Kalenda ya udahili baada ya form four inaridhisha?

Kalenda ya udahili baada ya form four inaridhisha?

Masiya

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2012
Posts
7,602
Reaction score
7,341
Najiuliza vijana wamefanya mtihani wa form4 October mwaka jana, March/April (miezi 5/6 baadae) tumekuwa na uombaji wa kujiunga na masomo chini ya NACTE na Vyuo vikuu Vichache. Selection za F5 (advance) hadi sasa bado, zinategemewa mwezi huu wa sita-takribani miezi 7/8 toka vijana walipo maliza mitihani.

Raundi nyingine chini ya NACTE na Vyuo vikuu vinavyo toa certificate na diploma, ni kuanzia labda July /August na masomo kuanza October/November -takribani mwaka mzima baada ya mitihani ya F4. Hivi kweli tumeshindwa kufupisha muda wa vijana kukaa nje ya masomo kwa miezi yote hii?
Je hii inaridhisha?

Nakumbuka enzi hizo mtu alimaliza form four November na kupata selection mara moja na form 5 walikwenda January hata kabla ya majibu ambayo February /March yalitoka.

Najua zama hizo zimepita lakini naamini siyo lazima vijana wakae muda wote huo nje ya masomo.
 
Bandugu inaelekea hili jambo la kijana aliemaliza F4 kusubiri hadi mwaka mzima kwenda chuo/F5 sio kero kwetu. Ni maisha tu!!!!
 
Hii ni mbaya, mwanafunzi anapata mimba na kuzaa kabla ya kujiunga F5
 
In short, Tanzania yetu hii ipo hovyo sana kila idara
 
Back
Top Bottom