Kama ingelijua hili, CCM ingeacha tambo kabisa!!!!

Kama ingelijua hili, CCM ingeacha tambo kabisa!!!!

Bado Kidogo 2015

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2012
Posts
207
Reaction score
78
Wanabodi,

Katika mkutano ulimalizika majuzi hapa mjini Dodoma - Kizota serikali ya CCM imewataka wanaCCM kutembea kifua mbele na kuepuka tambo za wapinzani kuwa hawajafanya kitu!!!!! Kauli hiyo na nyingine nyingi za matambo zilizotoka zilikuwa na lengo la kuwaaonyesha wananchi na wanaCCM kwa ujumla kuwa chama chao kimefanya na kinafanya kazi kubwa mpaka hapo kilipofikia!!!!!

Ok, tukiachana na hilo ipi ni hali halisi??? Kiukweli namkubuka babu yangu aliyesema "ukiona mtu anajitamba sana jua hana kitu" Nami kauli hiyo naona ina ukweli kwa 75%.

1. Huwezi ukawa unashindwa kutekeleza majukumu yako ya ndani kisha ukajisifu kwa kujenga nyumba. Nyumbani watoto wanalala na njaa lakini wewe nje unasema nina nyumba nne. Kitendo cha serikali ya CCM kushindwa hata kutekeleza mahitaji ya serikali yake yenyewe ni hatari sana. Mpaka sasa karibu nusu ya mwaka wa fedha unataka kukatika lakini serikali imeshindwa kuleta hata nusu ya bajeti ya kila wizara iliyopitishwa na bunge ni aibu kubwa. Kama kuna mtu anabisha achukue bajeti ya mwaka wa fedha 2011/2012 alinganishe na 2012/2013 kwa mtiririko wa mafungu au utekelezaji.

Wizara nyingi za serikali zinalia njaa, wanashindwa kutengeneza magari, mafuta hawana, vitendea kazi ofisini hakuna, na mbaya zaidi saizi kumezuka mtindo wa kuchelewesha hata haki zao yaani mishahara!!! Ni mjinga gani atayefurahia kutengenezwa kwa barabara huku akijua fedha nyingi ya mabarabara hayo ni mikopo???

2. Nikiachana na watumishi wa serikali wao wanajuana na mwajiri wao, vipi hali halisi ilivyo mtaani. Karibu watu wengi saa hizi wanalia hali kuwa ngumu kuliko ilivyokuwa miaka ya nyuma. Kwa kuwa wananchi wengi wa Tanzania hatuhoji hali hii imekuaje??? Ukweli ni kwamba SERIKALI IMEPUNGUZA MATUMIZI YAKE na kusababisha mzunguko wa fedha kuwa mdogo.

Wapo wanaweza kubisha, lakini wafanya biashara wengi wanaofanya biashaara na serikali wapo njiani kugoma kutokana na kutolipwa. Hali hii ingekuwa ina uafadhali kama basi serikali ingejitahiti hata kukidhi mahitaji ya kiuendeshaji ya serikali yenyewe!!!!

Kwa mantiki hiyo basi, kama mkulima analia, mfanyakazi analia na hata hao wafanyabiashara wengi wanakiri hali ya kipato chao siyo nzuri kutokana na wengi kutokuwa na fedha LIPI WANALOJIVUNIA SERIKALI YA CCM mapaka kuwafanya watembee kifua mbele????

Naamini chama chochote kama kingekuwa madarakani kisingeshindwa kufanya haya wanayofanya wanaCCM na kujitamba. Kama vyanzo ni kwenda kukopa hata ukiniweka mimi nitashindwa kukopa nije niwafanyie haya wanayofanya serikali ya CCM????

Kiukweli kama serikali ya CCM inataka wanachama na serikali yake ifanye zaidi ya haya inayoyasema ili tuone tofauti badala ya kujisifia kwa kitu ambacho kila mtu anaweza kukifanya as long as yupo madarakani!

Kwa kuhitimisha, serikali ya sasa iache matambo badala ya kufanya kazi. Hali ni mbaya sana mtaani, wakulima wanalia, wafanyakazi wanalia, ni wafanyabiashara tu angalau kidogo vinginevyo serikali nayo inalia lakini inataka kuwaaminisha wananchi inacheka!!!!

Huo ni kwa kadri ya uelewa wangu wa form 4 ya kata niliyomaliza majuzijuzi. Kama ningefika hata form six, I could dig more for the benefit of others.

Copy, Mzee Mwanakijiji, Mchambuzi PakaJimmy Mungi, Crashwise Ritz zomba Rejao @Naape Jr Preta BADILI TABIA, Mwana Mtoka Pabaya mikaeli p aweda, Tumaini Makene, Money stunna, Bujibuji, maggid; Molemo,
Ruttashobolwa Yericko Nyerere, na wengineo wengi ambao sijwataja.

MoDs naomba usiunganishe na nyuzi ngingine.

Nawasilisha.
 
CCM ni laini kama maini kutoka kwa Mwenyekiti wao mpaka chini kabisa.
Siku zote wao ni bora sana kwa maneno, lakini kwenye vitendo ndo utakapowajua kumbe ni maduwanzi kabisa.
CHADEMA kwa sasa ndiyo tumaini la wanyonge, ccm wanadhani bado wanawaongoza akina kingunge wa miaka ya 70.
 
Kwa binafsi nadhani maneno hayahubiri sana kuliko matendo. Kama Yesu angekuwa anahubiri pekee bila matendo mema basi sidhani kama ukristo ungefika hapa au kama Muhammad naye angekuwa anafanya kinyume na yale anayohubiri ni wazi waislam wasingekuwepo leo hii.

Hali kadhalika CCM inachotufanya ni tofauti sana na inachokihubiri. Kwa nantiki hiyo niungane na wale wazungu waliosema "Action speaks louder than words"

Acha waendelee na mikakati tu huku hali inazidi kuwa mbaya.
 
niaminivyo mm hakuna uongozi ambao utakosa kukosolewa manake hata mwanadamu aliyeumbwa na Mungu ambaye ni mkamilifu sana, hajakamilika sembuse yale tunayoyaumba sisi binadamu??

yapo mambo ambayo serikali imeshindwa kuyatekeleza yakaleta tija kwa taifa lakin pia yapo ambayo yametekelezwa yakaleta tija.

sion ubaya kwa mwenyekiti wao kwataka wanachama wake waite kifua mbele wakihubiri ema wa ccm kwani ndicho tunachotegemea kwa chama chochote kile cha siasa. hapa tatizo nilionalo ni kwa sisi wananchi kwamba tunapriotize wapi je kwa mwenye uwajibikaji mzuri ama kwa mwenye sera nzuri??
 
gfsonwin Kama huoni tatizo watu kulia hali ngumu ya maisha karibu kila kona basi unashida dada yangu. Tambo zikiendana na matendo ndiyo utamu unapopatikana lakini si vinginevyo.
 
Last edited by a moderator:
Kama huoni tatizo watu kulia hali ngumu ya maisha karibu kila kona basi unashida dada yangu. Tambo zikiendana na matendo ndiyo utamu unapopatikana lakini si vinginevyo.

hahahhah! hivi tatizo ni watu kulia shida ama tatizo ni watu kutambua kwanini wako kwenye dhiki???
binafsi sion tatizo kamwe kwa kikwete kumuambia mwanachama wake akatangaze habari njema za chama chake, mbona hilo sio jipya kabisa???

sasa nkwambie mm naona tatizo wapi?? tatizo nilionalo mm ni pale ambapo serikali inagharamia shghuli za chama fulan, mfano mzuri sioni sababu ya magari ya ikulu kutumikakwenye kazi za chama hata kama raisi anakwenda. kwann ccm isinunue ari la raisi ambalo atalitumia anapokuwa anafanya kazi za chama?? tena ligharamiwe na ccm mafuta dereva na parking?

kiimsingi hili ni tatizo tena kubwa sana na tunapaswa kutofautisha majukumu ya kichama na yale ya kiserikali katika taifa letu kwa stail hii unakuta chama fulan kinahudumiwa na serikali indirect, wakati chama kingine wakibaki kapuku.
 
Unajua gfsonwin hoja yangu ipo katika kuzembea kwa serikali katika kuetekeleza majukumu ambako kuna sababisha matatizo kuanzia kwa seikali yenyewe mpaka kwa wananchi.

Mfano ulio wazi ni kushindwa kutekeleza bajeti yake iliyopishwa katika mwaka wa fedha 2012/2013. Licha ya hayo bado kuna uzembe mkubwa sana katika kutekeleza haya yale ya msingi kama uchelewevu wa mishahara ambao nao umeibuka siku hizi.

Hayo ya serikali na wajiri wao nawaachia wenyewe, njoo mtaani unafikiri hata wafanya biashara wanaolalamika kutolipwa kutokana na serikali kukosa fedha za kuwalipa wataendeshaje maisha????

Naomba upitie post yangu kwa uzuri zaidi utabaini ninakisema.

UTAKUWAJE UMEFELI MTIHANI HALAFU UNAWAAMBIA WATU WATAMBE??? WATAMBE KWA KUFELI AU KWA LIPI???
 
Bado Kidogo 2015 Binafsi sikupingi juu ya hili, ila nafikiri nakujibu kwa staili ya nyuma kwenda mbele.
kwamba kama ccm wanatangaza tambo sawa watangaze ila sisi wananchi tunachokiangalia ni tambo ama uwajibikaji???
 
Last edited by a moderator:
binafsi sikupingi juu ya hili, ila nafikiri nakujibu kwa staili ya nyuma kwenda mbele.
kwamba kama ccm wanatangaza tambo sawa watangaze ila sisi wananchi tunachokiangalia ni tambo ama uwajibikaji???

Sasa kuwaambia mawaziri watembee nchi nzima kuelezea mafanikio ya serikali yao huoni ni ufajaji wa vihela vichache vya wizara kuuishia makao makuu, how about others????

Maendeleo kama serikali inawajibika wala hayafanywi kutangazwa bali yanaonekana. Uwajibikaji ndiyo unaopima kelele za wanasiasa baada ya kuaminiwa. Tuwapawa CCM miaka mitano siyo watambe bali wafanye kazi,

Mbona Mkapa hajawahi kuwaambia wamaziri wake wapite mitaani watangae mazuri ya serikali ambayo ni wazi yalikuwa yalionekana na ndiyo maana JK akashinda kwa 80% 2005!!!
 
Umenikumbusha mbali sana yaani juu umeoga weee, tena umeogea mtoni ukapaka Vasta au Shanti au Vasteline kumbe ndani umevaaa VIP (aina ya chupi) ina siku ya tano haijui maji, upande wa soksi ndio usiseme, so ina maana CCM hawajafua soksi wala makufuli? Huku nje aaah wamenyoa Panki na kuchana wei, nimekupata Mpwa, ngoja watakapoanza hizo safari zao viatu na makfuli yatakavyoanza kunuka ndio watamkumbuka aliyewatuma
 
Sasa kuwaambia mawaziri watembee nchi nzima kuelezea mafanikio ya serikali yao huoni ni ufajaji wa vihela vichache vya wizara kuuishia makao makuu, how about others????

Maendeleo kama serikali inawajibika wala hayafanywi kutangazwa bali yanaonekana. Uwajibikaji ndiyo unaopima kelele za wanasiasa baada ya kuaminiwa. Tuwapawa CCM miaka mitano siyo watambe bali wafanye kazi,

Mbona Mkapa hajawahi kuwaambia wamaziri wake wapite mitaani watangae mazuri ya serikali ambayo ni wazi yalikuwa yalionekana na ndiyo maana JK akashinda kwa 80% 2005!!!
ndio maana nikasema ifike wakati tutenganishe kaz za chama na kazi za serikali. ama hukunielewa mkuu?
 
Mwenyekiti wao amewatuma eti M4C ikipita na wao wapite wawaeleze wananchi kuwa wamejenga shule,barabara na mengine mengi.......Hii ni Kauli ya Mwenyekiti.
 
niaminivyo mm hakuna uongozi ambao utakosa kukosolewa manake hata mwanadamu aliyeumbwa na Mungu ambaye ni mkamilifu sana, hajakamilika sembuse yale tunayoyaumba sisi binadamu??

yapo mambo ambayo serikali imeshindwa kuyatekeleza yakaleta tija kwa taifa lakin pia yapo ambayo yametekelezwa yakaleta tija.

sion ubaya kwa mwenyekiti wao kwataka wanachama wake waite kifua mbele wakihubiri ema wa ccm kwani ndicho tunachotegemea kwa chama chochote kile cha siasa. hapa tatizo nilionalo ni kwa sisi wananchi kwamba tunapriotize wapi je kwa mwenye uwajibikaji mzuri ama kwa mwenye sera nzuri??
Akili za am CCM ni nyepesi utadhani hawana wasomi wala hawana exposure.Uthadhani wanatuona sisi watanzania kwamba hatutembelei waendako na kukutana na wanao kutana nao.Ni ujinga mtu kuja na kutueleza kwanza kipimo cha maendeleo ya Watanzania ni uwingi wa maghorofa mjini na foleni ndefu za magari bila ulinzi madhubuti,usalama tete vibaka na ujambazi,dhuluma Polisi,mahakamani,na toka kwa watawala na basic needs zote ni ndoto kwa mtanzania wa kawaida
 
peopleos poweeer!wasubiri nguvu ya umma ndo itakayoamua,cidanganyikii saiv kama kuna m2 wa kawaida ambaye cio fisadi hateseki na ajitokeze hapa jamvini wadau
 
Akili za am CCM ni nyepesi utadhani hawana wasomi wala hawana exposure.Uthadhani wanatuona sisi watanzania kwamba hatutembelei waendako na kukutana na wanao kutana nao.Ni ujinga mtu kuja na kutueleza kwanza kipimo cha maendeleo ya Watanzania ni uwingi wa maghorofa mjini na foleni ndefu za magari bila ulinzi madhubuti,usalama tete vibaka na ujambazi,dhuluma Polisi,mahakamani,na toka kwa watawala na basic needs zote ni ndoto kwa mtanzania wa kawaida

Na hata majuzi mwenyekiti wao aliwataka kuacha akili za kanga, kuficha kichwa kuacha mwili mzima nje.
 
Tunahaki ya kutembea kifua mbele, maake tumefanya mengi unaposema wanajenga kwa kukopa ni nchi gani ambayo haikopi kwa ajili ya maendeleo ya watu wake, hatudanganyiki tuna macho tunaona wewe endelea kulia na chadema yako wenzako wanacheka na ccm yao, pole sana mkubwa na mawazo mgando yako!!!
 
Back
Top Bottom