Mr George Francis
JF-Expert Member
- Jun 27, 2022
- 274
- 486
KAMA FAMILIA YENU MNAISHI KWA UPENDO, MSHUKURUNI SANA MUNGU.
Miaka ya nyuma pindi tunakuwa kwa kiasi kikubwa familia nyingi zilikuwa na upendo, maelewano, na kutembeleana mara kwa mara.
Lakini leo hii mambo yamebadilika ndugu wengi wamekuwa na hali ya kutoelewana, kuchukiana au hata kutoonana kabisa.
Sababu zinaweza kuwa nyingi lakini miongoni mwa hizo ni hizi zifuatazo.
1. Wivu na ushindani wa maisha.
Mmoja akifanikiwa kimaisha, kielimu, au biashara, wengine wanaweza kuhisi wivu au chuki dhidi yake.
Lakini pia huyu aliyefanikiwa anaweza kuwa na dharau, kiburi na jeuri ya fedha kiasi cha kuwaona wenzake kama wajinga, hawajitambui, hawajitumi na hawana akili za kutafuta.
Mwisho wa siku kukosekana kwa upendo, unafiki na chuki baina yao lazima kujitokeza.
2. Urithi na mali za familia.
Hii pia ni sababu kubwa sana ya ndugu wa familia moja kuingia kwenye migogoro ya wenyewe kwa wenyewe.
Baada ya wazazi kuaga dunia, ugomvi wa kurithi ardhi, nyumba, biashara, fedha unaharibu uhusiano kati ya wanandugu.
Mara nyingi huishia Magakamani au hata chuki ya maisha yote.
3. Maisha ya kisasa na urbanization.
Watu wengi wanaishi maisha ya kimjini mjini kama Dar es Salaam. Mila mtu ana maisha yake binafsi, kazi, na majukumu yake.
Hakuna tena muda wa kukutana, kutembeleana, au kushiriki shida na furaha kwa pamoja.
Familia nyingi zimekuwa "kila mtu na maisha yake." Kujitenga kumeongezeka.
Hata watoto likizo hawaendi tena kwa shangazi au kwa mjomba kama zamani. Hivyo, ndugu tunaishi hatuna ukaribu wala mazoea.
4. Malezi na mazingira ya utotoni.
Baadhi ya ndugu walilelewa kwa ubaguzi mmoja anapendwa zaidi, mwingine anapuuzwa kama vile sio ndugu.
Hivyo watoto wanakuwa wanaendelea na chuki hiyohiyo mpaka watu wazima.
5. Ukosefu wa malezi ya maadili na ushauri wa wazazi. Huku pia kunachangia kuvunjika kwa umoja baina ya ndugu.
Mzazi anashindwa mukanya mtoto wake pale anapoona mtoto huyo anaonesha chuki kwa ndugu zake.
Hivyo, mtoto anakuwa anaona kama ni sawa tu na ni haki yake kufanya vile.
6. Ubinafsi uliokithiri.
Kwa tuliocheza mpira wa makaratasi kijijini kwetu Tangeni, tulikuwa tunaita hali hii kama "nifunge nene."
Yaani unakuta mchezaji mpo timu moja lakini marazote anataka kufunga yeye tu ili aonekane anajua zaidi kuliko wengine.
Mtu hatakama upo kwenye nafasi ya kufunga alafu yeye ana mpira yupo tayari apige nje ila sio kukupa wewe mpira ufunge.
Mfano huu upo kwenye familia nyingi siku hizi. Mtu anaweza kuwa na fursa ambayo hawezi kuitumia lakini hataki kukupa wewe ufanikiwe.
Uliguruni tunasema "katsopata." Hii ni mbaya sana.
NB: Ndugu tupendane na tuishi kwa kushirikiana. Tusaidiane ili kila mmoja avuke na atimize ndoto zake na awe na uwezo wa kusaidia wengine walio nyuma yetu.
Lakini bado kuna familia chache zinazoshikamana na kupendana. Kama familia yenu mnaishi vizuri kwa upendo na kuthaminiana mshukuru Mungu na muombeane sana, msije kubadilika.
Vilevile kuanzia leo unaweza kupima upendo kwa ndugu zako kwa kujaribu kuweka mawasiliano yenu sawa.
Mpigie simu kaka, mpigie simu dada, mpigie simu mjomba, nenda kamtembelee shangazi, rudi kijijini kwenu ukasalimie kidogo.
Punguza wivu na shukuru kwa hatua uliyopiga hadi sasa. Mshukuru Mungu kwa kukupa aina ya ndugu ulio nao bila kujali hali zao.
Usiwaseme ndugu zako vibaya. Ukikuta jina la ndugu yako linachafuliwa mtetee, kanusha habari za uongo zinazoongeleka dhidi yake.
Panga mikutano ya familia mara kwa mara hata kama ni WhatsApp group au ziara ndogo nyumbani.
Kaeni chini mjadili maendeleo ya mmojammoja jinsi ya kusaidiana na kuboresha hali ya familia kwa ujumla.
Kumbuka kwamba familia ndiyo msingi wa maisha yetu. Bila upendo wa ndugu, maisha yanakuwa magumu zaidi.
Hizi pesa, majumba na magari mazuri huku mjini zisitudanganye. Hawa marafiki wenye pesa kama sisi wasituzubaishe tukaona wao wana maana zaidi kuliko ndugu zetu.
Siku ukiugua atakayekuja kulala hospitali kukuuguza sio tajiri John, wala sio boss Joseph. Hao hawawezi kuacha miradi yao kwaajili yako. Waheshimu ndugu zako.
Je, unaonaje hali ilivyo kwenye familia yenu? Mambo safi au tukuache kwanza tunakutia hasira ? 😀
#No_learnig_No_earning
So We Have To Learn
Content By George Francis
#motivation #highlight #mrgeorgefrancis #viral