chakii
JF-Expert Member
- Sep 15, 2013
- 21,694
- 28,935
MBUNGE wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR Mageuzi), ameanza ziara ya wiki mbili mkoani Kigoma, akiambatana na Katibu Mkuu wa chama hicho, Mosena Nyambabe wakipeleka kwa wananchi sakata la ufisadi wa sh. bilioni 200 za akaunti ya Escrow inayowakabili vigogo wa serikali.
Akizungumza na Tanzania Daima Jumapili kwa njia ya simu, Nyambabe alisema chama hicho kinaendelea kumuunga mkono Kafulila katika hoja hiyo ambayo ilisababisha hadi kutishiwa maisha na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Fredrick Werema.
Nyambabe alisema kuwa hoja ya Escrow pamoja na suala la vitisho kwa Kafulila, vimepangwa kuwa ajenda kubwa katika mikutano ya NCCR-Mageuzi.
Soma pia: Uzi maalum wenye matukio yote yaliyojiri kwenye sakata la ufisadi wa ESCROW
"Ni jukumu letu kwa viongozi makini na wenye kulitakia mema taifa letu kuwa wakweli na kuwapa taarifa stahiki wananchi na sio kuwapotosha," alisema.
Kashfa hiyo iliibuliwa bungeni na Kafulila, akiwataja vigogo sita wa serikali wakiwemo mawaziri kadhaa aliodai wamehusika na ufisadi wa fedha hizo zilizokuwa zimewekwa katika akaunti ya Escrow iliyokuwa katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Kafulila aliwataja Waziri Muhongo, naibu wake Eliakim Maswi, Waziri wa Fedha Saada Mkuya, Gavana wa BoT, Prof. Beno Ndullu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema na Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, Mhandisi Felchesmi Mramba.
Licha ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuchunguza suala hilo, Kafulila na wadau wengine wanataka iundwe Kamati Teule ya Bunge kwa kuwa suala hilo linagusa mamlaka kubwa katika dola.
Akaunti hiyo ilifunguliwa mwaka 2004 kutokana na mgogoro wa kibiashara kati ya IPTL na Tanesco ambapo shirika hilo lilipeleka shauri hilo kulalamikia gharama kubwa wanazotozwa na IPTL.
PAP inadai kuinunua IPTL kutoka kwa Merchar iliyokuwa ikimiliki asilimia 70 ya hisa na VIP iliyokuwa na umiliki wa asilimia 30.
Chanzo: Tanzania Daima