Kaini na Abeli

Kaini na Abeli

Mwanamke wa mithali 31

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2024
Posts
1,345
Reaction score
3,120
NO REFORM NO ELECTION

1. Kaini na Abeli walikuwa watoto wa kwanza wa Adamu na Eva.

Kaini alikuwa mkulima alipanda mimea na mazao.

Abeli alikuwa mchungaji alifuga kondoo.

2. Wote wawili walimtolea Mungu sadaka:

Kaini alitoa mazao ya shamba.

Abeli alitoa mwanakondoo bora kabisa kutoka mifugo yake.

3. Mungu alimkubali Abeli na sadaka yake,
lakini hakukubali sadaka ya Kaini si kwa sababu Kaini alitoa mazao tu, bali kwa sababu moyo wake haukuwa wa unyenyekevu mbele za Mungu.

4. Kaini aliudhika na kujaa wivu, akamchukia ndugu yake Abeli.
Hatimaye, alimwua Abeli alipokuwa shambani,
Huu ukawa uuaji wa kwanza duniani.
Yaani kaini alikua binaadamu wa kwanza kufanya mauaji Duniani,

5. Mungu alimuuliza Kaini,

Abeli ndugu yako yuko wapi?
Kaini akajibu,
Sijui, kwahiyo mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?

6. Mungu akamlaani Kaini, akamwambia damu ya ndugu yake inapaza sauti kutoka ardhini.

Kaini akawa mtoro, akihangaika duniani bila amani,alikua akitanga tanga huku na huko
Damu ya ndugu yake ilimshtakia ardhini,

Lakini Mungu pia alimwekea alama ya kumlinda, ili mtu yeyote asimuue.

Haya umejifunza nini kutokana kwa Kaini na Abel ???

1. Mungu huangalia moyo, si tu kile tunachotoa.

2. Wivu na chuki vinaweza kusababisha maovu makubwa.

3. Tuna wajibu wa kuwa walinzi wa ndugu zetu kuwapenda, kuwajali, na kuwaheshimu.

4. Hata baada ya dhambi, Mungu bado ni mwenye rehema
(alimlinda Kaini licha ya kosa lake).
 
Asante kwa ujumbe, japo ni utatanishi tupu.
 
Mungu alimpenda Kaini licha ya kutokubali sadaka yake, Kaini alikuwa bahili sana . Mungu akafurahishwa na ujasiri wa Kaini kuliko sadaka yake. Abeli alimtolea Mungu vinono, Mungu akafurahishwa na sadaka ya Abel kuliko na Abel mwenyewe. Adhabu kubwa aliyopewa Kain ni kulaaniwa ardhi dhidi yake. Yaani alipigwa ban kwenye kilimo, lakini Kaini alifanikiwa sana kwenye kazi tofauti na kilimo. UK ina watu 70M lakini wakulima hawafiki 200k na ni nchi tajiri Duniani.
 
Back
Top Bottom