Goliath mfalamagoha
JF-Expert Member
- Aug 3, 2012
- 602
- 2,505
KAIMU MHANDISI MKUU WA KITENGO CHA UJENZI MANISPAA YA ILALA AWAJIBISHWA.
Kamati ya Fedha na Utawala ya Baraza la Madiwani la Manispaa ya Ilala, Jijini Dar es Salaam imemwajibisha Kaimu Mhandisi Mkuu wa Kitengo cha Ujenzi wa Manispaa ya Ilala Eng. Japhary Bwigane kutokana na utendaji kazi mbovu.
Sanjari na hatua hiyo, watumishi wengine wa kitengo hicho waliowajibishwa ni Eng.Siyajali Mahili na Daniel Kirigiti ambao ni wasaidi wa mkuu huyo.
Watumishi hao wote watatu wanatuhumiwa kwa usimamizi mbovu wa miradi mbalimbali chini ya kitengo hicho. Kitengo hicho chini ya Eng. Bwigane kimekuwa na utendaji kazi usioridhisha kwa muda mrefu ikiwemo usimamizi mbovu wa ujenzi wa barabara za Manispaa ya Ilala hivyo kupelekea kujengwa chini ya kiwango, miradi kutokamilika kwa wakati ikiwemo daraja la Bonyokwa kuchelewa kukamilika kwa wakati.
Baadhi ya barabara zilizojengwa chini ya kiwango ni Ukonga barabara ya Moshi baa, tabata st. Mary's nk.
Uamuzi huo ulifikiwa na kamati ya fedha na utawala kufuatia kikao kilichofanyika tarehe 18/04/2016 siku ya jumatatu katika ukumbi wa manispaa hiyo
Akizungumza na waandishi wa habari hii leo ofisini kwake Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala mhe. Charles Kuyeko CHADEMA/UKAWA juu ya uamuzi huo alisema Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala ameelekezwa kuendelea na taratibu za kinidhamu juu ya watumishi hao ikiwemo kushushwa vyeo.
Mstahiki Meya, mhe.Charles Kuyeko ametumia fursa hiyo kuwaasa watumishi wa Manispaa hiyo kutekeleza majukumu yao kwa kufuata sheria, kanuni, taratibu na miongozo ya utumishi wa umma, na kuwaeleza kuwa hakuna atakayevumiliwa kwa kutofuata sheria, kanuni, miongozo na taratibu zilizowekwa.
Naye Naibu Meya, mhe. Kumbilamoto
akiongea katika mkutano huo na waandishi wa Habari amewaasa watumishi wa Manispaa hiyo wawe na moyo wa kupenda kufanya kazi na wajitume katika kutimiza majukumu yako kwa mujibu wa taratibu za ajira zao.
Aidha mhe. Kuyeko amewahakikishia wananchi wa Manispaa ya Ilala kuwa yeye na baraza la madiwani ambalo linaloongozwa na UKAWA watahakikikisha Idara zote na vitengo vinafanyakazi kwa ufanisi wa hali ya juu, Mtendaji yeyote mbovu hatavumiliwa.
Imetolewa na;
Alex D. Massaba
Katibu wa Meya Manispaa ya Ilala, DSM.