Thomas Sankra Jr
JF-Expert Member
- Mar 14, 2013
- 418
- 128
- Thread starter
- #21
Wewe ndiyo Msaliti namba moja, kwanza umevunja Sheria za Nchi yetu kwa kuiita Tanganyika wakati hiyo Nchi haipo kuna Nchi moja tu, Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Pili wewe ni Muongo mkubwa, pamoja na changamoto nyingi tulizonazo lkn bado tumejitahidi na tumepiga hatua kubwa tu mbele ukilinganisha na tulikotoka, Mifano hai ipo mingi kuna watu nawajua ambao wametokea Familia maskini kabisa lkn wameweza kusoma mpaka Chuo Kikuu na sasa wamepata kazi na wameondokana na Umaskini, si ajabu hata wewe ukawa mmojawapo!
Idadi ya Wamama wanaozalia Hospitalini imeongezeka kwa maana nyingi vifo vya mama na mtoto vimepungua, vijana wengi tu wanapata kazi wana maisha mazuri ingawaje bado kazi ni kubwa mbele, lkn tunakwenda vizuri!
Hivyo, Acha Uongo na ni najua kwa uhakika wewe hauko Hospitalini na wala haujaumizwa, ila uko hapa kuwakebehi wale waliokufa na kuumizwa kwa manufaa yako binafsi, wewe ndiyo moja ya wachochezi wakubwa mnaokaidi Sheria za Nchi kwa kwenda kinyume na Matakwa ya Serikali (Halali), Acha uchochezi waache marehemu wa watu wapuumzike kwa Amani na usijali zamu yako kwenda Hospitalini itafika tu!
ahsante sitakujibu hata moja "wameru tuamke usingizini iliboru,tengeru,meru juu na Chini na wote waliopo sehemu mbalimbali ya tanganyika na nje wamezarau mila zetu"