mabuba
Senior Member
- Dec 5, 2006
- 133
- 90
Kudhibiti wakwepa kodi ni lazima,
Walifanya yao nchi pasi huruma,
Walikula na kukomba kwa kukomoaa
Ni udikteta uchwara, basi mimi nautaka.
Wafanyakazi hewa hatukuwataka,
Sasa arobaini imefika, wajifanya hasira,
Waondolewe kwa mbwembwe
Ni udikteta uchwara, basi mimi nautaka.
Madawati yanaundwa kwa hara,
Watoto wapate jisitiri,
Hili nalo nongwa, aibu,
Ni udikteta uchwara, basi mimi nautaka.
Wabunge wasionidhamu.
Chamoto wanakiona,
Wamefurushwa bungeni,
Ni udikteta uchwara, basi mimi nautaka.
Wengine wanadanya, kule mjengoni,
Tulia amewatuliza, wauita uchwara,
Koma yenu imefika, ukweli uwe wazi
Ni udikteta uchwara, basi mimi nautaka.
Miungu kwenye utumishi, zao zinahesabika,
Wabanangaji kwenye kazi, muda umetimu,
Weledi na mahiri, nyuso zenye tabasamu,
Ni udikteta uchwara, basi mimi nautaka.
Mafisadi wanahaha, kificho kukiingia,
Wanaona kihama, chao kimefika,
Wanatumia kila mbinu, kuficha zao kucha,
Ni udikteta uchwara, basi mimi nautaka.
Walimuona dhaifu, Jakaya Muungwana,
Sasa kaja wakuwasimamia, waanza lalama,
Aliwaacha wajifunze, matusi yawatoka,
Ni udikteta uchwara, basi mimi nautaka.
Walifanya yao nchi pasi huruma,
Walikula na kukomba kwa kukomoaa
Ni udikteta uchwara, basi mimi nautaka.
Wafanyakazi hewa hatukuwataka,
Sasa arobaini imefika, wajifanya hasira,
Waondolewe kwa mbwembwe
Ni udikteta uchwara, basi mimi nautaka.
Madawati yanaundwa kwa hara,
Watoto wapate jisitiri,
Hili nalo nongwa, aibu,
Ni udikteta uchwara, basi mimi nautaka.
Wabunge wasionidhamu.
Chamoto wanakiona,
Wamefurushwa bungeni,
Ni udikteta uchwara, basi mimi nautaka.
Wengine wanadanya, kule mjengoni,
Tulia amewatuliza, wauita uchwara,
Koma yenu imefika, ukweli uwe wazi
Ni udikteta uchwara, basi mimi nautaka.
Miungu kwenye utumishi, zao zinahesabika,
Wabanangaji kwenye kazi, muda umetimu,
Weledi na mahiri, nyuso zenye tabasamu,
Ni udikteta uchwara, basi mimi nautaka.
Mafisadi wanahaha, kificho kukiingia,
Wanaona kihama, chao kimefika,
Wanatumia kila mbinu, kuficha zao kucha,
Ni udikteta uchwara, basi mimi nautaka.
Walimuona dhaifu, Jakaya Muungwana,
Sasa kaja wakuwasimamia, waanza lalama,
Aliwaacha wajifunze, matusi yawatoka,
Ni udikteta uchwara, basi mimi nautaka.