribia tu, tulifukuzwa na wazee hatimae walitukamata na kutupeleka kambini ili tutailiwe, wazazi wetu walipewa taarifa tu, baada ya kutailiwa.
 
Jandoni wanaenda wale waliokulia kule Mgwashi ,itilima ,nanjilinji na vijiji vya ndani nadani huko nkasi na kibindo au simuyu heheheheh

Sie Wa dar baba zetu walikuwa wanatupelea aghakhan kutahiriwa mawaidha tunapewa pale bar ya udassa club tukishushia na kiepe yai na nyama ya kuku kisha tunaenda kubembea hahahahha

Usimaindi ni maisha tu
 
Tittle yako ilipaswa iwe hivi
KAMA UMEPITIA JANDONI PITIA HAPA TUWASIMULIE VIJANA WA MARA, MWANZA,SHINYANGA,SIMIYU GEITA, N.K
 
Back
Top Bottom