Kama serikali ilitoa bilioni 3.4 kwa maendeleo ya Kilimo 2016/2016,basi kila mkulima alipata 1000!!

iparamasa

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
13,438
14,916
Tunaambiwa kwamba Kilimo kinafanywa na asilimia 70 ya watanzania wote.

Serikali ilitenga bilioni 101 kama bajeti ya maendeleo lakini ilitoa shilingi bilioni tatu point nne!

Kwa hesabu za harakaharaka,asilimia 70 ni kama watanzania milioni 35,kwa hesabu rahisi,kila mkulima kwa mwaka 2016/2017 alipata shilingi elfu

Je tunawatendea haki wakulima ambao ni asilimia 70 ya watanzania wote? Kuna dalili ya mapinduzi ya Kilimo?Tanzania ya viwanda itapata malighafi kutoka wapi?

Na kwa sasa Kilimo sio moja ya vipaumbele vya bajeti,kwa maana halisi asilimia 70 ya watanzania sio kipaumbele,hivyo kuna hatari kubwa ya kutengeneza watu masikini kwa asilimia 70!!
 
Tunaambiwa kwamba Kilimo kinafanywa na asilimia 70 ya watanzania wote.

Serikali ilitenga bilioni 101 kama bajeti ya maendeleo lakini ilitoa shilingi bilioni tatu point nne!

Kwa hesabu za harakaharaka,asilimia 70 ni kama watanzania milioni 35,kwa hesabu rahisi,kila mkulima kwa mwaka 2016/2017 alipata shilingi elfu

0!!

Tanzania ina wakulima milioni 35? Halafu kwa kawaida utaratibu wa bajeti ni kwamba kila mtu anagawiwa hela? Hivi kwanini Watanzania tunapenda sana kutunga matatizo kuliko kuonesha njia? Wewe iparamasa unalima nini, Keyboard?
 
Makadirio hukusoma shuleni?

Taarifa zinasema tanzania kwa asilimia 70 wanajihusisha na Kilimo,au unataka kuniambia 70% wameajiriwa viwandani na maofisini?
 
Kama serkali ina 3.4 bilioni kwa maendeleo ya kilimo, what is your problem? Kama haina zaidi ulitaka ikaibe? Au iprint hela?
 
Makadirio hukusoma shuleni?

Taarifa zinasema tanzania kwa asilimia 70 wanajihusisha na Kilimo,au unataka kuniambia 70% wameajiriwa viwandani na maofisini?
70% ya watu wenye uwezo wa kufanya kazi Je umetoa watoto Wazee wanafunzi walemavu na wasiojiweza?
 
Back
Top Bottom