PreGE2025 Kama sio sifa ni nini? Mbunge Musukuma atangaza kuwachangia gharama za kuchukua fomu, watiania wanaolitaka jimbo lake

PreGE2025 Kama sio sifa ni nini? Mbunge Musukuma atangaza kuwachangia gharama za kuchukua fomu, watiania wanaolitaka jimbo lake

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

McLaren

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2025
Posts
889
Reaction score
2,863
Wakuu,

Yaani katika wabunge wenye sifa huyu nae ni namba moja.

Mbunge wa Jimbo la Geita vijijini, anayemaliza muda wake, Joseph Kasheku (Msukuma) ameahidi kuwa atawachangia gharama za fomu wapinzani wake watakaopungukiwa pesa za kuchukua fomu ya ubunge wa jimbo hilo.

Msukuma amesema hayo mbele ya waandishi wa habari mjini Geita mara baada ya kurejesha fomu ya kutia nia kugombe ubunge jimbo la Geita vijiji kupitia Chama Cha Mpainduzi (CCM).

Amesema uzoefu wake wa kisiasa unamfanya ajiamini na asiwe na hofu juu ya mtia nia ama mpinzani yeyote ambaye atajitokeza kuchukua fomu kwa kuwa ni haki ya kikatiba kila mmoja kugombea.

"Nimetangazia watu wote wanaotia nia jimboni kwangu, ukipungukiwa hela ya kuchukulia fomu njoo, ukiwa huna hela nia yako inakutuma kwenda kugombea ubunge njoo, mimi natoa.

msukuma.png
 
Yaaani ana ujinga na ushamba shule hakuna ndio anaona yuko sawa ngoja aliwe kichwa ndio atajua kuwa yye ni mtu mdgo sana jimboni kwako na chamani
 
Back
Top Bottom