Kafulila azua balaa bungeni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kafulila azua balaa bungeni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sulphadoxine, Jul 13, 2011.

 1. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #1
  Jul 13, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Tuesday, 12 July 2011 22:01 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]0diggsdigg

  WABUNGE WATAHARUKI, WASEMA BILA MPANGO
  Leon Bahati na Habel Chidawali, Dodoma
  MBUNGE wa Kigoma Kusini, Davidi Kafulila (NCCR-Mageuzi), amezua balaa bungeni baada ya kutoa kauli iliyozua mjadala mkali bungeni, huku wabunge wa CCM wakiomba mwongozo wa mwenyekiti na kumtaka afute kauli.

  Akichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa mwaka 2011/12 jana, Kafulila alisema Serikali imekuwa legelege na ndiyo maana imeshindwa kukusanya kodi za kutosha na kutoa huduma duni za afya nchini.Kauli hiyo ilizua mtafauruku huku wabunge wa CCM wakimtaka afute kauli lakini alikataa.

  Kufuatia mtafaruku huo ulitokana na wabunge kuanza kuzungumza bila mpangilio, Mwenyekiti wa Kikao cha Bunge, Jenista Mhagama, kuhairisha kikao dakika saba kabla ya wakati ili kupunguza mvutano uliokuwepo.Wakati Mhagama anatangaza kuhairisha kikao sehemu kubwa ya wabunge wa CCM na upinzani walikuwa wamesimama wakiwa na shauku ya kuomba mwongozo wa mwenyekiti kuhusiana hoja hiyo.

  Mvurugano
  Kabla ya kuahirisha kikao, Mhagama alitoa fursa ya mbunge au waziri kuchangia, lakini kulikuwa na sauti zilizokuwa zinasikika kupitia vipaza sauti za wabunge waliokuwa wamewasha vinasa sauti kinyume na taratibu za Bunge.Maneno ya wabunge yaliyokuwa yanasikakika ni kama vile: "…cha ubishi…", "…so what…," "…hiyo siyo taarafa…," "…hujui…" "Nani hana heshima nani, hana heshima…"

  Hata Kaimu Kiongozi Mkuu wa Shughuli za Serikali Bungeni, Samwel Sitta aliposimama kujaribu kuokoa jahazi, kauli yake ilionekana kama kamwaga petroli kwenye moto, kwani wabunge waliendelea kubishana bila utaratibu. Hata Mhagama aliposimama ili kutoa ufafanuzi, alivurugugwa na sauti za wabunge zilizokuwa zinampinga kupitia kwenye vipaza sauti.

  Baada ya kuona hivyo alisema: "Hata kama mnazungumza huko, kauli ninayoitoa mimi ndiyo yenye nguvu, kwa kuwa ni Spika wa kikao hiki."Pamoja na Mhagama kusisitiza kuwa anaposimama kuzungumza, au mtu mwingine anapopewa ruhusa na Spika, au Mwenyekiti kuzungumza, mtu mwingine hairuhusiwi kuwasha kinasa sauti na kuzungumza, wabunge hawakuvizima.

  Chazo cha mvutano
  Kuchafuka kwa hali ya hewa kulianza hivi; Kafulila alipewa fursa ya kuchangia hotuba ya Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, alisema fedha zilizoombwa na Wizara ni kidogo sana kwa sababu ni sawa na asilimia 10 ya mapato yote ya Serikali, kiwango ambacho ni kinyume na maazimio ya Abuja ambayo Tanzania imesaini.

  Alisema maazimio hayo yanaelekeza nchi kutumia asilimia 15 kwa ajili ya huduma za afya."Serikali imekosa dhamira ya kutekeleza mipango mizuri ambayo itasaidia Huduma za Afya," alilalamika Kafulila na kuongeza kuwa wanaoumia ni walalahoi.Alipandisha hasira za wabunge wengi aliposema Serikali imekuwa haiwaonei huruma Watanzania wengi wanaoteseka kwa kukosa matibabu, kwa vile wao wana mishahara mikubwa ambayo inawawezesha kutibiwa mahali popote wanapotaka.

  Alitoa mfano kuwa Sitta na familia yake kuwa hawana tatizo kuhusu tiba kwa sababu wanaweza kutibiwa popote.Alisistiza kuwa uwezo wa Tanzania kuweza kuiwezesha sekta ya afya nchini na kutoa huduma bora ipo, lakini Serikali imekuwa ikizembea hata katika suala la ukusanyaji wa kodi.

  Alijenga hoja zake huku akinukuu jarida linalochanganua mambo ya kiuchumi duniani la Economist, kitabu cha taarifa za Serikali na kauli alizowahi kuzitoa Baba waTaifa, Mwalimu Julius Nyerere.Alisema kwamba, Tanzania inatimiza miaka 50 ya Uhuru huku wakishindwa kuboresha huduma za afya, lakini akasema hamlaumu Waziri wa Afya kwa sababu suala hilo halipo ndani ya uwezo wake.

  Akasema takwimu zinaonyesha kuwa hapa nchini hakuna uwiano mzuri wa kitaalamu kati ya idadi ya daktari na Watanzania.Alisema zamani watoto wa wabunge na wakurugenzi walikuwa wakitibiwa kwenye hospitali za Serikali, lakini sasa wanatibiwa kwenye hospitali za kisasa za sekta ya binafsi ambako dawa zipo kwa wingi.

  Utetezi wa mawaziri
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige, alipopewa nafasi alisema maelezo ya Kafulila siyo ya kweli kwa sababu familia yake wakati wote inatibiwa katika hospitali za Serikali.Wakati anazungumza hayo, zilisikika sauti kwenye vipaza sauti zikisema: "Hiyo siyo taarifa! Hujui! Wabunge wote wanaweza."

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji), Dk Mary Nagu naye alisimama na kutetea hoja ya Maige akisema kuwa siku zote amekuwa akijitahidi kuboresha huduma za hospitali ya Serikali iliyopo jimboni kwake.

  Mhagama
  Mhagama alimtaka Kafulila aendelee kuchangia, lakini awe mwangalifu na kauli zake ambazo zinaweza kusababisha utata.Kafulila alisimama na kutetea kauli yake akisema: "Mimi nasema mbunge ana uwezo wa kutibiwa sehemu yoyote, iwe nchini au nje ya nchi. Ndiyo maana hamuwekezi vizuri kwenye sekta ya afya."

  Dk Kigwangalla
  Baada ya kumaliza, Dk Hamis Kingwangalla (Nzega-CCM) alisimama na kuomba mwongozo wa Spika akisema Kafulila ametoa lugha ya maudhi dhidi yake, chama chake cha CCM na Serikali yake aliposema kuwa, serikali legelege hushindwa kukusanya kodi.Kigwangalla alisema, siyo kweli kwa sababu takwimu zinaonyesha kuwa makusanyo ya kodi yamekuwa yakiongezeka kwa kadri muda unavyokwenda.

  Mhagama ilibidi amtake Kafulila ajibu hoja ikiwezekana aifute, lakini wakati huo kulikuwa na wabunge kadhaa waliokuwa wanaomba muongozo wa Mwenyekiti.Mhagama aliwanyamazisha akisema; "Huwezi kutoa muongozo juu ya muongozo mwingine. Subiri kwanza ajibu ndio uombe nafasi."

  Kafulila alijibu akisema hayupo tayari kufuta kauli yake kwa vile ukweli ni kwamba, mazingira halisi hapa nchini yanampa mbunge yeyote kutibiwa popote na hata ikiwezekana nje ya nchi.Alisema wabunge wengi hawatibiwi kwenye hospitali za Serikali ndiyo maana hawaoni umuhimu wa kutenga fedha za kutosha ili kuboresha huduma za afya.Kuhusu kauli kwamba, Serikali ni legelege na imeshindwa kukusanya kodi, alisema maneno hayo siyo yake, bali ni ya Baba wa Taifa.


  Mhagama alimpa nafasi Sitta kwa kuwa anakaimu nafasi ya Waziri Mkuu bungeni, lakini hoja yake ilimalizika kwa kuonyesha shauku ya wabunge wa upinzani kutaka kuomba muongozo wa spika.Sitta aliwataka wabunge wa CCM kutoendelea kubishana na wabunge wa kambi ya upinzani kwa sababu ya kutoa maneno ya kuudhi dhidi ya Serikali iliyopo madarakani ni wajibu wao.

  "Nawasihi wenzangu wa CCM wasihangaike kubishana kwa sababu kauli za kuundhi ni kazi yao. Ukishindana nao utapata shida bure," alishauri Sitta.Lakini Sitta aliwasha moto zaidi aliposema kwamba, wabunge wa kambi ya upinzani ni wanafiki kwa vile wamekuwa wakitoa kauli nyingi za namna hiyo.Sitta alisema hivi karibuni wabunge hao wa kambi ya upinzani walisema bungeni kuwa posho za wabunge ni kuwaibia wananchi lakini wanazipokea.

  Baada ya hapo wabuge waliendelea kubishana bila utaratibu, mpaka muda wa kikao ulipokaribia kwisha alitumia madaraka yake kuahirisha kikao hicho akisema: "Sasa muda umekwisha Nanahairisha shughuli za Bunge hadi jioni."Baada ya hapo wabunge walikaa kimya hadi alipotoka ukumbini na baadhi ya wabunge wakalipuka na kuanza kuimba wakisema: "CCJ! CCJ! CCJ!…."

  Ole Sendeka ataka bunge livunjwe
  Katika hatua nyingine Mbunge wa Simanjiro, Chrispher Ole- Sendeka (CCM), amemtaka Rais wa Jakaya Kikwete kutumia nafasi yake na kulivunja Bunge mara moja ili warudi katika uchaguzi kwa kile alichokieleza kuwa Bunge limejaa wahuni wengi.Ole Sendeka alitoa kauli hiyo jana nje ya viwanja vya Bunge wakati akizungumza na Mwananchi kufuatia mjadala mkali uliozua mabishano wakati wa kujadili hotuba ya bajeti ya Wizara ya afya na Ustawi wa Jamii.Sendeka alisema Bunge limekosa mvuto na hata jamii inayowasikiliza wanaona kuwa hakuna maana yoyote ya kuwa na Bunge ambalo limekosa mwelekeo kama ilivyo sasa kwa bunge la kumi.

  Mwanasheria Mkuu
  Hata hivyo, kauli ya Sendeka ilitofautiana na maoni nya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema, aliyesema kuwa suala la malumbano ndani ya ukumbi wa Bunge ni kitu cha kawaida na kwamba halipaswi kuchukuliwa kama ni jambo kubwa kiasi hicho.“Hapa sio jambo kubwa sana, wala sioni sababu za kusema ichukuliwe hatua gani kwakuwa mahali popote ambako kuna mabunge ya vyama vingi, lazima vitu kama hivi vitokee kwa hiyo naona ni vitu vya kawaida
  kabisa,’’ alisema Werema
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. eucalyptos

  eucalyptos JF-Expert Member

  #2
  Jul 13, 2011
  Joined: Jan 23, 2010
  Messages: 381
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Mimi nashauri mheshimiwa Makinda akaongezee elimu juu ya kufundisha "KINDAgateni" maana anajitahidi but bado.
  Anyway, ukweli ukitajwa wale wanaofaidi hapo "wanakuwa wakali kama mbogo na wanapewa nafasi"? hasa wale wa kujivua.... Mbona sikusikia SITA akiambiwa afute kauli yake mbovu?

  Mungu ikumbuke tanzania na wafute wote wanaowakandamiza tanzania kila kukicha....AMEN!
   
 3. n

  nkomelo JF-Expert Member

  #3
  Jul 13, 2011
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 212
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Sita ameanza kujimaliza mwenyewe, alikuwa mahali pazuri kwenye medani ya siasa, bahati mbaya ameingia mkenge sasa anaanza kujimaliza mwenyewe kwa kucheza mchezo ule ule ulio wamaliza wengine wa kuibeba ccm ili hali wao walimtema na kumfanya dhalili. Namshauri mzee wetu, alifanya vizuri aliweka historia wengi wanakumbuka. angeacha kucheza na Nyani kwenye shamba la mahindi na atarajie mavuno.
   
 4. Nyuki

  Nyuki JF-Expert Member

  #4
  Jul 13, 2011
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hapa mh.olesendeka kachemka, kutofautiana kimtazamo na kiitikadi miongoni mwa wabunge ni jambo la kawaida na si uhuni bravo AG.Werema
   
 5. mchemsho

  mchemsho JF-Expert Member

  #5
  Jul 13, 2011
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 3,158
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Ukweli mchungu.!
   
 6. n

  nyamagaro JF-Expert Member

  #6
  Jul 13, 2011
  Joined: Feb 25, 2010
  Messages: 385
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  Hii ya CCJ!, CCJ ni kiboko, nadhani ililenga kuonyesha unafiki wa Mr 6.
   
 7. M

  Mghaka JF-Expert Member

  #7
  Jul 13, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 320
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hivi mbunge anayeangalia kwa jicho la siasa kinzani na chama tawala wabunge wa ccm walitegemea aseme nini? hivi kusema serikali ni legelege inatosha kwa mbunge`mwelevu kuomba Taarifa kwa spika? mbona ccm wanachochea ghasia bungeni. Wanajifanya mawakili wa serikali mpaka wanatia kichefuchefu. Hivi kiapo chao kilikuwa kuilinda serikali? wao wakifanya hivyo mawaziri watafanya nini? ni lini serikali itawajibika kwa Bunge kwa niaba ya wananchi? Mungu awabariki wabunge wa CCM
   
 8. JamboJema

  JamboJema JF-Expert Member

  #8
  Jul 13, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,148
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Nashindwa kuelewa mantiki ya wabunge kuimba CCJ! Walikuwa wabunge wa upinzani au CCM? Hii yaweza kuwa walikuwa wanatuma ujumbe kwa Sitta? Sielewi.
   
 9. F

  FUSO JF-Expert Member

  #9
  Jul 13, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,858
  Likes Received: 2,336
  Trophy Points: 280
  Sita asahau milele kuwa Raisi wa nchi hii. CCJ founder - aibu tupu mtu mzima.
   
 10. T

  Triple DDD Senior Member

  #10
  Jul 13, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 151
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kazi ipo, mzee wa CCJ anataka umaarufu sana kumfunika Pinda sasa imekula kwake.

  Unajua jamaa alitaka kuja CHADEMA akaahidiwa uwaziri akatimu na press conference ilikuwa
  imeandaliwa akazuiwa na usakama wa taifa baada ya Kutoswa na mafisadi.

  Alitumia nguvu kumtosa lowasa while ilikuwa ni deal ya CCM richmond. EL nae akamtosa Uspika
  Mkuki kwa nguruwe. Hana lolote ni wale wale tu
   
 11. W

  Willegamba Member

  #11
  Jul 13, 2011
  Joined: Apr 14, 2011
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama ccm na ccj walitafsiri kafulila ni kafulia wacheze sebene mziki unafuata. Namuunga mkono 100% mh. Kafulila kuwa Serikali iliyopo madarakani ni legelege maana kila kona mambo ni legelege sio ktk elimu, afya, umeme, uwekezaji kila kona ni siasa badala ya utendaji na uwajibikaji. Sita haniumizi kichwa maana alishalegalega tangu ccj nae gamba ccm.
   
 12. s

  sativa saligogo Senior Member

  #12
  Jul 13, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 126
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu, akina 6 na ccm wanajipanga upya cdm shold ready btn the lines???? ulitegemea 6 atakaimu u-Waziri Mkuu???? suala hapa si kujadili matukio ni hoja za nguvu na kujipanga kabla ya bomb-shed!!
  dont underate the opponent even though is blind!!!!
   
Loading...