Egnecious
JF-Expert Member
- Jul 8, 2015
- 879
- 969
KAIMU MKUU WA MKOA DC HAPI *DAR INA CHAKULA CHA KUTOSHA*
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Ally Salum Hapi Pamoja na Kamati ya ulinzi na usalama Kanda maalum Ya Dar es salaam leo amefanya ziara ya kutembelea maghala ya chakula serikali na binafsi pamoja na masoko yaliyopo katika manispaa zote za jiji ili kujiridhisha na hali ya chakula kwa Mkoa wa Dar es Salaam.
Akizungumza mara baada ya ukaguzi maeneo ya Wakala wa Hifadhi ya Chakula Kanda ya Kipawa, Ghala la Chakula na Nafaka Gahala la NFRA kanda ya kipawa, Soko la Tandika, Soko la Buguruni, Soko la Tandale na Manzese,kaimu mkuu wa mkoa Hapi amesema ameridhishwa na hali ya chakula kwa Mkoa wa Dar es Salaam na kueleza kuwa chakula kipo cha kutosha ikiwemo mchele, mahindi, maharage na vile vyakula vyote vya kilimo cha kijani.
Hivyo hakuna uhaba wa chakula na tetesi za njaa na uhaba wa chakula ni hadithi za kusadikika, alisisitiza Hapi.
Hapi amewataka wakazi wa Dar es Salaam waendelee na shughuli za uzalishaji kwani wafanyabiashara wote wamemuaminishia kuwa chakula kipo na hawana desturi ya kuficha chakula na mfanyabishara atakayefanya hivyo atachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kosa la uhujumu uchumi na serikali itaendelea kuwaunga mkono.
Pia kuhusu kamata kamata ya magari ya wafanyabishara amemuagiza Kamanda Siro kufuatilia suala na kuzitaka mamlaka zinazofanya hivyo kuacha mara moja, na wanaosambaza taarifa za uhaba wa chakula na njaa serikali itahakikisha inawashughulikia kwani wanaleta taharuki kwa wananchi.