CAPITALMAN
Member
- Jul 25, 2013
- 20
- 14
Hello wanaJF wenzangu, jambo nalotaka kushare nanyi leo ni mtazamo wangu juu ya nini kinachotokea hivi sasa katika kampeni za kuomba kura kuelekea Octobner 25 ambapo watatnzania tutakuwa tukipiga kura, kuwacahagua viongozi wetu watakaotuongoza ktk kusababisha maendeleo ya nchi yetu kwa miaka mitano ijayo.
Hili si jambo dogo hata kidogo na ambalo halipaswi kupuuzwa, ukifuatilia sera za mgombea wa CCM utagundua kwamba anakiri kwamba ccm katika uongozi wake, haikuweza kufanya yaliyowaahidi watanzana kwa takriban miaka 50 ya uhuru wa Tanzania. Swali ninalojiuliza ni kwamba Dr Magufuli atafanyaje mabadiliko yatokee ktk mfumo uliyooza wa chama chake? Najaribu kuwaza kwa sauti, anakiri barabara hajizajengwa kwa viwango vinavyotakiwa, maji ni shida, hospitali hazina dawa, elimu yetu kwa sasa ni mbovu, anakiri pia kwamba serikali kwa sasa imejaa rushwa.
Lakini kichekesho Zaidi ni kwamba anatuambia atayashughulikia hayo, kwa mfumo huu huu ambao waliyoyasababisha haya, ndio waliompa nafasi ya kugombea na ndo hao hao wanaompigia kampeni, sasa nashindwa kuelewa hivi atayaletaje hayo mabadiliko? Vituko vya rushwa ndani ya ccm kila siku ktk kmpeni zao, tunazisikia, tena zikitolewa na wale wale naye na wanaompigia chapuu kwenye kampeni zake.
Sera hizi ndizo ambazo ccm wamekuwa wakizisema kila mwaka, na baada ya miaka mitano tunarudi tena na nyimbo zilezile.
MTAZAMO WANGU: Wapinzani pekee ndio wanaotakiwa kutuambia hizo sera, ccm wanapaswa watuambie kwanini wanazirudia hizi sera kila mwaka? watuambie walishindwa wapi na mwaka huu watafanyaje? Wataboreshaje elimu mwaka huu? wataondoaje mfumo wa rushwa ndani ya ccm, atawashughulikiaje viongozi wenzake tena ambao ndio wanaomweka madarakani?
MWISHO: Tufanye maamuzi sahihi, tujaribu mabadiliko, kwa miaka mitano, wasipoyaleta maendeleo tuwatoe, hakuna chama kilichoandikiwa kukaa madarakani milele.Tanzania hii ni yetu sote, uchumi wa nchi yetu hivi wanafaidi wachache, si sawa. Mabadiliko hayakwepeki mwaka huu.