Kama ningekuwa Pinda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kama ningekuwa Pinda

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Lukolo, Mar 7, 2012.

 1. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #1
  Mar 7, 2012
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Hali ya nchi hivi sasa inaelekea siko kufuatia mgomo mpya uliotangazwa na Madaktari. Wataalamu hawa ambao wamesomeshwa kwa gharama kubwa na serikali walimtikisa pinda kipindi kilichopita kiasi cha kumfanya ashuke na kuwa kama piritoni mbele yao. Naunga mkono alichofanya wakati huo kwa kuwa baadhi ya madai yao yalikuwa na msingi.

  Lakini hata baada ya kutekeleza baadhi ya madai yao ya msingi, madaktari hawa wametangaza mgomo mwingine eti kushinikiza serikali imuondoe waziri. Haiingii akilini kabisa. How comes wanaacha kuwahudumia watanzania eti kwa kuwa serikali haijamfukuza waziri? Wana masilahi gani binafsi na huyu waziri hawa madaktari?

  Hapa ndipo ninapotamani ningekuwa Pinda. For sure ningeifunga Mhimbili kwa siku kadhaa na kumfuta kazi daktari yeyote aliyepo kwenye mgomo. Pinda, chukua ushauri wangu ni kazi rahisi tu. Itagharimu maisha ya watanzania kwa muda lakini itarudisha nidhamu ya kazi. Tangaza mgogoro na madaktari Pinda. Tuma vijana wako wachunguze na kuorodhesha wale wote waliopo kwenye mgomo, na jioni ya leo tangaza kuwafukuza kazi hawa wote, wanyangánye hati za kusafiria, halafu kesho tangaza upya nafasi ya ajira katika udaktari, ukitoa nafasi kwa applicant kutoka popote duniani.

  Tanzania kwa sasa ni moja ya nchi inayowalipa vizuri madaktari wake ukilinganisha na baadhi ya nchi. Uwezekano wa kupata madaktari kutoka nchi nyingine ni mkubwa pia. Lakini kwa kuwa hawa waliofukuzwa watakuwa hawana hati za kusafiria na hivyo hawawezi kuonmba kazi nje ya nchi, ni dhahiri kwamba wataomba kazi nchini (hizo mpya utakazozitangaza). Lakini mara hii wakianza kwa mkataba mpya wenye mashariti magumu. Kama zilivyo sheria za kazi, wakifukuzwa kazi itamaanisha kwamba na stahili zao zote zimepotea (isipokuwa katika mashirika ya hifanyi ya jamii). Hili linaweza kuwa fundisho kwa hawa wataalamu wanaochezea maisha ya watanzania.

  Hivi na walimu wangekuwa wakatili kama mlivyo nyie madaktari watoto wenu wangepelekwa wapi? Real I wish I was Pinda. Kwa hakika ningekubali vifo vya watanzania kwa siku mbili ili kurudisha nidhamu kazini. Haisaidii kuendelea kuwabembeleza huku watu wakipoteza maisha. Hawa jamaa wanalipwa vizuri kuwashinda wafanyakazi wengi wa serikali katika secta nyingine lakini wakorofi kama nini? Ni vema watanzania pia tukaisaidia serikali kuwapinga hawa madaktari waliokosa ustaarabu na uzalendo mbele ya watanzania. Mnawaua watanzania kwa ajili ya kutaka waziri afukuzwe? Magaidi wakubwa nyie.

  Pinda tangaza mgogoro na hawa wahuni wanaotaka kuiweka serikali yako mfukoni.
   
Loading...