Mabibi na mabwana kwa kuziangalia nchi za East Africa (EA) sisi kama Tanzania tuna kufanana zaidi na Uganda tukijilinganisha na wengine. Labda hata tungefikiria Muungano mwingine nchi ya tatu sasa ikiwa wao.
Uganda chama tawala kimekita mizizi yake barabara na kwa mujibu wa vyama vingine vilivyopo, chama tawala hakina mpango wowote wa kuviachia vyama vingine hata kupata nafasi tu ya kupumua.
Uganda mambo ya tume ya uchaguzi ni kama kwetu. Iko kama yale mambo ya "copy and paste." Vyama vingine vimekuwa vinapigia kelele suala la tume huru bila ya mafanikio. Hii ni kama ilivyo kwetu tu ambapo chama tawala kinaamini tume iliyopo ni huru na inatosha sana.
Vyombo vya dola vinalalamikiwa kukibeba NRM na kuhakikisha vyama pinzani vinatatizika vilivyo hata katika kufanya kampeni tu ambazo zipo kwa mujibu wa katiba.
Wagombea tokea upinzani katika kampeni zao wana hatari ya kusimamishwa na hata kufutwa kabisa hasa wanapokuwa wanatumia lugha za kuudhi kwa chama tawala. Kutoyaona maendeleo yaliyofanywa na chama tawala ni moja ya lugha hizo zenye kuudhi sana.
Kutoyatambua maendeleo yanayoitwa makubwa yaliyofanywa na vyama tawala huitwa kutumiwa na mabeberu.
Upinzani umefanywa kuwa uadui. Kutofautiana kisiasa na Museveni ni heri ya kosa la jinai. Huko ya wasiojulikana ni kama ya kwetu tu. Ya kupotea na hata kuuwawa watu, upinzani yanawahusu sana.
Upande wa chama tawala na upinzani kumegawanyika mno kiasi hayapo maridhiano yoyote yanayoweza kufikiwa. Mshupaza shingo mkuu akiwa chama tawala.
Wakuu tuna mengi ya kufanana na waganda. Ilikuwa si haba kuyaangazia tukiwa na nia thabiti ya kudumisha zile ndoto za waasisi wetu akiwamo wa taifa letu mwalimu Nyerere (rip) za kuliunganisha Bara hili kuwa nchi moja.
Ikumbukwe baba wa taifa alionyesha njia kwa kuunganisha mataifa mawili yaliyokuwa yamefanana zaidi wakati ule na leo tuko hapa tulipo.
Safari alishaianzisha na iendelee na zingine. Hapo kaskazini si bure pana mwenzetu. Pana matumaini. Yaani pana prospects.
Bila kusahau viongozi wetu wakuu majembe wa mataifa mawili rafiki haya wana kauli mbiu moja ya kuwa:
"Maendeleo, hayana chama!"
Ninawasilisha.