Kaini alivyomuua Habili alitokomea mbali huko alioa bint je alikua jamii gani naomba kujua

JITU LA MIRABA MINNE

JF-Expert Member
Mar 28, 2015
726
475
Ni swali tata kwangu,kwani Adam na Hawa walipoanzisha familia walimzaa kaini na Habili,Kaini kutokana na wivu wa sadaka zake kukataliwa na Mungu akamuua Habili kwa wivu kwa kua sadaka yake ilikubaliwa moja kwa moja,
Mara baada ya Kaini kuharibu kazi alitokomea safari ya mbali na Huko alioa bint wa kuitwa sijui nani je bint huyo alitoka jamii gani?nafunga breki naomba kujuzwa hapo
 
Biblia Haiweki wazi Sana kuhusiana na Hilo, Inasema Tu BAADAYE kaini Akalala na mkewe, Hii Baadaye Inaonyesha sio kipindi kilekile baada ya kulaaniwa na Mungu. Inaonekana Kuna kipindi kilipita na ndio akaja kuzaa na mkewake (Mwanzo 4:17)

Sasa Mkewake Alitoka wapi? Biblia haisemi, Ila Biblia Inaonyesha Adamu alikua na mabinti pia(Mwanzo 5:4), So huenda Kaini alijichagulia Kati ya Dada zake, Akaoa.

Hilo liliwezekanaje? Inaonekana katika mazingira flani Ilibidi Mungu Aruhusu mambo yanayoonekana sio ya kawaida ua ustaarabu yafanyike ili kutunza au kuendeleza Ukoo. Fikiria mfano wa wale mabinti wawili wa Loti Baada ya mama Yao kugeuka nguzo ya chumvi, walipoona Baba Yao anazeeka na hakuna mwanaume wa kuwazalisha waliamua kuzaa na Baba Yao(Mwanzo 19:31-36)

Hata Sara Mke wa Abrahamu mwenyewe alimruhusu kijakazi wake aitwaye Hagari azae na Mume wake maana alikua Tasa kabla Mungu hajamuwezesha kushika mimba ya Isaka(Mwanzo 16:3,4)

Katika Hali zote Mungu aliacha Tu iwe hivyo kutokana na mazingira, Ikiwa hangependezwa na uzao wa namna hiyo huenda angewaua. Kwahiyo Ikizingatiwa kwamba kwa kipindi Cha Adamu ilikuwepo familia yake Tu, Basi tunaweza kusema kwamba Kaini alimuoa Dada yake.

Hiyo Ni Tafakuri yangu Tu.
 
Wakati anaadhibiwa na kufukuziliwa mbali alimsihi Mungu amuonee huruma maana "watu huko niendako wakiniona wataniua " Mungu akamjibu nitakuwekea alama na hakuna mtu atayekugusa, by then watoto walokuwa wamezaliwa na Adam na Eva ni wawili tu hao watu Cain anaodai watamuua walitoka wapi?
 
He he he heeee.. Hapo kweye "watu" aliokua anawahofia Kaini, umenifikirisha, sikuwaza in deep, but Kesho nitajitahidi nije na jibu, saivi usiku Sana. Tutapata Tu Jibu ingawa kwa mbinde Sana.
 
Tukio la kuua kwa Kaini lionaongelewa miaka mingi baada ya kuanzishwa kwa familia ya kwanza ya Adamu na Eva.
Adamu hakuwa na watoto wawili pekee ila hapo walio tajwa hapo ni wale tu waliokuwa wateule wa Mungu Na wakwanza katika watule hawa alikuwa ni Habili(kaini anatajwa katika tukio la kumuua habili).
Baada ya Habili kufa maandiko yanasema
Adamu alipata mtoto mwingine mahali pa Habili(mbadala wa Habili ambaye ni mteule wa Mungu) akamuita Theti.
Hiki ndo kizazi cha wateule wa Mungu wakati wa Adamu.

Lakini adamu alikuwa na watoto wengi sana
Soma mwanzo 5,1-2.

Hivyo basi katika habari kuwa watu walitoka wapi ni kwamba kutokana na watoto wengi waliozaliwa katika familia ya Adamu, wakaanzisha familia nyingine ambazo nazo zilikuwa na vizazi vyao.
Na hizi familia walioana ndugu yaani kaka na dada kutoka kwenye familia moja ya Adamu.

Ndipo baada ya watu kuongezeka juu ya uso wa nchi ndipo Mungu alipotoa agizo la kukataza watu wasioe dada zao wa familia moja kwasababu hapakuwa na sababu tena.

"Basi MTU asioe UMBU lake"

Hiyo ni kwa mujibu wa bibilia mkuu
Kama nimekujibu swali lako hapo.
 
Tukio la kuuwawa kwa Kaini lionaongelewa miaka mingi baada ya kuanzishwa kwa familia ya kwanza ya Adamu na Eva.
Adamu hakuwa na watoto wawili pekee ila hapo walio tajwa hapo ni wale tu waliokuwa wateule wa Mungu Na wakwanza katika watule hawa alikuwa ni Habili(kaini anatajwa katika tukio la kumuua habili).
Baada ya Habili kufa maandiko yanasema
Adamu alipata mtoto mwingine mahali pa Habili(mbadala wa Habili ambaye ni mteule wa Mungu) akamuita Theti.
Hiki ndo kizazi cha wateule wa Mungu wakati wa Adamu.

Lakini adamu alikuwa na watoto wengi sana
Soma mwanzo 5,1-2.

Hivyo basi katika habari kuwa watu walitoka wapi ni kwamba kutokana na watoto wengi waliozaliwa katika familia ya Adamu, wakaanzisha familia nyingine ambazo nazo zilikuwa na vizazi vyao.
Na hizi familia walioana ndugu yaani kaka na dada kutoka kwenye familia moja ya Adamu.

Ndipo baada ya watu kuongezeka juu ya uso wa nchi ndipo Mungu alipotoa agizo la kukataza watu wasioe dada zao wa familia moja kwasababu hapakuwa na sababu tena.

"Basi MTU asioe UMBU lake"

Hiyo ni kwa mujibu wa bibilia mkuu
Kama nimekujibu swali lako hapo.
Bible iko very specific na very clear mkuu, kwamba Adam akamjua mkewe hawa "kwa mala nyingine tena"....hayo ya wateule na wasokuwa wateule ndo kule kwenye kusadikika aisee.
 
Mkuu namaanisha kwa Adamu alikuwa na watoto wengi tu.
" Adamu akaishi miaka mia kenda, akazaa wana waume kwa wake...." Soma mwanzo 5,1-2.
Ila sasa kuna watoto ambao walikuwa wakitajwa zaidi ambao ni kaini na Habili na Habili alipendwa zaidi na hata sadaka yake imepokelewa Zaidi kuliko ya Kaini.
Na hata Habili alipokufa bado maandiko yanasema Adamu alipata mwana Akamwita Theti mahali pa Habili.
Huyu Theti ndo aliye endeleza kizazi cha watakatifu hadi kufika kwa Nuhu.
Soma bibilia vizuri utaliona hilo ninalolisema.
Katika kila kizazi utakuta kuna mtoto mmoja ambaye atapewa kipaumbele kuliko wengine.

Utakuta mlolongo unaoeleza kuwa
Fulani akamzaa Fulani, akaishi miaka kadhaa, akazaa wana waume na wake akafa.

Angalio hilo mkuu
 
Bible iko very specific na very clear mkuu, kwamba Adam akamjua mkewe hawa "kwa mala nyingine tena"....hayo ya wateule na wasokuwa wateule ndo kule kwenye kusadikika aisee.
Ha ha ha haaaaa.. Kila nikiwaza hii thread nakosa usingizi kabisa.
 
Habari hizi hazina tofauti na zile story za Safina ya Nuhu....Ujue Hawa watu weupe wanataka kutuumiza vichwa tushindwe kuwafatilia babu zetu kina Mkwawa tukeshe kuwafilia Babu zao wao
Unajaribu kumaanisha "The Holy Bible" Ni fiction book Mkuu?
 
Wakati anaadhibiwa na kufukuziliwa mbali alimsihi Mungu amuonee huruma maana "watu huko niendako wakiniona wataniua " Mungu akamjibu nitakuwekea alama na hakuna mtu atayekugusa, by then watoto walokuwa wamezaliwa na Adam na Eva ni wawili tu hao watu Cain anaodai watamuua walitoka wapi?
Unajua adam na hawa walikuwa wanazaa watoto wangapi kwa mimba 1.?
Wakati cain na habil wana gombana unajua walikuwa na umri gani?
Unataka kusema baada ya kuzaliwa cain na habil adam na hawa hawakuzaa tena?
 
Ni swali tata kwangu,kwani Adam na Hawa walipoanzisha familia walimzaa kaini na Habili,Kaini kutokana na wivu wa sadaka zake kukataliwa na Mungu akamuua Habili kwa wivu kwa kua sadaka yake ilikubaliwa moja kwa moja,
Mara baada ya Kaini kuharibu kazi alitokomea safari ya mbali na Huko alioa bint wa kuitwa sijui nani je bint huyo alitoka jamii gani?nafunga breki naomba kujuzwa hapo
Kiongozi tafuta kwanza adam na hawa.walikuwa wanazaa watoto wangapi kwa mimba moja.
Alafu jiulize cain na habil walikuwa na umri gani walipogombana.unafikiri adam na hawa hawakuwa wamezaa watoto wengine?
Na ukumbuke kipindi binadamu ndo tumeletwa duniani kulikuwa hakuna UDADA TUNAKULAGA.
 
Habari hizi hazina tofauti na zile story za Safina ya Nuhu....Ujue Hawa watu weupe wanataka kutuumiza vichwa tushindwe kuwafatilia babu zetu kina Mkwawa tukeshe kuwafilia Babu zao wao
Safina hauamini nini?
 
Ni swali tata kwangu,kwani Adam na Hawa walipoanzisha familia walimzaa kaini na Habili,Kaini kutokana na wivu wa sadaka zake kukataliwa na Mungu akamuua Habili kwa wivu kwa kua sadaka yake ilikubaliwa moja kwa moja,
Mara baada ya Kaini kuharibu kazi alitokomea safari ya mbali na Huko alioa bint wa kuitwa sijui nani je bint huyo alitoka jamii gani?nafunga breki naomba kujuzwa hapo

Ni mwarab na ndiyo maana unaona mpaka leo hawana suluhu na wayahudi, wanauana na wataendelea kuuana mpaka kiama. Hapa Bongo mtu anaona fahari kujifananisha na mwarab, shida kweli kweli.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom