"Kagera na falsafa ya serikali na hatima ya Baadaye"

Mlyamimbo

Member
Oct 24, 2014
59
34
Habari za mwaka mpya wanaforum?Nimeona na mimi leo niitazame kidogo falsafa ya serikali na mtazamo wake juu ya wahanga wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Katika nyakati tofauti serikali ya jamuhuri imekuwa ikitoa kauli nzito na zakukatisha tamaa kwa wahanga wa tetemeko la ardhi huko Kagera, kwa upande wangu Sina shida sana na kauli za viongozi wangu nyingi zenye utata zilizopita ila kwa hii ya "Serikali siyojukumu lake kujengea wananchi nyumba zao" Nikauli sahihi inayotumika katika mazingira yasiyo sahihi.

Nikweli kabisa serikali kazi yake nikutengeneza mazingira rafiki ya raia wake kuweza kujiendeshea maisha yao wenyewe(at normal condition), lakini wahanga wa kagera ni raia lakini mazingira yaliyowakumba kwa serikal makini inayomuogopa mungu lazima iwachukulie zaid ya sifa ya uraia wao (special citizen) mpaka pale hali yao ya maisha itakaporejea kwenye normal situation.

Lakini kitendo cha serikali kusema haina wajibu wa serikali na kurekebisha tu miundo mbinu na ofisi za serikali(that is not good),Kwa busara serikali ilipaswa kuwaweka both in consideration(infrastructure & people), "A good leader invest in people & not building's, na siku zote mazoe hujenga tabia watawaliwa wasipopiga kelele kwenye Jambo hili Basi hii itageuka kuwa tabia ya serikali. Kuna siku kutatokea jaga jingine let say mulipuko wa ugonjwa(kipindupindu) na serikali itatoa msaada kwa watumishi wa umma tu kwasababu siyojukumu lake kutoa matibabu kwa raia(na huko ndiko tunakoelekea).

Ngoja niachane nahayo kwasababu siyo jukumu la serikali kuwajengea raia(wahanga) wake nyumba, swali: kama siyojukumu la serikali kuwajengea raia wake(wahanga)nyumba, je nijukumu la serikali kupanga matumizi ya pesa ambayo siyo yake?

Swali: Kama serikali siyo jukumu lake kusaidia wahanga, je na raia hawaruhusiwi kusaidia raia wenzao waliopatwa na maafa?

Swali: Serikali ya awamu hii bado inalegitimacy ya kuchangisha watu kusaidia wahanga wa majanga mbali mbali?

Swali: Kama sijukumu la serikali kujengea wahanga(raia) nyumba, je nijukumu la raia(wananchi) kulipa Kodi at the same time kuchangia serikali ikipatwa na maafa?
Swali: Kati ya serikali na raia Nani alipatwa na majanga?

Mimi bado napata mkanganyiko kidogo juu ya swala hili when we let it pass like this litatutafuna huko mbeleni, kwa sababu serikali itakuwepo kwaajili ya serikali and not citizen.

"Tusipoziba ufa tutajenga ukuta"
"Mazoe hujenga tabia"
 
Maswali haya magumu kama chuma cha pua. Safi sana mkuu kwa kuitumia siku yako ya leo vizuri, sijuhi ingekuwaje binadamu sote tukatumia hata 0.25% ya ubongo wetu kufikilia mambo ya muhimu kiasi hiki
 
Kumbe wakina ngaiza waliotaka kupindua serikali waliona mbali ona mkoa huu unavyonyanyaswa kiasi hiki wanaharakati uteteeni mkoa huu
 
Hoja nzito iliyokuja kwa wakati wake.Mvua hakuna njaa iko njani.Lazima laana itatutafuna tu ndipo tujivunze kudhibiti ndimi zetu. Wana Kagera hawakuomba ukimwi wala tetemeko na sasa hatujaomba mvua zisinyeshe tutakujajutia kauli zetu muda si mrefu.Ee Mwenyezi Mungu tunusuru.
 
Back
Top Bottom