Utakapo lipima gunia la mahindi, mchele, viazi or whatever kwenye mezani ukapata mathalan kgs 80.
Na kisha ukachukua pear ya viatu vyenye uzito wa nusukilo takriban , ukaweka juu ya gunia , hapana ubishi mezani lazima itasoma kwa kuongezeka uzito.
Muujiza ama sintofahamu inakuja kwa Binadamu.
Panda mwenyewe kwenye mezani, kisha soma kgs zako , tuchukulie umepata kgs 75 then shuka mezanini , kale Nyama, wali, maembe, bugia na maji & juice .
Hivyo ulivyovila viwe na uzito wa kgs 1.5 hadi 2 kgs hivi , na kisha rejea kupanda mezani upime tena utakachokikuta ni kgs zako zilezile 75 !
Msingi wa swali hapa, ni hii ziada ya kgs ulizozibugia zinakwenda wapi? Na zisiongeze uzito wako?
Kuna miujiza gani?
Vyakula hivyohivyo kabla hujavila ukivibeba kwenye mfuko ukaushikilia mkononi ukajipima kgs zinaongezeka.
Kosa ni kuziweka tumboni ! Zinapotea ! Huko zinapo potelea ndy nataka nielimishwe.
Nawasilisha.