Wakuu salaam,
Huyu mkuu nakumbuka aliibua ushahidi wa ufisadi hasa ule wa kagoda, kitu kilichopelekea yeye kutiwa msukosuko na "watawala" hata kuhojiwa masaa kadhaa na kutakiwa kuwasilisha ushahidi huo kwa DPP. Naye bila kusita alifanya hivyo.
Sasa tangu wakati ule hatujasikia muendelezo wowote wa suala hilo na huyu mkuu Kainerugaba naye hatujamsikia tena. Je kulikoni?
Ushahidi wa Kainerugaba umefanyiwa kazi na wahusika?
Yeye mkuu Kainerugaba yupo wapi kwa sasa?
Note:
Mojawapo ya sababu zilizonifanya kumkumbuka huyu mkuu ni suala la Bw. Nahodha kumtaka Samwel Sitta kupeleka ushahidi kuwa Mh. Mwakyembe alipewa sumu. Nina hakika hata kama atapeleka ushahidi wa uhakika lakini kuna uwezekano mkubwa wa kuutia kapuni ushahidi huo kama ambavyo dpp amefanya katika masakata kibao huko nyuma. Kwani hata Mh. Mwakyembe alishawahi kuwakilisha ushahidi mara kibao wa yeye kutishiwa maisha lakini "watawala" waliishia kukejeli tu.