Kagera Sugar waendeleza ubabe dhidi ya Simba uwanja wa Kaitaba, Wainyuka mabao 2 - 1

Danny greeny

JF-Expert Member
Feb 6, 2014
3,856
1,645
FULL TIME| Kagera 2 - 1 Simba
27' Mbaraka Yusuph (Kagera)
45' Edward Christopher (Kagera)
65' Muzamiru Yassin (Simba)


Dk 90, Dakika 5 za nyongeza

Dk 83, mkwaju wa faulo anapiga Banda unawagonga mabeki na kuwa kona. Inachongwa, Kaseja anadaka

SUB Dk 82, Ally Ramadhani anaingia upande wa Kagera kuchukua nafasi ya Ame Ali

Dk 82, Fakhi anaokoa na kuwa kona, Simba wanachonga na kuwa kona, inachongwa hapa Kazimoti anadhibitiwa na inaokolewa

SUB Dk 81, Simba wanamtoa Kichuya na nafasi yake kuchkuliwa na Mwinyi Kazimoto

Dk 81, Mo Ibra anaachia mkwaju mkali hapa lakini Kaseja anadaka kwa ufundi kabisa na kuutoa nje kwa kuwa Ame Ali yuko chini

SUB Dk 76, Themi Felix anaingia kuchukua nafasi ya Edo Christopher

Dk 71, Simba wanapata kona nyingine, inachongwa na Kichuya lakini Kagera wanaokoa

Dk 69, Simba wanapata kona, Kichuya anaichonga inaokolewa na Matogolo na kuwa kona, inachongwa tena na Kaseja anadaka vizuri

Dk 67, Mavugo anapiga shuti sentimeta chache linapita juu

SUB Dk 66, Kagera wanamtoa Makarai anaingia Anthony

Goal DK 65, Muzamiru Yassin anaipatia Simba bao

SUB Dk 58, Simba wanamtoa Ndemla na nafasi yake inachukuliwa na Liuzio

KADI DK 57, Mkude analambwa kadi ya njano kwa kuzozana na mwamuzi msaidizi

Dk 52, Simba wanafanya shambulizi jingine, lakini Fakhi anaokoa na kuwa kona. Kaseja yuko chini pale

Dk 50, kona safi ya Kichuya, Kaseja anaruka na kudaka vizuri kabisa

Dk 49, Kichuya anaachia mkwaju mkali kabisa, Kaseja anaokoa vizuri na kuwa kona.

Dk 48, krosi nzuri ya Muzamiru lakini hakuna mtu hapa, Mavugo anajaribu kuuwahi

Goal Dk 45, Mechi inaanza kwa kasi na Edward Christopher anafunga bao safi kabisa kwa shuti kali baada ya mabeki wa Simba kuzubaa

HALF TIME: Kagera 1 - 0 Simba

SUB Dk 58, Simba wanamtoa Ndemla na nafasi yake inachukuliwa na Liuzio

KADI DK 57, Mkude analambwa kadi ya njano kwa kuzozana na mwamuzi msaidizi

Dk 52 Simba wanafanya shambulizi jingine, lakini Fakhi anaokoa na kuwa kona. Kaseja yuko chini pale

Dk 50, kona safi ya Kichuya, Kaseja anaruka na kudaka vizuri kabisa

Dk 49 Kichuya anaachia mkwaju mkali kabisa, Kaseja anaokoa vizuri na kuwa kona.

Dk 48, krosi nzuri ya Muzamiru lakini hakuna mtu hapa, Mavugo anajaribu

Dk 45, Edward Christopher anafunga bao safi kabisa kwa shuti kali baada ya mabeki wa Simba kuzubaa

Dk 45 sasa, Kaseja yuko chini akiendelewa kutibiwa baada ya kuokoa shuti la Banda

Dk 44, Banda anapanda akigongewa mpira, anafika ndani ya 18 anapiga shuti lakini Kaseja anapangua hapa

Dk 40, mpira wa adhabu wa Ajibu unatoka sentimeta chacge kwenye lango la Kagera

Dk 36 krosi nzuri kabisa ya Edo, Ame Ali Zungu anaruka na kupiga kichwa mbele ya Banda. Unatoka nje kidogooooo

Dk 34, Muzamiru anawageuza mabeki wa Kagera na kutoa pasi nzuri kwa Ajibu, anapaisha juuuuu

Dk 32, mpira umesimama kwa kwua kuna mchezaji wa Kagera anatibiwa

Dk 30, Bao hilo linaonekana kuanza kuwapa presha Simba ambao wanacheza haraka bila ya kuwa na umakini

GOOOOOOOO Dk 27, Mbaraka anageuka, nje ya 18, anaachia shuti kali kabisa na mpira unajaa wavuni

Dk 25, Mavugo anapata nafasi lakini shuti lake linakuwa kuubwa

Dk 23, Kagera wanapata kona hapa baada ya Juuko kuutoa mpira, inachongwa hakuna kitu

Dk 21 Semvuni wa Kagera naye anajinyoosha lakini shuti lake linakuwa kuuuuubwaaaa

Dk 19, Ndemla anageuka na kuachia shuti kali lakini linatoka juu sentimeta chache

Dk 17 Ndemla katika nafasi nzuri anaachia shuti lakini Kaseja anaokoa na kuwa kona, inachongwa na Kichuya lakini wanaokoa

Dk 16, Mavugo anageuka na kuachia shuti kali kabisa lakini mpira unaokolewa na Fakhi

Dk 10 Zimbwe anafanya kosa kubwa kwa kupiga mpira mfupi wa kichwa lakini shuti la Mangoma linaokolewa na Agyei

Dk 8, Kichuya anaingia na kuachia shuti kali lakini goal kick

Dk 6, Simba wanaaanza kupanga mashambulizi upya lakini inaonekana Fakhi yuko vizuri

Dk 4 sasa, Kaseja yuko chini dakika ya pili akiwa anatibiwa. Inaonekana ni baada kupangua shuti la Ndemla

Dk 2, Ndemla anageuka na kuachia mkwaju mkali kabisa hapa, lakini Kaseja anaonyesha umahiri, anapangua kwa ufundi kabisa na kuwa kona

Dk 1, mpira umeanza taratiibu kila upande ukionekana unataka kufanya vizuri.

KIKOSI CHA KAGERA

Gk-Juma Kaseja-1
2. Godfrey Taita-20
3. Mwaita Gereza-21
4 .Juma Shemvuni-25
5. Mohamed Fakhi-23
6. George Kavila-15 (C)
7. Seleman Mangoma-2
8. Ame Ally-9
9. Edward Christopher-28
10. Mbaraka Yusuph-24
11. Japhet Makalai-27

Subs
Gk-John Mwenda-30
2. Hassan Khatibu-19
3. Eradius Mfulebe-29
4. Antony Matogolo-26
5. Ally Ramadhan-13
6. Themi Felix-17
7. Paul Ngalyoma-8
KIKOSI CHA SIMBA
Gk-Daniel Agyei-1
2. Mzamiru Yassin-19
3. Mohamed Hussein-15
4. Abdi Banda-24
5. Juuko Murshid-6
6. Jonas Mkude-20 (C)
7. Shiza Kichuya-25
8. James Kotei-3
9. Laudit Mavugo-11
10. Said Ndemla-13
11. Ibrahim Ajib-23

Subs
Gk-Peter Manyika-30
2. Novalt Lufunga-21
3. Mwinyi Kazimoto-8
4. Pastory Athanas-16
5. Jamal Mnyate-14
6.Mohamed Ibrahim-4
7. Juma Liuzio-10

C
redit: SalehJembe Blog

Picha

k1.jpg
K2.jpg
k3.jpg
k4.jpg
k5.jpg
k6.jpg
 
Kwa wale mnaobet matokeo ni Kagera 1 - 2 Simba kwa mujibu wa Dalali wa Mechi golikipa wa zamani maarufu wa Simba ambae leo nahisi anadakia timu Pinzani
 
Naamini Kagera itatwaa ushindi au Simba watalazimisha sare.
 
Taita mwamba

Dah George kavila nilikuwa napenda sana kumtizama enzi hizo villa squad




Kagera kazi kwenu
 
Back
Top Bottom