Kama tetesi hizi ni kweli viongozi Simba mtaharibu!

Acha inyeshe....

Tumekubali kubaki na wachezaji wazee acha itugharimu.

Alafu huyu Mangungu anahitaji Bakora siku si nyingi.
 
Wakuu,

Matokeo ya weekend yametuvuruga Simba kuanzia mashabiki, wachezaji, makocha hadi viongozi! Ni kama hakuna anayejua tumekosea wapi.

Kuna tetesi mitandaoni kuwa kocha Robertinho amepewa game tatu kuamua hatma yake, Azam, Vipers in and out. Huu ni uganga wa kienyeji sio hesabu za mpira.

Unapompa kocha mechi tatu, wachezaji wana sehemu gani? Kama kwa unprofessional reasons wachezaji wakiamua kumhujumu kocha? Kwa kipimo kipi kuona huyu kocha mpya ni kocha wa ovyo?

Tunategemea management mlifanya tathimini ya kutosha na kuona huyu atafaa kutengeneza Simba itayotisha misimu kadhaa, Sasa imani yenu imefia wapi ghafla?

Simba main victims wa matokeo mabaya daima ni kocha na hii imejikita hadi kwa mashabiki! Tumeishia kuwa na lundo la makocha hadi aibu! Mnafikiri tatizo ni hao makocha au kichaka cha kuficha udhaifu wa viongozi?

Tusisahau hawa viongozi wamevurunda usajili bora hata Singida Big stars! Wachezaji wote waliosajiliwa wamevurunda! narudia wote kasoro Phiri! Ntibatokiza na Baleke ni dirisha dogo na hapo huyo Baleke hata Mazembe hawamtaki wanamtoa kwa Mkopo tu! Wamemleta Sewadogo hajacheza msimu mzima!

Huyu kocha akirudi leo Vipers alafu tukutane nae Feb 25 hatumuwezi ndio mjue hawa makocha wanaonewa tu. Hata hii Yanga iliyoimarika ni kumvumilia Nabi! Mashabiki wa Yanga walishaona Nabi hawezi hizi game lakini ilikuwa mihemko tu!

Viongozi njooni na mkakati mpya wa scouting ambao tutanunua wachezaji wa maana, lakini pia ili kuepusha hujuma badala ya kumpa kocha mkuu mechi 3 toeni game tatu kwa benchi lote la ufundi na pia wachezaji wakatwe maslahi yao tukitolewa ili uwajibikaji uwe timu nzima sio kuonea kocha mkuu tu.

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
Tatizo kubwa la simba ni umri mkubwa wa wachezaji, Ntibazonkiza Bocco, Kapombe, Majura, Mkudee...
 
Tatizo la simba ni viongozi na sio coach. Hapa naanza kumwelewa babu Zoran Maki . kwamba wachezaji hawana viwango.
 
Kuna kazi kubwa pale kiungo na pia tunahitaji kuwa shape upya Kapombe na Tshabalala wawe bora kwenye ukabaji then kushambulia iwe ni kitu cha pili lakini ulinzi kwanza.

Angalia Nabi alichofanya juzi ambacho kwasisi mashabiki wa Simba tungeua kocha. Umuweke nje Aziz K na sureboy aanze Mudadhiri? Alafu baadae umtoe Bangala aingie Gift?

Sisi Simba tunaharibu wachezaji sana sana, hata Chama kuna muda anacheza ki father na Sakho pia. Tunafanya makocha wawe waoga kwa hawa wachezaji!

Simba wote hadi mashabiki tunapaswa kubadilika, baada ya game ya Raja mashabiki wanataka timu apewe Mgunda! Hivi tuna funza vichwani sisi?

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
Ä°takuwa na mnafunza kichwani mzee, sio bure
 
Makolo yanaruka na kukanyagana yanaruka kinyama×2🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom