Kama kweli lengo la upinzani ni kushika dola; kwanini iwe ajabu kutumika katika serikali?

Stroke

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
34,671
40,912
Binafsi nimeshangazwa sana na maneno yasiyo na hekima wala busara juu ya wapinzani kutumika serikalini.

Mshangao huo umefikia hatua ninapata mashaka ya nia na agenda ya siri waliyonayo wapinzani kuhusiana na melengo yao ya kutaka kuongoza Taifa hili.

Miaka yote wamekuwa wakijitanabaisha kwamba wanataka kushika dola na kutuletea maendeleo. kuna waliowapokea na kuna ambao hawakuwapokea. Kwa wale waliowapokea wanasababu zao, na kwa wale ambao hawajawapokea wanazosababu zao vile vile.

Sasa inapokuja nafasi ya kuonesha weledi wao, katika kutoa huduma kwa wananchi yanazuka maneno ya usaliti napata mashaka sana.

Najiuliza kama kuwatumikia wananchi ni usaliti na kama ni usaliti ni kwa nani, nani huyu ambaye anaonekana kusalitiwa ni wa muhimu sana kuliko nia njema ya kuwahudumia wananchi kwanza.

Je hi haki ya nani huyu ambayo inatakiwa kulindwa sana kuliko haki ya wananchi kupewa maendeleo.

Ni ajabu sana, kama jambo la Uchama litakuwa ndio priority ya kwanza kuliko ile ya haki ya wananchi kupata maendeleo.

Kama nia ya vyama vyote ni kuleta maendeleo, kwanini iwe ajabu sana kwa upinzani kutumika serikali?

Ni nini kipo nyuma ya hii nguvu kubwa ya Uchama kuliko Utaifa?

Je nguvu hiyo kubwa ya Uchama inayotaka kufunika Utaifa imegubikwa na Umimi na ubinafsi kuliko Usisi??

Mtu yote mzalendo kwa Taifa lake, atapata mashaka ya nini kipo nyuma ya maneno kwamba mpinzani hawezi kutumika serikalini na akitumika anaonekana msaliti?
 
Ondokeni ikulu Chama chakavu Chadema watupeleke mbele. Tumechoshwa uongozi wa hovyo w masisiemu
 
Back
Top Bottom