Kama Lipumba anatumwa na CCM kuivuruga CUF, Chadema wanatumwa na nani kukivuruga CUF?

kalulukalunde

JF-Expert Member
May 27, 2016
1,056
1,083
Nimesikitishwa na wabunge wawili wa Cahadema, Tundu Lissu na Saidi Kubenea kwa nyakati tofauti walipotoa kauli zinazofanana, walikaririwa na baadhi ya vyombo vya habari wakisema nchini wakisema mgogoro wa kisiasa ndani ya Cuf, unachochewa zaidi na Prof Lipumba kutokana na kazi aliyotumwa na CCM kuvuruga Ukawa.

Kwa hoja hiyo zilizoibuliwa na wabunge hao wawili wapenda kuchukua fursa hii kuwapa pole wananchi wa majimbo yanayoongozwa na wanasiasa hao, Tundu Lissu na Saidi Kubenea. Pole yangu naitoa kwa hasara kubwa waliyonayo kwa kuongozwa na wabunge wenye fikra duni za kifikra.

Kwanza inakuwaje kwa wabunge wote wawili wa chadema kumshambulia Prof. Lipumba ambaye ni mwanachama au kiongozi wa Cuf na si Chadema, wanapata wapi ujasiri huo na watwambie kuna nini nyuma ya pazia kwa wao kuingilia mgogoro wa Cuf ambao hauwahusu?

Kwa mfano gazeti moja la kila siku limemkariri kubenea akisema kuwa Prof. Lipumba, kama anataka kuisadia CCM iendelee kukaa madarakani, basi aachanae na Cuf na kwenda kuanzisha chama chake.

Kwamba Lipumba katika mgogoro huo na Cuf anaonekana anaonekana kutekeleza kazi aliyotumwa na Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) kwa niaba ya CCM ili kuiua Cuf.

Kwa haikia maneno hayo ya kubenea hayawezi kutamkwa na kiongozi au mwananchama ambaye hana maslahi ya kisiasa na chama husika, hivyo yatatamkwa na mwanachama au kiongozi wa Cuf ambaye yupo kwenye mapambano ya kimaslahi na Prof Lipumba.

Lakini ajabu maneno hayo yanatamkwa na Mbunge wa Chadema tena mjumbe wa baraza kuu na mkutano mkuu na hausisiani kwa lolote na Cuf, lazima hapo kuna tatizo tena kubwa. Wewe kiongozi wa Chadema unataka Cuf iongozwe na nani na kwanini? Kwanini walitaka kuwachagulia Cuf viongozi?

Kwanini wewe mwananchama wa chama kingine unayetaka kuwachagulia Cuf viongozi tusikutilie shaka kama umna nia mbaya na unatumika kukivuruga chama ambacho wewe huna mahusiano nacho hata kidogo.

Siku zote mwanasiasa mweledi huwa anaweka akiba ya maneno tofauti na Kubemnea ambaye siku zote kuweka akiba ya maneno kwa kuwa hakuna ajuae kesho na hilo ni tatizo kubwa au shida kubwa kwa Kubenea.

Na sema akiba ya maneno ni shida kwa kubenea kwa kuwa ni huyu huyu alikuwa kituandikia katika magazeti yake juu ya ufisadi wa Lowassa na kwamba hata asafishwe na dodoki aina gani lakini hasafishiki kwa ufisadi aliokuwa nao, lakini leo bila haya wala aibu anamuandika kupitia magazeti hayo hayo kuwa Lowassa Muungwana.

Ukweli wabunge kama hawa kina Kubenea, hata ukienda katika majimbo yao, utasikia simulizi za nyingi zinazowahusu, zikiwemo wao kujiona bora kuliko wapiga kura wao, huku wakiwaona wapiga kura hawana akili.

Wanasiasa wa aina hii siku zote wanasumbuliwa na ulimbukeni wa kisisa, ndio maana huropoka ropoka ovyo kila wanapopata fursa ya kusimama mbere ya kamera za wanahabari bila kuweka akiba ya maneno.

Hebu kina Mbowe, Lissu na kubenea watwambie ukweli ikiwa Prof. Lipumba anatumwa na TISS kuivuruga ukawa, Chadema wanatumwa na nani kuivuruga Cuf hadi wataka kuwachagulia kukichagulia mwenyekiti na viongozi wengine wa chama hicho.

Chademna waache kuvihusisha vyombo vya ulinzi na usalama katika mambo ya kisiasa pale tu wanapokuwa wameshindwa hoja au kukosa cha kuongea, vyombo vya ulinzi vinafanya kazi kubwa kuhakikisha kuwa tunaishi na amani na utulivu na siyo kazi yao hata kidogo kujihusisha na mambo ya siasa.

Hivyo kuvichafua vyombo vya usalama na kujiondolea credibility ambayo itawafanya wananchi tuwadharau wao na vyama vyao kwa kuviona havina nia njema na Tanzania yetu ambayo tunaishi wao na sisi kwa amani.

Ni bora wakatumia muda mwingi kufanya shughuli za maendeleo katika majimbo yao kuliko kuvishutumu vyombo vya usilnzi na usalama kwa kuwa haitawasaidia katika kuongeza wala kupunguza kura katika chaguzi zijazo zaidi ya vyombo hivyo kuhakikisha chaguzi zinafanyika kwa amani na utulivu.
 
Wanazidi kupotea kwa kutotibu ugonjwa.....waulize pia kama wana"CCM" ndio walimwongoza Lipumba Je CUF wanaomwunga mkono Mtatiro na Seif mbona hawakutokea kupinga?....inamaana wanaCUF pia hawawataki Seif na Mtatiro?
 
Chadema ni wajanja sana sababu kinachotokea ndani ya cuf leo wao walijua haya yatatokea tena wao wamekua na furaha sana kwa kuona nyumba ya jirani inafuka moshi, kisiasa kwakuona chama kitabaki chao tu chenye nguvu. Kama waliweza kumshawishi Mh Edo kujiunga CDM ilishindikanaje kumshawishi Maalim Sefu kuumaliza mgogoro katika vikao vyao vya ndani badala yake CDM ndio wamekuwa wa kwanza kusimama kwenye majukwaa na kuutangaza mgogoro wa CUF kwa kumnyooshea kidole mtu mmoja, acheni janja hiyo. Nawasilisha
 
Hujielewi wewe,, wenye akili tunajua, Polisi nguvu waliyotumia Jana kuvunja office sio ya kawaida, tunajua michezo yenu imekula kwenu hii
 
Nimesikitishwa na wabunge wawili wa Cahadema, Tundu Lissu na Saidi Kubenea kwa nyakati tofauti walipotoa kauli zinazofanana, walikaririwa na baadhi ya vyombo vya habari wakisema nchini wakisema mgogoro wa kisiasa ndani ya Cuf, unachochewa zaidi na Prof Lipumba kutokana na kazi aliyotumwa na CCM kuvuruga Ukawa.

Kwa hoja hiyo zilizoibuliwa na wabunge hao wawili wapenda kuchukua fursa hii kuwapa pole wananchi wa majimbo yanayoongozwa na wanasiasa hao, Tundu Lissu na Saidi Kubenea. Pole yangu naitoa kwa hasara kubwa waliyonayo kwa kuongozwa na wabunge wenye fikra duni za kifikra.

Kwanza inakuwaje kwa wabunge wote wawili wa chadema kumshambulia Prof. Lipumba ambaye ni mwanachama au kiongozi wa Cuf na si Chadema, wanapata wapi ujasiri huo na watwambie kuna nini nyuma ya pazia kwa wao kuingilia mgogoro wa Cuf ambao hauwahusu?

Kwa mfano gazeti moja la kila siku limemkariri kubenea akisema kuwa Prof. Lipumba, kama anataka kuisadia CCM iendelee kukaa madarakani, basi aachanae na Cuf na kwenda kuanzisha chama chake.

Kwamba Lipumba katika mgogoro huo na Cuf anaonekana anaonekana kutekeleza kazi aliyotumwa na Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) kwa niaba ya CCM ili kuiua Cuf.

Kwa haikia maneno hayo ya kubenea hayawezi kutamkwa na kiongozi au mwananchama ambaye hana maslahi ya kisiasa na chama husika, hivyo yatatamkwa na mwanachama au kiongozi wa Cuf ambaye yupo kwenye mapambano ya kimaslahi na Prof Lipumba.

Lakini ajabu maneno hayo yanatamkwa na Mbunge wa Chadema tena mjumbe wa baraza kuu na mkutano mkuu na hausisiani kwa lolote na Cuf, lazima hapo kuna tatizo tena kubwa. Wewe kiongozi wa Chadema unataka Cuf iongozwe na nani na kwanini? Kwanini walitaka kuwachagulia Cuf viongozi?

Kwanini wewe mwananchama wa chama kingine unayetaka kuwachagulia Cuf viongozi tusikutilie shaka kama umna nia mbaya na unatumika kukivuruga chama ambacho wewe huna mahusiano nacho hata kidogo.

Siku zote mwanasiasa mweledi huwa anaweka akiba ya maneno tofauti na Kubemnea ambaye siku zote kuweka akiba ya maneno kwa kuwa hakuna ajuae kesho na hilo ni tatizo kubwa au shida kubwa kwa Kubenea.

Na sema akiba ya maneno ni shida kwa kubenea kwa kuwa ni huyu huyu alikuwa kituandikia katika magazeti yake juu ya ufisadi wa Lowassa na kwamba hata asafishwe na dodoki aina gani lakini hasafishiki kwa ufisadi aliokuwa nao, lakini leo bila haya wala aibu anamuandika kupitia magazeti hayo hayo kuwa Lowassa Muungwana.

Ukweli wabunge kama hawa kina Kubenea, hata ukienda katika majimbo yao, utasikia simulizi za nyingi zinazowahusu, zikiwemo wao kujiona bora kuliko wapiga kura wao, huku wakiwaona wapiga kura hawana akili.

Wanasiasa wa aina hii siku zote wanasumbuliwa na ulimbukeni wa kisisa, ndio maana huropoka ropoka ovyo kila wanapopata fursa ya kusimama mbere ya kamera za wanahabari bila kuweka akiba ya maneno.

Hebu kina Mbowe, Lissu na kubenea watwambie ukweli ikiwa Prof. Lipumba anatumwa na TISS kuivuruga ukawa, Chadema wanatumwa na nani kuivuruga Cuf hadi wataka kuwachagulia kukichagulia mwenyekiti na viongozi wengine wa chama hicho.

Chademna waache kuvihusisha vyombo vya ulinzi na usalama katika mambo ya kisiasa pale tu wanapokuwa wameshindwa hoja au kukosa cha kuongea, vyombo vya ulinzi vinafanya kazi kubwa kuhakikisha kuwa tunaishi na amani na utulivu na siyo kazi yao hata kidogo kujihusisha na mambo ya siasa.

Hivyo kuvichafua vyombo vya usalama na kujiondolea credibility ambayo itawafanya wananchi tuwadharau wao na vyama vyao kwa kuviona havina nia njema na Tanzania yetu ambayo tunaishi wao na sisi kwa amani.

Ni bora wakatumia muda mwingi kufanya shughuli za maendeleo katika majimbo yao kuliko kuvishutumu vyombo vya usilnzi na usalama kwa kuwa haitawasaidia katika kuongeza wala kupunguza kura katika chaguzi zijazo zaidi ya vyombo hivyo kuhakikisha chaguzi zinafanyika kwa amani na utulivu.
ww sindoo ulikuwa unalalamika kuhusu uhakiki wa watumishi hewa kumbe nawe ccm goja ukome
 
Lazima tuamini hivyo kuwa Lipumba anatumiwa na CCM, angalia hata wafuasi wake leo hii humu ndani kama wakina Ruta wanaosema lazima tuwe na Upinzani Imara, hivi ni kweli hawa leo wamegeuka kuwa mtetezi wa CUF.

WANACCM HUWA WANASHABIKIA UGOMVI WA VYAMA VYA UPINZANI KAMA UGOMVI HUO UNAWANUFAISHA.

CHADEMA HAWAJATUMWA NA MTU BALI WANATETEA YULE ANAYEFANANA NAO KIMALENGO.
 
Mabadilisha gia za angani Chadema yanaua upinzani nchini kwa tamaa ya pesa.

Kwa nini Mbowe auza chama kwa Mafisadi kutoka ccm?
 
Back
Top Bottom