Kama Tendwa mungu Aifute CHADEMA tuone basi...

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
34,097
Reaction score
43,309
[h=5][/h][h=5]
tendwa_john.jpg

Kama Tendwa Mungu basi aifute CHADEMA tuone
[/h][h=5] Lula wa Ndali Mwananzela
Toleo la 307
17 Jul 2013

HAKUNA ulevi mzuri; ulevi ni ulevi tu. Uwe ulevi wa wanzuki, tembo, ulanzi au konyagi ulevi ni ulevi tu. Na ulevi wote una sifa moja kubwa – unapoteza uwezo wa mtu kujitawala na unamfanya ajihisi au ajidhani yuko tofauti na alivyo. Ulevi unatengeneza geresha katika kichwa cha mnywaji kwa kumpa mawazo ambayo anaamini ni sahihi kabisa hadi atakapoamka asubuhi na kujikuta amelala kwenye matope. Ulevi unaweza kumfanya mtu na akili zake aage anakwenda kujisaidia haja ndogo nje kumbe amefungua mlango wa kabati! Hakuna ulevi mzuri!

Ulevi wa madaraka nao ni hivyo hivyo; hakuna ulevi wa madaraka ambao ni mzuri. Walevi wa madaraka wanafanana kabisa na walevi wa kileo; wote wanaamini wako zaidi ya walivyo! Tuliimba zamani “Pombe Si Chai amelewa mgandini akatumbukia katika shimo”! Yeye mwenyewe – Pombe Si Chai – alipofika mtaroni badala ya kuruka akiwa karibu aliruka akitokea mbali akidhani mtaro uko mbali, kumbe badala ya kuruka ndio akatumbukia. Ni huyu huyu – Pombe Si Chai – ambaye baada ya kulewa akitoka shambani alijikuta amelala kifudifudi chini ya mti na alivyoshituka usingizini akaona mtu kavaa kofia amemwinamia; bila ajizi alinyanyua shoka lake na kumtwanga mtu yule! Alishituka na maumivu makali kwenye goti kwani aliweka kofia yake mwenyewe! Hakuna ulevi mzuri!

Ulevi ni ulevi tu hata uwe wa madaraka. Walevi wa kileo na wale wa madaraka wamefanana vitu vingi lakini kikubwa ni kuwa wote wanaamini kuwa wanaweza kufanya mambo ambayo hawana uwezo nayo. Mlevi anaweza kufikiri yeye ni ofisa wa JWTZ na kuanza kuwapigisha kwata watoto na mke; mlevi wa madaraka anaweza kufikiria yeye ni ofisa wa JWTZ na kuanza kuwapigisha kwata watumishi walio chini yake. Hapa ndipo tunapoona ulevi wa Msajili wa Vyama vya Siasa nchini John Tendwa.

Tendwa anajiamini yeye ni kama mungu fulani hivi; kwamba ana nguvu za maisha ya kisiasa nchini kiasi kwamba anaweza kuteremsha radi na moto kuwaunguza wote ambao hawataki kukaa sawa na kufuata kile anachoamini ni sheria. Katika kuthibitisha kuwa anajiona yeye mungu, Tendwa amepiga mkwara Chama cha Demokrasia na Maendeleo kuhusiana na mpango wake wa kutoa mafunzo ya ukakamavu na siasa kwa wanachama wake ili kujilinda dhidi ya watu wote wanaojaribu kukidhulumu chama hicho.

Ikumbukwe kuwa siku chache zilizopita CHADEMA kilitoa uamuzi wa Kamati Kuu kuanzisha mafunzo ya ukakamavu kwa vijana katika kambi mbalimbali nchini. Uamuzi huu umekuja baada ya chama hicho kikuu cha upinzani nchini kujikuta kikiwa matatizoni na vyombo vya dola na hasa ukimya wa msajili huyo kukemea vitendo vya uvunjaji amani ambavyo vimekuwa vikifanywa na jeshi la polisi dhidi ya CHADEMA. Baada ya mlolongo wa matukio ya umwagikaji damu mikononi mwa vyombo vya dola – polisi – CHADEMA imejikuta haina ujanja isipokuwa kuja na mfumo wake wa kujilinda na kulinda wanachama na viongozi wake.

Hili ndilo lililomkoroga Tendwa.Yeye hataki CHADEMA wajilinde; anasema wasijilinde wategemee polisi kuwalinda. Ni kana kwamba amekuwa mbuni ambaye hataki kuangalia yanayoendelea pembeni na hivyo kuweka kichwa chake mchangani. Tendwa haamini kabisa kuwa kuna tatizo katika jeshi la polisi na hasa uhusiano wake na CHADEMA. Yeye kama walivyo wana CCM wengine anaamini kuwa matukio ya umwagikaji damu kwenye mikutano ya CHADEMA yamefanywa na CHADEMA. Anaamini kabisa – kwa makosa ya fikra (irrationally) – kuwa CHADEMA wanatakiwa kutii “bila shurti” amri zozote hata za kijinga kwa sababu zimetolewa na polisi. Tendwa anaamini kuwa polisi wanaweza kumuamuru mtu yeyote kufanya lolote, popote na kwa vyovyote tena bila kuulizwa. Na mtu yeyote akiuliza polisi aukuwabishia basi polisi wanaweza hata kumuua! Fikra zake inaonekana hazipishani na mmoja wa mawaziri wakuu dhaifu kabisa katika historia ya nchi yetu – Mizengo Pinda. Mizengo Pinda kama Tendwa anaamini kuwa polisi wanaweza kupiga wananchi kwa sababu yoyote na popote kwa vile tu wananchi wamebisha au kutumia haki yao ya kuipinga serikali. Ipo haki ya kuipinga serikali kama vile ulivyo wajibu wa kuikubali. Pinda akiwa kama mlevi mwingine wa madara – kumbuka ulevi ni ulevi tu na mlevi ni mlevi tu – aliamuru vyombo vya dola kuwapiga wananchi wanaoweza kuwa wanatumia haki yao ya kuandamana au kuipinga serikali. Alisema yale maneno ya kufuru ya demokrasia “nyie wapigeni tu”! Tendwa naye anaonekana ni muumini wa itikadi hiyo ya kilevi!

Lakini nyuma ya hili ni kuwa Tendwa anaamini yeye ni mungu wa aina fulani – hata kama siyo Mungu Mwenye Enzi! Anaamini kuwa kutokana na madaraka yake anaweza kuifuta CHADEMA kwa sababu imethubutu kusema kuwa sasa itaanza kujilinda. Anataka CHADEMA ati ijisalimishe mbele za polisi na isifanye lolote kulinda maisha ya wanachama wake nchini. Kwamba, chama tawala kinaweza kufanya hivyo na tayari kinafanya hivyo lakini CHADEMA wakifanya basi itakuwa nongwa. Ni sawa sawa na ule msemo kuwa ndege wote walie lakini akilia bundi uchuro! CCM ina vijana wake wanaokilinda chama na wameshapewa maagizo mara nyingi kujilinda na kuwalinda viongozi wake na kukilinda chama; Tendwa katika ulevi wake hakuthubutu kusema lolote lakini leo kwa haraka na kwa sauti ya kilevi anasema ati kuwa CHADEMA wakiendelea na mpango wao atakifuta!

Naomba kumthubutisha Tendwa; kama yeye Mungu akifute CHADEMA. Akifute na kwa vile akifanya hivyo hawezi kuhojiwa na yeyote na sheria haimpi madaraka ya kukirudisha. Akifute ili awe katika historia yetu mungu mtu aliyeweza. Kwa vile anaamini ana madaraka na uwezo wa kufanya hivyo kwa mujibu wa sheria basi atumie madaraka hayo badala ya kuwapiga watu mkwara wa kilevi! Anasema kwa sauti kama ya kilevi – nitawafutilia mbali kwa sababu mnataka kushindana na CCM!

Sasa akifute basi kama yeye mungu na tuone kama watu watakwenda kufukiza uvumba na kutoa sadaka kwenye ofisi zake kumbembeleza abadili mawazo; Asiishie kutishia watu maana hii si mara ya kwanza kufanya hivyo. Akifute ili watu wote tuanze kutoa fungu la kumi kwake na kumpeleka maombi yetu; afute ilia one kama Watanzania wataanza kutunga nyimbo za pambio na qasida kumsifia mtukufu mungu wetu msajili! Si inasemwa mtu mzima hatishiwi nyau; na simba hatishiwi kuku! Kwa nini awatishe CHADEMA kama anaweza kufanya kweli; mtu mzima hatishi anafanya kweli kama anataka kufanya kweli.

Lakini tayari tunajua siyo mungu; si amesema kuwa hawezi kuifuta CCM? Kitu ambacho si kweli. Sheria inampa madaraka ya kukifuta chama chochote cha siasa; haisemi ati chama hicho kikiwa madarakani na kikivunja sheria basi hakiwezi kufutwa; kinaweza na anajua kinaweza kufutwa. Tatizo ni kuwa mungu wetu Tendwa hawezi kuifuta CCM kwa sababu itakuwaje kama chama kingine kitaingia madarakani? Atakosa hata ubalozi wa nyumba sabasaba!

CHADEMA waendelee na mpango wao wa kutoa mafunzo – na wakitaka msaada wangu wa kuwaandalia mafunzo nitawafanyia bure kabisa. Na waseme na kumthubutisha msajili kuwa wataendelea na mpango huo halafu tuone Msajili akifute CHADEMA. Halafu akikifuta asiishie kukifuta kwenye makaratasi tu; akifute kwenye mioyo ya Watanzania na akifute kwenye historia ya Tanzania. Asimame na acheke akitutangazia kuwa amekifuta.

Halafu tutajua kuwa yeye mungu!
- See more at:
http://raiamwema.co.tz/kama-tendwa-mungu-basi-aifute-chadema-tuone#sthash.EceTOUPz.dpuf
[/h]
 
CHADEMA kipo miyoyoni mwa watz
uchaguzi wa 2010 nilifikiri ndo mwisho wangu wa kuishi nje
nilijiandaa kurudi nyumbani na kufanya kazi kwa hali na mali kukuza uchumi wa nchi yetu Tanzania
Ndoto zangu zilizimwa gafla niliposikia ikulu imeingiliwa kwa wino wa kalamu
Mungu ibariki CHADEMA Mungu ibariki Tanzania
 
tendwa_john.jpg

Kama Tendwa Mungu basi aifute CHADEMA tuone

Lula wa Ndali Mwananzela
Toleo la 307
17 Jul 2013

HAKUNA ulevi mzuri; ulevi ni ulevi tu. Uwe ulevi wa wanzuki, tembo, ulanzi au konyagi ulevi ni ulevi tu. Na ulevi wote una sifa moja kubwa – unapoteza uwezo wa mtu kujitawala na unamfanya ajihisi au ajidhani yuko tofauti na alivyo. Ulevi unatengeneza geresha katika kichwa cha mnywaji kwa kumpa mawazo ambayo anaamini ni sahihi kabisa hadi atakapoamka asubuhi na kujikuta amelala kwenye matope. Ulevi unaweza kumfanya mtu na akili zake aage anakwenda kujisaidia haja ndogo nje kumbe amefungua mlango wa kabati! Hakuna ulevi mzuri!

Ulevi wa madaraka nao ni hivyo hivyo; hakuna ulevi wa madaraka ambao ni mzuri. Walevi wa madaraka wanafanana kabisa na walevi wa kileo; wote wanaamini wako zaidi ya walivyo! Tuliimba zamani "Pombe Si Chai amelewa mgandini akatumbukia katika shimo"! Yeye mwenyewe – Pombe Si Chai – alipofika mtaroni badala ya kuruka akiwa karibu aliruka akitokea mbali akidhani mtaro uko mbali, kumbe badala ya kuruka ndio akatumbukia. Ni huyu huyu – Pombe Si Chai – ambaye baada ya kulewa akitoka shambani alijikuta amelala kifudifudi chini ya mti na alivyoshituka usingizini akaona mtu kavaa kofia amemwinamia; bila ajizi alinyanyua shoka lake na kumtwanga mtu yule! Alishituka na maumivu makali kwenye goti kwani aliweka kofia yake mwenyewe! Hakuna ulevi mzuri!

Ulevi ni ulevi tu hata uwe wa madaraka. Walevi wa kileo na wale wa madaraka wamefanana vitu vingi lakini kikubwa ni kuwa wote wanaamini kuwa wanaweza kufanya mambo ambayo hawana uwezo nayo. Mlevi anaweza kufikiri yeye ni ofisa wa JWTZ na kuanza kuwapigisha kwata watoto na mke; mlevi wa madaraka anaweza kufikiria yeye ni ofisa wa JWTZ na kuanza kuwapigisha kwata watumishi walio chini yake. Hapa ndipo tunapoona ulevi wa Msajili wa Vyama vya Siasa nchini John Tendwa.

Tendwa anajiamini yeye ni kama mungu fulani hivi; kwamba ana nguvu za maisha ya kisiasa nchini kiasi kwamba anaweza kuteremsha radi na moto kuwaunguza wote ambao hawataki kukaa sawa na kufuata kile anachoamini ni sheria. Katika kuthibitisha kuwa anajiona yeye mungu, Tendwa amepiga mkwara Chama cha Demokrasia na Maendeleo kuhusiana na mpango wake wa kutoa mafunzo ya ukakamavu na siasa kwa wanachama wake ili kujilinda dhidi ya watu wote wanaojaribu kukidhulumu chama hicho.

Ikumbukwe kuwa siku chache zilizopita CHADEMA kilitoa uamuzi wa Kamati Kuu kuanzisha mafunzo ya ukakamavu kwa vijana katika kambi mbalimbali nchini. Uamuzi huu umekuja baada ya chama hicho kikuu cha upinzani nchini kujikuta kikiwa matatizoni na vyombo vya dola na hasa ukimya wa msajili huyo kukemea vitendo vya uvunjaji amani ambavyo vimekuwa vikifanywa na jeshi la polisi dhidi ya CHADEMA. Baada ya mlolongo wa matukio ya umwagikaji damu mikononi mwa vyombo vya dola – polisi – CHADEMA imejikuta haina ujanja isipokuwa kuja na mfumo wake wa kujilinda na kulinda wanachama na viongozi wake.

Hili ndilo lililomkoroga Tendwa.Yeye hataki CHADEMA wajilinde; anasema wasijilinde wategemee polisi kuwalinda. Ni kana kwamba amekuwa mbuni ambaye hataki kuangalia yanayoendelea pembeni na hivyo kuweka kichwa chake mchangani. Tendwa haamini kabisa kuwa kuna tatizo katika jeshi la polisi na hasa uhusiano wake na CHADEMA. Yeye kama walivyo wana CCM wengine anaamini kuwa matukio ya umwagikaji damu kwenye mikutano ya CHADEMA yamefanywa na CHADEMA. Anaamini kabisa – kwa makosa ya fikra (irrationally) – kuwa CHADEMA wanatakiwa kutii "bila shurti" amri zozote hata za kijinga kwa sababu zimetolewa na polisi. Tendwa anaamini kuwa polisi wanaweza kumuamuru mtu yeyote kufanya lolote, popote na kwa vyovyote tena bila kuulizwa. Na mtu yeyote akiuliza polisi aukuwabishia basi polisi wanaweza hata kumuua! Fikra zake inaonekana hazipishani na mmoja wa mawaziri wakuu dhaifu kabisa katika historia ya nchi yetu – Mizengo Pinda. Mizengo Pinda kama Tendwa anaamini kuwa polisi wanaweza kupiga wananchi kwa sababu yoyote na popote kwa vile tu wananchi wamebisha au kutumia haki yao ya kuipinga serikali. Ipo haki ya kuipinga serikali kama vile ulivyo wajibu wa kuikubali. Pinda akiwa kama mlevi mwingine wa madara – kumbuka ulevi ni ulevi tu na mlevi ni mlevi tu – aliamuru vyombo vya dola kuwapiga wananchi wanaoweza kuwa wanatumia haki yao ya kuandamana au kuipinga serikali. Alisema yale maneno ya kufuru ya demokrasia "nyie wapigeni tu"! Tendwa naye anaonekana ni muumini wa itikadi hiyo ya kilevi!

Lakini nyuma ya hili ni kuwa Tendwa anaamini yeye ni mungu wa aina fulani – hata kama siyo Mungu Mwenye Enzi! Anaamini kuwa kutokana na madaraka yake anaweza kuifuta CHADEMA kwa sababu imethubutu kusema kuwa sasa itaanza kujilinda. Anataka CHADEMA ati ijisalimishe mbele za polisi na isifanye lolote kulinda maisha ya wanachama wake nchini. Kwamba, chama tawala kinaweza kufanya hivyo na tayari kinafanya hivyo lakini CHADEMA wakifanya basi itakuwa nongwa. Ni sawa sawa na ule msemo kuwa ndege wote walie lakini akilia bundi uchuro! CCM ina vijana wake wanaokilinda chama na wameshapewa maagizo mara nyingi kujilinda na kuwalinda viongozi wake na kukilinda chama; Tendwa katika ulevi wake hakuthubutu kusema lolote lakini leo kwa haraka na kwa sauti ya kilevi anasema ati kuwa CHADEMA wakiendelea na mpango wao atakifuta!

Naomba kumthubutisha Tendwa; kama yeye Mungu akifute CHADEMA. Akifute na kwa vile akifanya hivyo hawezi kuhojiwa na yeyote na sheria haimpi madaraka ya kukirudisha. Akifute ili awe katika historia yetu mungu mtu aliyeweza. Kwa vile anaamini ana madaraka na uwezo wa kufanya hivyo kwa mujibu wa sheria basi atumie madaraka hayo badala ya kuwapiga watu mkwara wa kilevi! Anasema kwa sauti kama ya kilevi – nitawafutilia mbali kwa sababu mnataka kushindana na CCM!

Sasa akifute basi kama yeye mungu na tuone kama watu watakwenda kufukiza uvumba na kutoa sadaka kwenye ofisi zake kumbembeleza abadili mawazo; Asiishie kutishia watu maana hii si mara ya kwanza kufanya hivyo. Akifute ili watu wote tuanze kutoa fungu la kumi kwake na kumpeleka maombi yetu; afute ilia one kama Watanzania wataanza kutunga nyimbo za pambio na qasida kumsifia mtukufu mungu wetu msajili! Si inasemwa mtu mzima hatishiwi nyau; na simba hatishiwi kuku! Kwa nini awatishe CHADEMA kama anaweza kufanya kweli; mtu mzima hatishi anafanya kweli kama anataka kufanya kweli.

Lakini tayari tunajua siyo mungu; si amesema kuwa hawezi kuifuta CCM? Kitu ambacho si kweli. Sheria inampa madaraka ya kukifuta chama chochote cha siasa; haisemi ati chama hicho kikiwa madarakani na kikivunja sheria basi hakiwezi kufutwa; kinaweza na anajua kinaweza kufutwa. Tatizo ni kuwa mungu wetu Tendwa hawezi kuifuta CCM kwa sababu itakuwaje kama chama kingine kitaingia madarakani? Atakosa hata ubalozi wa nyumba sabasaba!

CHADEMA waendelee na mpango wao wa kutoa mafunzo – na wakitaka msaada wangu wa kuwaandalia mafunzo nitawafanyia bure kabisa. Na waseme na kumthubutisha msajili kuwa wataendelea na mpango huo halafu tuone Msajili akifute CHADEMA. Halafu akikifuta asiishie kukifuta kwenye makaratasi tu; akifute kwenye mioyo ya Watanzania na akifute kwenye historia ya Tanzania. Asimame na acheke akitutangazia kuwa amekifuta.

Halafu tutajua kuwa yeye mungu!
- See more at:
http://raiamwema.co.tz/kama-tendwa-mungu-basi-aifute-chadema-tuone#sthash.EceTOUPz.dpuf

Hata huyu mwndishi naye mlevi tu sijui anataka kumfurahisha nani, Msajili wa vyama anaweza kukifuta chama chochote na wote wanaojifanya wasemaji kama huyu mwanishi na asiwe na kuandika zaidi ya kulalamika tu.
 
Huyu bwana Tendwa mara nyingi nadhani kuna hatua hakupitia kimakuzi ama uzee umemjia vibaya kwa maana ya kutojiandaa...
 
CHADEMA kipo miyoyoni mwa watz
uchaguzi wa 2010 nilifikiri ndo mwisho wangu wa kuishi nje
nilijiandaa kurudi nyumbani na kufanya kazi kwa hali na mali kukuza uchumi wa nchi yetu Tanzania
Ndoto zangu zilizimwa gafla niliposikia ikulu imeingiliwa kwa wino wa kalamu
Mungu ibariki CHADEMA Mungu ibariki Tanzania

Chadema ni kampuni wewe, acha kuwakebehi watanzania zaidi ya milioni 40.
 
Huyu bwana Tendwa mara nyingi nadhani kuna hatua hakupitia kimakuzi ama uzee umemjia vibaya kwa maana ya kutojiandaa...

Ukubwa jalala, mtamtukana mzee wa watu na ukweli utabaki pale pale kuwa uwezo wa kukifuta chama chochote cha siasa anao
 
Chadema ni kampuni wewe, acha kuwakebehi watanzania zaidi ya milioni 40.

Wewe thatha nakwambia kama Tendwa ni mwanaume na aifute CHADEMA sasa tumwonyeshe kilichomnyoa kanga manyoa ya shingo!
 
Last edited by a moderator:
Kama Tendwa ana Jinsia ya Kiume kweli afute Chadema aone kilichomtoa kanga manyoya.
 
Acha ujinga wako usio na fikira mjinga mkubwa wewe!

Hawa CHADEMA wamechanganyikiwa nini? Badala ya kujitathmini na kubadilika wanaaza kushambulia tamko la msajili wa vyama kuhusu ujinga wao wao.
 
Tendwa mnafiki tu!... Ni mwanaCCM aliyeandaliwa kupiga propaganda za kuua upinzani.
 
Ndo maana wazungu wanatucheka na kutukejeli
hatujajitambua hata haki yako ya msingi huijui'
ccm wameshatunyonya vya kutosha na sasa hivi wanapigana kufa na kupona ili wabaki madarakani
maana nchi walishaiweka rehani muda mrefu
wananchi hadi leo ukiugua huna hospital ya uhakika ya kukutibu
huna uhakika wa elimu bora
huna uhakika wa maji safi na salama hata Obama alipewa angalizo la kutokunywa maji Tz
wewe bado unaendelea kuwa tetea mafisadi wanauza wanyama mchanya kweupe
madini yote wamegawa watz wanakufa kwa sababu ya CN ma Hg hadi wamebabuka usoni huoni hilo
1012371_438654349566543_241317027_n.jpg

Chadema ni kampuni wewe, acha kuwakebehi watanzania zaidi ya milioni 40.
 
Hata huyu mwndishi naye mlevi tu sijui anataka kumfurahisha nani, Msajili wa vyama anaweza kukifuta chama chochote na wote wanaojifanya wasemaji kama huyu mwanishi na asiwe na kuandika zaidi ya kulalamika tu.

Mwanishi ndio kitu gani?
 
Hawa CHADEMA wamechanganyikiwa nini? Badala ya kujitathmini na kubadilika wanaaza kushambulia tamko la msajili wa vyama kuhusu ujinga wao wao.

Wewe ndo pritenda mkubwa, unakuja na viposti vyako vya matango pori,mimi sio mfuasi wa lumumba kwaiyo isijokombe kwangu.
 
Hata huyu mwndishi naye mlevi tu sijui anataka kumfurahisha nani, Msajili wa vyama anaweza kukifuta chama chochote na wote wanaojifanya wasemaji kama huyu mwanishi na asiwe na kuandika zaidi ya kulalamika tu.

Ohh! kumbe ni wewe mlevi wa bangi za ccm..... nsipoteze muda kwako. Garbage !
 
Back
Top Bottom