Kama taifa tutafakari maamuzi ya kiongozi wetu

ego

JF-Expert Member
Apr 10, 2013
1,620
1,407
Tumekuwa tukisikia maamuzi makubwa anayoyafanya kiongozi wetu ya papo kwa papo. mfano wapo wafanya biashara wamepewa maekari ya ardhi, wapo wafanya biashara wanapewa madini wachimbe na kadhalika kupitia hoja ya kujenga viwanda.

kama taifa inabidi tujadili mambo haya na kutizama kama tamaduni hii tunayoifikisha itatufikisha kule tunakotaka kwenda.

kwa mtizamo wangu viongozi wetu wanatakiwa waweke utaratibu wa kushughulikia kila jambo na kusimamia utaratibu huo ufuatwe. Mambo ya viongozi kutumia madaraka yao kuamua ni hatari sana kwa taifa maana humo ndimo viongozi wasiowaaminifu hutumia fursa hizo kufanya maamuzi yasiyonufaisha jamii.

mfano tuna mifano katika jamii yetu katika jambo linaitwa richmond ambako kiongozi mkubwa mwenye cheo alifanya maamuzi na yeye akawa anajitetea kuwa alifanya kutokana na dharura lakini taifa lilipokuja kutafakari maamuzi yale yalionekana kuwa na hasara kwa taifa kuliko faida.

nje ya nchi yetu tunaweza kuona nchi kama korea kusini wamkimtoa kiongozi wao madarakani kwa kuhisi alitumia maamuzi yake kunufaisha baadhi ya makampuni makubwa.

kwa taifa ni vema viongozi wetu wakijikite katika kusukuma wanaohusika kutimiza wajibu wao na pale wanaohusika wanaposhindwa kutimiza wajibu basi watizame sababu nini? kama sababu ni ziko nje ya uwezo wa wahusika basi viongozi wasukume au watatue changamoto hizo na sio kufanya maamuzi wenyewe. kama wahusika wanashindwa kutimiza wajibu wao kwa uzembe basi wawajibishwe na nafasi wapewe watu wenye ujasiri na busara za kufanya mammuzi.

viongozi wakumbuke leo hii wanaweza kuona jambo fulani linachelewa na wakafanya maamuzi kwa kutizama jambo moja lakini kesho kama maamuzi yao yataonekana yalileta hasara kubwa kwa taifa kwa namna nyingine nia yao nzuri haitakaa kuonekana. Lengo la kuweka utaratibu na kutumia wataalamu kufuatilia utaratibu huo ni kuhakikisha wanapofanya maamuzi wanachukua the best interest kwa taifa na wasipofanya hivyo taifa litawauliza.

tuutafakari vizuri utaratibu huu na tujiridhishe kama unajenga au tunatengeneza tamaduni inayoweza kuturudisha tunakotaka kukimbia.
 
Nchi hii ukitaka kujua kila kitu unajitafutia stress tu, sasa uweke na ugumu huu wa maisha yalivyo inahitaji kujitoa mhanga sana
 
Back
Top Bottom