Kama kuondoka Lowasa na Sumaye hakukuwapa funzo wanaCCM, hili la Nape na funzo jingine!

NAKEMBETWA

JF-Expert Member
Apr 20, 2012
3,517
3,133
Wakuu salam

Kuna msanii aliwahi kuimba kuwa, kama Yanga ikifa Simba itacheza na nani, au Simba ikifa Yanga watacheza na nani?


Kuna usemi pia kuwa, Ukiwa mkuu wa gereza jitahidi kuboresha gereza maana huwezi jua kuna siku wewe, au mkeo au mwanao au mjukuu au rafiki au nduguyo wa karibu ataenda gerezani!

Wakuu kwa muda mrefu siasa zetu zimekuwa za kukomoana na visasi kibao, hadi inafikia mtu akiwa CCM au Chadema anajisahau kabisa kana kwamba vyama vingine ni maadui na hutamani hata kuvifuta au vife kabisa!

Kama wana CCM wangekuwa wanasimamia ukweli toka mifumo ya vyama vingi ilipoanza, kuanzia Chaguzi huru, wangesimamia katiba ya wananchi isiyo na upendeleo leo hii hii sidhani kama wangefungwa midono na mikono na mtu mmoja na kuwaamuru wafanye anavyotaka!

Kwa muda mrefu viongozi wanapokuwa CCM wamekuwa wakigandamiza na kuviwekea mizengwe vyama vya upinzani kwa kuwa tu wao si sehemu ya vile vyama, ila wanapokuja kutoswa wanakuja kujilaumu kwa nini waliweka mazingira mabaya ambayo yanawatafuna tena wao wenyewe!

Nafikiri leo Chaguzi zetu zisingekuwa na magoli ya mikono, labda tungekuwa na wabunge 50/50 Chama tawala na Upinzani na sidhani kama Rais angepata ubavu wa kuminya na kuwapiga mikwala wabunge!

Nani alidhani leo Lowasa au Sumaye au Kingunge wangeonekana hawana maana tena kule CCM?

Nawaasa wana CCM jitahidini kusimamia ukweli ili baadae msije mkajutia na kukosa hata pa kukimbilia mambo yakiwawia vigumu huko chamani!

Mungu aendelee kutufumbua macho!
 
Back
Top Bottom