Nadhani mnakumbuka mkwara wa kubomoa nyumba zote zilizojengwa kinyume cha utaratibu. Majiji yakaja na takwimu ya kuvunja maelfu ya majengo. Tukaambiwa hotel kubwa kubwa zilizojengwa ufukweni zitashushwa kama ubua. Mpaka sasa hatujui zoezi lilikwishaje! Mabangaroo bado yanapendeza ufukweni
Tunakumbuka pia safari za kushutukiza. Bandarini, TRA, Benki kuu, Muhimbili na mawaziri wakishutukiza kila mahali. Wengine walienda na waandishi alfajiri kuwafungia watu milango ya ofisi, kutoa siku 7 au 14, mwezi nk. Leo sikumbuki ziara ya mwisho ya kushutukiza ilifanyika lini na wapi!
Linaloelekea kufa jingine ni tumbua majipu. Nilishasema kwamba serikali hii ilikuwa haitumbui bali ilikuwa inateua watu wapya kwenye nafasi mbali mbali. Ilikuwa lazima umuondoe mtu fulani nafasi fulani ili umteu mtu mwingine. Lakini zoezi hilo ikabidi liingize sifa kidogo! Inabidi yule unayemuondoa utangaze umemtumbua. Kama unabisha hilo nikumbushe nafasi za uteuzi zilipopungua au kuisha ni lini umesikia mtu anatumbuliwa?