Ngida1
JF-Expert Member
- Aug 25, 2009
- 586
- 206
Watu wengi hawafahamu kuwa huwezi kumchukuwa farasi ukamuambia awaongoze punda, au kumchukuwa paka ukamwambia awaongoze mbwa.
Similarly, huwezi kumchukua mtu ambae tayari ni billionaire na ukamuambia awaongoze watu maskini. Maskini wataongozwa na maskini mwenziwao, kwasababu ndie atakaefahamu shida na taabu zao na billionaire aendelee na biashara zake!
Ukiwa na assets zenye thamani ya kufikia karibu bilioni moja, wewe sio tena katika kundi la Watanzania wengi ambao ni maskini nchini. Sio uwongo kuwa wabunge wetu leo wanapata madonge manono manono, lakini wabunge wangapi leo wana-assets zinazofikia bilioni moja kutokana na kuwa wabunge tu? Wabunge wangapi leo wanazo nyumba, viwanja na vitalu hapa na pale nchini?
Ni kweli kabisa kuwa kutokana na hizi pesa zetu ambazo thamani yake leo ipo chini sana, bilioni moja sio chochote na hata ukiwa unazo hatuwezi kukuita kuwa wewe ni tajiri mkubwa. Tunachozungumzia hapa sio thamani ya assets za mtu, bali hii tabia ya kukusanya assets hapa na pale, kule na huku, hiki na kile.
Mwl Nyerere alikuwa Rais wa nchi hii kwa miaka mingi sana na hata idadi ya miaka wengine hatuikumbuki tena kwa sasa. Alipofariki bado hajakuwa na assets zilizofikia bilioni moja even at today's exchange rate.
Waheshimiwa Memba wa Baraza La Mapinduzi asilia la Zanzibar wote kwa sasa wamefariki, lakini nani katika wao aliacha nyumba, viwanja na vitalu hapa na pale Unguja na Pemba, wakati walikuwa na uwezo wa kuichukuwa Zanzibar nzima kuwa mikononi mwao?
Hivyo hawa hawakuweza kujikopea mamilioni ya pesa kutoka mabenki au kujitafutia nyumba, viwanja na vitalu kila mahali nchini? Of course waliweza, lakini waliamua kuwaongoza wanyonge na wao wakabakia wanyonge ili wajue shida zao vizuri. Hawa ndio walikuwa viongozi wa wanyonge na viongozi wa kweli.
Shida ya maisha na njaa ndio majanga ya kila siku ya wengi wetu nchini na kama haupo katika kaumu yetu basi hutofahamu shida zetu.
Wapo wengine watakaosema kuwa mtu mmoja peke yake atafanya nini? Hesabu huanza na moja, bila ya moja hutopata 2 na bila ya 2 hutopata 3!
Huwezi kuwa kiongozi wa umma na huku una-assets kila corner ya nchi kama yule mfanya biashara wa Hamelin!
Lakusikitisha zaidi ni kuwa, watu wanatumia lugha zile zile za kuwakebehi wanyonge wa nchi hii - yaani lugha za akina Mzee Chenge na Prof Tibaijuka, za Dollar milioni moja kuwa ni vijisenti na Shilingi milioni 10 kuwa ni pesa za mboga tu, wakati wananchi wengi nchini wanatafuta Shilingi elfu kumi kwa kutwa na hawazipati. Nini anakusudia pale mtu anapoeleza eti…" Nina akaunti mbili tu moja benki ya NMB na nyingine benki ya CRDB na zote hazina fedha zaidi ya shs Mil. 15 kila moja."
Ingelikuwa akaunti zote mbili hazina fedha zaidi ya laki tano au milioni moja sote tungelifahamu kuwa hazina kitu, lakini sio chini ya milioni 15! Sasa milioni 15 wewe unaziona ni ndogo? Wangapi wa nchi hii watafika kufariki bila ya kutia machoni mwao milioni 15 seuze kuzimiliki?
Kama mtu anatamani kuiongoza nchi hii siku moja basi ni ruhsa na sisi tunampa hongera. Lakini, kuongoza nchi hakuendi sambamba na kujikusanyia mimali, kwasababu wengi wetu hapa Tanzania ni maskini na mafukara na tungelipenda mtu wakutuongoza afahamu hivyo.
Leo mtu anao ngo'mbe 1000, baada ya miaka 5 ya Ikulu hao ngo'mbe ni lazima watakuwa 50,000 na baada ya miaka 10 hatujui watakauwa idadi gani. Zaidi, kuwa na 1000 heads of cattle is a big headache, hivyo juu yake unataka tena kuengezea 45 million heads of Tanzanians? Kwa kweli, wewe utakuwa ni mtu wa ajabu sana.
Leo mtu anazo assets Kigoma, DSM, Mtwara, baada ya miaka 5 ya Ikulu atakuwa pia na assets na Mwanza, Zanzibar, Arusha, Iringa, Mbeya, etc. Baada ya miaka 10 assets zake zitakuwa katika kila mkoa wa Tanzania.
Kwahivyo, sisi wanyonge - wakwezi na wakulima wa nchi hii, tunatamka waziwazi kuwa, wewe na yule mwenye ng'ombe 1000 zizini kwake hamtufai katika kiny'ang'anyiro cha mwaka huu!
Hii sio kwasababu tunawachukia matajiri, bali ni kwasababu wazee wanasema kuwa dalili ya mvua ni mawingu. Ukiona mawingu, basi mbio mbio kaanue mpunga wako uliouanika nje, else mpunga utakuja kuroa!
Hivi sasa tusharoa chapachapa na kwahivyo hatutaki kuja kuroa tena. Zaidi, safari hii Wazanzibari ni zamu yetu. We are the only ones who can extricate this beautiful country from a quagmire of corruption in which it is now wallowing!
Chanzo: Zanzibar Ni Kwetu