Kama Mwigulu angekuwa raisi wa nchi, angeshasaini kunyongwa wafungwa wote wanaosubiri kunyongwa

Kama wewe sio mwigulu basi utakua mke wake au mpenzi wake au king'asti wake

Hapana mi sipo katika hao unaowataja na wala sio fans wake pia,ila ni bora kuwekana sawa kuna faida gani kukurupuka na kuanzisha uzi kwa yale unayoyawaza tu ambayo hujafanya uchunguzi wowote wa kina hii tabia tukiiendekeza haitaijenga JF.
Kumbuka uwepo wa JF ni mwiba kwa watendaji wengi ambao hawapo sawa katika mambo yao au nyadhifa zao.Hatuna haja ya kuiweka rehani na kuwapa sababu ya kuiondoa au kuanzishwa kwa sheria ngumu zitakazotufanya tushindwe kuwa na uhuru tulionao sasa.
Tusiwe kama madereva wa Tanzania ambao wameshindwa kusoma alama za mwendo kasi mpaka wawekewe matuta ili kupunguza spidi, ustaarabu ni kitu pekee kinachotutofautisha na wanyama.Mwenzio akikosea muelekeze usimpe kichwa kwakuwa athari yake haitaishia kwake tu yaweza kuja hata kwako.
 
Kama kawaida yako unakurupuka kwa majibu mepesi, Mi nimejiunga muda mrefu sana tangu enzi za Jamboforums.Ila nina ID nyingi na hainifanyi niandike kipuuzi kama uandishi wako wewe.JF haikuanzishwa ili kupaka watu matope bila sababu za msingi,ingekuwa hivyo hata isingefika hapa ilipo.Hiki sio kijiwe cha kahawa, ni jukwaa la manufaa na linaheshimika.
Acha uongo na unafiki!Huyo unaemtetea si ndio kinara wa kupaka watu matope!

Usitufanye wajinga!
 
Hapana mi sipo katika hao unaowataja na wala sio fans wake pia,ila ni bora kuwekana sawa kuna faida gani kukurupuka na kuanzisha uzi kwa yale unayoyawaza tu ambayo hujafanya uchunguzi wowote wa kina hii tabia tukiiendekeza haitaijenga JF.
Kumbuka uwepo wa JF ni mwiba kwa watendaji wengi ambao hawapo sawa katika mambo yao au nyadhifa zao.Hatuna haja ya kuiweka rehani na kuwapa sababu ya kuiondoa au kuanzishwa kwa sheria ngumu zitakazotufanya tushindwe kuwa na uhuru tulionao sasa.
Tusiwe kama madereva wa Tanzania ambao wameshindwa kusoma alama za mwendo kasi mpaka wawekewe matuta ili kupunguza spidi, ustaarabu ni kitu pekee kinachotutofautisha na wanyama.Mwenzio akikosea muelekeze usimpe kichwa kwakuwa athari yake haitaishia kwake tu yaweza kuja hata kwako.

Aliyekosea ni nani kati ya ccm wezi, mafisadi, waongo nk na cdm waliomnyima zito madaraka kwa kugundua ni kibaraka
 
Kama umefuatilia mwenendo wa mwanasiasa huyu hasa kwa kutazama matukio anayotuhumiwa kuhusika nayo,kauli na michango yake pale mjengoni, ni dhahiri utaridhika na kuamini kuwa ni mtu mwenye roho ngumu na pengine amekosa "ubinadamu".

Pale mjengoni zikiletwa sheria kandamizi lazima aunge mkono!Ikija hoja kuhusu mauaji atatetea wauwaji. Hata waliouwawa katika mikutano ya chama X sehemu mbalimbali nchini hakosi kutajwa!

Huyu jamaa akishika dola,wafungwa wa kisiasa watakuwa mamia na wengi wataishia jela kama sio kuuwawa.

Kwa maneno machache tu,huyu jamaa akibahatika kuingia pale magogoni cha kwanza itakuwa kusaini wafungwa wote wanaosubiri hukumu ya kifo wanyongwe.Kwa jinsi navyomuona,akiletewa document kama hiyo atasaini mara moja huku akitabasamu.

Huyu ni mtu ambae damu ikimwagika kwake sio issue na ndio maana hata ile sheria kandamizi ya mwaka 1976 kuhusu .... aliunga mkono ipitishwe pale mjengoni!
Nyinyi ndo mnaompa kichwa Mwigulu mpenda sifa. UNAWEZAJE KUMDHANIA ETI ANAWEZA KUSHIKA DOLA? Yeye anajitambua kuwa hana lolote, lkn kwa maneno yenu haya ndo maana anajisifu kuwa eti ni mchumi daraja la kwanza. misifa inamjaa. Huyu mtu hana lolote, kazi ni kujionyeshaonyesha tu na kujifanya anamikakati. hana lolote
 
Back
Top Bottom