Kama ndiyo hivi, unene ni mateso!

Gaddaf i06

JF-Expert Member
Nov 14, 2022
1,759
2,795
Habari za wakati huu,

Jamani kuna unene mwingne unatuweka katika wakati mgumu sana aise!

Juzi kati hapa kaja jamaa fulani kununua nguo, mnene kwelikweli. Basi nguo alizohitaji, hakupata size yake, nikamwelekeza kwingine.

Baada ya muda (kama masaa 2) alirudi akidai hajafanikiwa . Dah, basi nikamshauri akaonane na mafundi, huyoo na tape yake.

Jana kaja mwingne tena wa aina yake, kazunguka wee holaa!
. Badae akafanikiwa kupata baadhi kwa jamaa yangu hapo.

Jamaa amekuja kunisimulia kwamba kamuuzia kwa bei ya tikitaka! (bei aliyotamka muuzaji haikupingwa) nahisi ni kutokana na kuzunguka kwa muda mrefu bila mafanikio, kwakweli jamaa kanyanyasika!


...hapana..
KATAA UNENE!
 
kweli mkuumaana waweza kuwa bonge mwepeesi!
images_1671023098780.jpg

91 kg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom