kbm
JF-Expert Member
- Oct 5, 2012
- 5,224
- 1,687
Dar es Salaam.
Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2014/15 itaanza keshokutwa huku ratiba ya ligi hiyo ikizipa nafasi za kusafiri umbali mfupi zaidi timu za Ruvu Shooting, Azam na Yanga wakati Kagera Sugar, Mbeya City, Polisi Morogoro na Stand United ndizo zitakazosafiri umbali mrefu zaidi.
Kwa mujibu wa hesabu zilizofanywa na gazeti hili kwa kutumia programu ya kupima masafa (umbali na muda) yaani GPS ‘Global Positioning System' kujua umbali uliopo kati ya uwanja fulani na timu inapotokea kwenda kucheza mechi, zimejulikana timu hutumia kilomita ngapi kutoka sehemu moja hadi nyingine.
Ligi Kuu ina timu 14 na kila moja itacheza mechi 26 mpaka ligi kukamilika kwa kutumia viwanja 10. Timu hizo 14 za Ligi Kuu zinatoka mikoa minane na kila timu itacheza nyumbani na ugenini, lakini kati ya hizo, timu saba zinatoka Ukanda wa Mashariki ya Tanzania kwenye mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Morogoro, wakati timu tano zilizosalia; mbili zinatoka Tanga ambao ni Ukanda wa Kaskazini, nyingine mbili zinatoka Kanda wa Ziwa huku timu moja ikitoka Ukanda wa Kusini na mbili zikitoka Kanda ya Nyanda za Juu Kusini.
Uwepo wa timu nyingi za sehemu moja kwenye ligi unachangia kufanya timu zinazotoka mbali na eneo hilo kusafiri zaidi ili kucheza nazo.
Pia upangaji wa ratiba ya ligi huchangia timu kusafiri umbali mrefu na nyingine mfupi. Mfano Simba, Yanga na Azam katika mzunguko wa kwanza kwenye michezo 13 zitacheza michezo mitatu hadi minne nje ya Dar es Salaam wakati michezo tisa hadi 10 itachezwa Dar es Salaam.
Vilevile timu zinazotoka mkoa mmoja zitasafiri kwa tofauti ya hadi kilomita 1,000, kwani Mbeya City itasafiri kwenda Dar es Salaam na kucheza na JKT Ruvu, Azam na Simba, lakini Tanzania Prisons inayotokea Mbeya pia itacheza Dar es Salaam mchezo mmoja itaenda Tanga kucheza na Coastal Union kisha Dar es Salaam kucheza na Simba.
Yafuatayo ni makadirio ya umbali utakaotumiwa na timu msimu huu:
Kagera Sugar itasafiri km 21,123 kwa msimu huu, mzunguko wa kwanza km 7,493 wa pili km 13,630.
Mbeya City km 16,266, (mzunguko wa kwanza km 9,546 wa pili km 6,720).
Polisi Moro km 15,632, (mzunguko wa kwanza km 2,619 wa pili km 13,013).
Stand United km 15,572 (mzunguko wa kwanza km 5,590 wa pili km 9,982).
Ndanda FC km 14,462 (mzunguko wa kwanza km 8,461 wa pili km 6,001).
Chanzo: Mwananchi