Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,185
- 7,491
Siku hizi kila nikitaka kuanzisha uzi kwenye jukwaa hili, nikishamaliza kuandika, kuna kitu kinaniambia futa huo uzi na usiuposti, na kweli haraka haraka naufuta. Huu nao nauandika huku nikiomba Mungu nisije nikaufuta kabla ya kuupost.
Ndugu zangu; Wengi wetu naamini tunaamini kuwa Mungu ndio Mkuu na anaweza kufanya lolote akiamua. Tunaamini kuwa Mungu akitaka jambo lolote hulia ambia tu "Kuwa" nalo linakuwa.
Ndugu zangu, pamoja na jitihada zetu zote za kibinaadamu kama kutumia akili, kujituma , kujielimisha, kutafiti n.k , kuna mahali ambapo tunafika jitihada zetu zinakuwa haziwezi kutufikisha mbali. Bila kujali sana imani zetu, kwa wale tunaoamini kuwa Mungu yupo na Anaweza yote, muda umefika sasa.
Mungu anatuambia kupitia vitabu vitukufu kuwa tukifikwa na mikasa tusiyoiweza kuikabili; tuishughulikie kwa "sala/swala (maombi) na subra!
Ndugu zangu, Bila kufafanua sana (kwa kuwa kila mmoja wetu anaelewa), kila mtu anajua ni kwa nini nasema wakati sasa umefika. Waislamu anzeni kufunga na kusimama visimamo vya usiku kumuomba Mwenyezi Mungu atunusuru na madhila, dhahama na mabalaa. Wakristo ombeni kadiri muwezavyo na kila mtu kwa imani yake na amuombe Mungu kwa dhati kabisa atusaidie!.
Mungu akiamua tunaweza kupata unafuu kutokana na shida tulizonazo.(naomba nisifafanue) kila mtu anajua ana shida ipi na ipi na ni maeneo gani yenye shida mabayo sasa yanaonekana kuwa nje ya uwezo wa binadamu mmoja mmoja.
Tuiombeeni nchi yetu pia kwa ujumla.
Haya ni maoni tu kwa atakayeona kuwa inafaa kufanya hivyo, basi naafanye kwa kadiri ya uwezo wake.