njundelekajo
JF-Expert Member
- Dec 26, 2012
- 310
- 227
...KAMA NINGEKUA FREEMAN ELIKAEL MBOWE...
Ningechagua siku moja ya mwezi Januari 2019,ningeamka asubuhi sana siku hiyo kuliko kawaida yangu inaweza kua saa kumi na moja alfajiri hivi.Ningefanya mazoezi ya kuuweka sawa mwili wangu kwa muda wa dakika 30.
Saa kumi na moja na nusu ingenikuta sebuleni kwangu nimekaa peke yangu natafakari maisha yangu ya miaka 23 ya kisiasa sanjari na umri wa chama ninachokiongoza cha Chadema.Ningerudisha nyuma fikra zangu mpaka mwaka 1992 nilipoingia CHADEMA wakati huo nikiwa na umri miaka wa 32.
Ningehamisha mawazo yangu na mpaka wakati huu nikiwa na miaka 58 ya umri wangu na miaka 14 ya uenyekiti wangu wa chadema taifa.Nitaikumbuka Jumatatu ya tar 25/4/2008 siku ya kifo cha Chacha Wangwe kilivyonipa wakati mgumu,nitakumbuka nilivyoahidi kuwataja waliorusha bomu kwenye mkutano wa Arusha lililolipuka tareh 15/6/2013 saa 11 na dakika 50 jioni baada ya Mimi kushuka jukwaani.Nitakumbuka mpaka sasa sijawataja kama nilivyoahidi.
Nitaikumbuka Chadema ya Dr slaa,Chadema iliyoaminika na watanzania hata kupuuza amri halali za jeshi LA polisi kuhusu mandamani.Kabla sijakumbuka kifo cha Daudi Mwangosi kule Nyororo Iringa mwaka 2012 ,nitazipelekea hisia zangu tareh 5/januari mwaka 2011 kwenye mgogoro wa umeya Arusha na damu iliyomwagika siku hiyo.
Nitakumbuka namna nilivyomshughulikia Zitto Zuberi Kabwe.Ningejiuliza yupo wapi mwenyekiti wangu wa bavicha taifa Patrobas Katambi,vijana wangu niliowalea ndani y chama kina Moses Machali,David Kafulila,Mwita Waitara,Juliana Shonza,Mtera Mwampamba,James Mwakubinga.Ningetafakari sababu walizozitoa wakati wanaondoka Chadema
Itakua inakaribia saa kumi na mbili sasa ,nitanyanyua cm yangu na kumtumia ujumbe mfupi katibu wangu wa zamani a chama taifa Dr Wilbroad Slaa "tusameheane sana sana sikufikiria kwa kiasi gani ulikua sahihi kwa wakati ule" .Nitatuma ujumbe mwingine mfupi kwa afisa habari wa chama kamanda Tumaini Makene "naomba utoe taarifa kwa waandishi wa habari wote kua nitakua na press comference saa nne kamili asubuhi ya Leo makao makuu ya chama mtaa wa Ufipa Kinondoni"
Nitaingia ndani kujiandaa,nitavaa suti yangu nyeusi na Miwani yangu ya siku zote.Sitohitaji kupata kifungua kinywa .Nitamuita dereva wangu anifuate kunipeleka kwa katibu mkuu wa sasa Dr Mashinji .
Itakua imefika saa mbili sasa wakati nipo nyumbani kwa Dr Mashinji.Kwenye mazungumzo yetu nitamwambia kuhusu mkutano wangu na waandishi wa habari saa nne asubuh ya Leo.Sitomwambia nataka kuongea nini,hatoshangaa kwakua si mara ya kwanza mimi kufanya hivyo.Nitaawambia yeye na naibu katibu mkuu bara John Mnyika waje kwenye mkutano huo.
Saa tatu na nusu nitakua nimewasili mbele ya jengo la makao makuu ya chama ninachokiongoza.Nitasalimiana na waandishi wa habari na vijana na wapambe kadhaa wanaoshinda mbele ya ofisi za chama.Baadae nitaketi na kuanza rasmi mkutano wangu na waandishi wa habari.
Ningeweza tai yangu vizuri shingoni ,na kukohoa kidogo kurekebisha mikwaruzo ya sauti na kisha ningeanza kuzungumza Ndugu waandishi wa habari nimewaiteni kwenye mkutano huu kuzungumza na Wana chadema wote pamoja na watanzania kupitia ninyi.
Mkutano huu na ninachotaka kukizungumza hakijapitia mchakato wa chama na wala hakuna kiongozi yoyote wa Chadema anayejua nataka kuongea nini.Nimefanya hivi makusudi kwa sababu ya kutotaka mjadala mrefu katika jambo lenye maslahi mapana na taifa langu.
Lakini pia nimefanya hivi kwa sababu si mara ya kwanza mimi kutoa matamko ya chama pasipo kupitia vikao vya ndani vya chama,isitoshe mimi sitokua kiongozi wa kwanza wa upinzani kufanya hivi.Ikumbukwe miaka ya nyuma katibu wa chama cha wananchi CUF,Maalim Seif amekwisha wahi fanya wakati wa makubaliano yake juu ya serikali ya maridhiano na rais Ambi Karume.
Ndugu zangu waandishi wa habari pamoja na watanzania mnaonisikiliza sasa,chadema ni chama cha demokrasia na maendeleo. Kwetu sisi maendeleo na demokrasia ndio msingi wa imani na itakadi ya chama chetu.
Sio siri tena kwamba rais John Pombe Magufuli anaingia kwenye kundi la viongozi bora kabisa kuwahi kutoka katika nchi yetu .Hii inatokana na ukweli kwamba miradi mingi ya maendeleo iliyoshindikana kipindi cha nyuma imewezekana chini yake.
Ingawa natambua wenzangu ndani ya chama hawatanielewa ,lakini chadema kama chama kinachoamini katika maendeleo hakina sababu yoyote ya kupingana na serikali ya awamu ya tano.
Sambamba na hilo,kutokana na chama hiki kuendelea kupinga maendeleo ya wazi yanayofanywa na rais Magufuli ,tumepata athari kubwa sana kwa kukimbiwa na wanachama ,wabunge na viongozi wetu wengi waliojiunga na chama cha mapinduzi.
Hivyo basi kuanzia sasa ,mimi kama mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo natoa rai na wito kwa viongozi ,wabunge na wanachama wa Chadema nchi kuungana na rais Magufuli katika kuliletea taifa hili maendeleo. Nichotaka nieleweke kua sijasema nimejiunga na Chama cha mapinduzi au kuwataka watanzania woote wajiunge nacho ninachosema CHADEMA kama chama makini tumeamua kutoa pongezi rasmi kwa rais Magufuli kwa kasi ya maendeleo anayoyasimamia.Aksanteni sana na kwaherini.Sitohitaji swali toka kwa muandishi yoyote yule.
Baada ya kumaliza mkutano wangu na waandishi wa habari nitaelekea Ikulu kuzungumza na rais John Pombe Magufuli. Mazungumzo yetu yatakua siri .Tukimaliza mazungumzo yetu tutapiga picha ya pamoja tukishkana mikono.
Nitajisemeza kimoyo moyo "kila Masika na Mbu wake" kisha nitawapungia waandishi wa habari wakati natoka kwenye geti la Ikulu kuelekea kwangu kabla sijaaanza safari kesho yake kwenda jimboni kwangu Hai kuwahudumia wapigankura wangu walionikosa kwa takribani miaka 4 niliyokuwapo Dar-Es-Salamm kushindina na dola na kuongoza kampeni za kupinga kila kitu.
Noel Nguzo.R.