comrade igwe
JF-Expert Member
- Jan 12, 2015
- 7,295
- 3,950
Hayo yalisemwa bungeni juzi usiku na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais anayeshughulikia Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mh Angellah Kairuki alipokuwa anatoa ufafanuzi wa lini Serikali itaendelea kuajiri watumishi wa kada nyingine, kama ilivyoulizwa na Mbunge wa Viti Maalumu, Anna Lupembe (CCM).
“Azma ya serikali, kwanza kabisa hatuwezi kuajiri wananchi wote, tumekuwa tukisikia hapa wahitimu hawana ajira, wengine wanaendesha bodaboda… tunapopanga idadi ya watumishi wa kuajiriwa, tunaangalia mambo mengi, kuanzia mahitaji, vipaumbele hadi uwezo wa kibajeti.
“Tayari tumeshaanza kutoa vibali vya ajira zaidi ya watu 9,700 na tutaendelea kufanya hivyo, na hivi karibuni Rais amebariki kuajiriwa kwa madaktari wapya 258 na Jumatatu (keshokutwa) wanaripoti kazini.
Tutaendelea kuajiri na wataalamu wa kada nyingine, kabla ya kumalizika kwamwaka huu wa fedha mwezi Juni tutakuwa tumejiajiri kwa idadi tutakayoipanga kwaawamu, na katika mwakaujao wa fedha tutaendelea kuajiri watumishi wengine wa umma zaidi ya 52,436,” alisema.
Hata hivyo, alisisitiza Serikali itahakikisha hairudii makosa ya kuajiri watumishi hewa, wasio na sifa na weledi unaohitajika. Alisema kwakiasi kikubwa uhakiki wa watumishi wa umma kwa ujumla umekwisha, lakini kazi hiyo ni endelevu, kwani serikali itaendelea kufanya hivyo mara kwa mara.