wahafidhina wapo chadema
lione sjui umelogwa?mwenzio kaandika vitu vya maana vilivyosheheni ujumbe wa maana kwa watanzania we unaandika upuuz ukifkiri unaandika kwenye kuta za choo kama kwaida yako.
wahafidhina wapo chadema
unatisha!!!!!!!Wakati dogo anatema madini MWIGULU alikuwa anatafuna kucha kama mtoto wa ke anashawishiwa avue chupi.
Source : TBC1
Subiri usikie na upande wa pili halafu upime ndipo utakuwa na wakati wa kujua undai wa mambo.
Mimi nasubiri upande wa wakali wengine ndipo niamue wapo vichwa kama akina ngeleja,mwigulu,wasira,kingunge na wengine wengi hapo sasa nitaweza kupima.
Ongeza hapo na Lusinde,Kapiteni Komba na juma nkamia. Hivyo ndio vichwa " vyetu" ndani ya Chama " chetu"
Sent from my iPad using JamiiForums
we Mtanzania wa wapi bana? unahitaji upande wa pili useme nini kipya? Mimi ni muumini wa serikali 1, kama alivyoiacha Nyerere na Karume, lakini sasa hivi hiyo haipo!! kwani sasa hivi Zanzibar ni nchi tofauti na muundo wa serikali kama ilivyokuwa mwanzo wa muungano,Je unataka kuniambia kwamba hawa wazanzibari watakubali kuondoa kipengere cha kuitambua Zanzibar kama nchi kutoka kwenye Katiba yao? ili turejee kwenye serikali mbili nchi moja?Mimi nasubiri upande wa wakali wengine ndipo niamue wapo vichwa kama akina ngeleja,mwigulu,wasira,kingunge na wengine wengi hapo sasa nitaweza kupima.
kwa kweli yuko vizuri kafulila alivyo panga hoja zake kwa mtu makini atakubaliana na mimi.
Tatizo misimamo mingi ya wajumbe la bunge la katiba wengi wanatumia akili za kuambiwa na wamesahau formula ndogo tu.Jana mjadala ulikuwa moto kweli bungeni, Ila dondoo zifuatazo ndizo nilizifurahia:
1. Kama wananchi 17000 hawakustahili kutoa maoni na msimamo wa kuhitaji serikali tatu-Ni vipi Wajumbe 600 walioko dodoma kutunga Katiba kwa niaba ya watu mil 44???
2. Kama unasema watu waliotoa maoni walikuwa wachache wakati wa tume ya warioba kwa kuangalia kipengele cha Mawaziri kutokuwa Wabunge na aina ya Muungano tunaouhitaji-ni vipi watu 1000 waliotoa maoni HATUHITAJI USHOGA tanzania? inamaana nayo tuyakatae na tuseme no tunataka ushoga coz waliotoa maoni ni wachache???
Biasness iko kwa pande zote mbili ie. wenye kutaka serikali mbili na pia wenye kutaka serikali 3... Ukweli ni kuwa serikali tatu ni kuvunja muungano, Aidha serikali mbili itakuwa inatoa upendeleo kwa upande mmoja wa muungano! ... Dawa hapa ni Serikali moja ya majimbo!... Zanzibar kuwa state inayojitegemea yenye sharia zake same kwa Mashariki, magharibi, kusini, Kaskazini, Kati, Nyanda za juu kusini, Kanda ya Ziwa... Hoja hii ya majimbo kwasasa yanamashiko kwani zamani walikuwa wanaogopa eti kuna majimbo hayatakuwa na rasilimali kama kanda ya kati! Sasa hivi kanda ya kati ina Uranium, Zabibu na Dhahabu nyingi, Kanda ya Magharibi wanakila kitu including dry ports, Kanda ya kaskazini iko poa kwenye sekta ya utalii na madini, kusini zamani walikuwa masikini lakini baada ya ugunduzi wa gas wako on top of the list! Serikali ya majimbo ndio suluhu la kuendelea kuwa wamoja na hata uendeshaji wake utakuwa rahisi...
David Kafulila namuona akiwa katika kiwango cha juu cha weledi.Synovate ni kampuni ya tano dunianimkwa ukubwa,inajihusisha na kufanyamtafiti.Wanatumia sampuli ya watafitiwa 2700 kuwakilisha maoni ya watu mil300.
Walitoa matokeo kuwa Kikwete atashinda kwa 86% mwaka 2005 na tofauti haikuwa kubwa.Kikwete alishinda kwa zaidi ya asilimia 80.Kafulila umetisha.
CCM wanadai eti sampuli ya watanzania 17000 waliotoa maoni kuhusu muundo wa muungano,na kupendekeza serikali tatu eti ni wachache.Eti hawatoshi kuwakilisha maoni yawatu mil 44.
Kafulila anahoji,kama watu 17000 hawatoshi kuwakilsha watu mil 44 Wabunge mia 600 wa bunge la katiba wanapata uhalali wapi wa kuwawakilisha watanzania mil 44?
Kati ya watanzania 17000 na wabunge 600 wawapi wachache? Kafulila umekomaa kwa ujenzi wa hoja.CCM wanasema kuwa Nyerere angekuwepo asingekubali pendekezo la serikali tatu maana msimamo wakeulikuwa seeikali mbili kuelekea moja.
Kafulila anajibu hoja kuwa Nyerere hakuwa Mtume,alikuwa anakosea na baadae kujikosoa na hata kukubali kukosolewa.
Nyerere alivikataa na kuvifuta vyama vingi vya siasa mwaka 1965,lkn ilipofika mwaka 1992 kutokana na udhaifu wa ccm,kulihitajika vyama vingi,licha ya watanzania kukataa vyama vingi kwa madai kuwa vitaleta vita lkn Nyerere alishinikiza wenzake kuukubali mfumo wa vyama vingi ambao mwaka 1965,aliukataa.Kafulila you have made my day.
CCM wanadai kuwa serikali ya muungano itakuwa haina vyanzo vya uhakika vya mapato na hivyo utakuwa tegemezi kwa serikali washirika.
Kafulila anadai kuwa tume ya warioba haikuwa sahihi kwa asilimia mia moja,ndio maana ya uwepo wa Bunge ya katiba kwa ajili ya kuiboresha rasimu kwa kuonyesha vyanzo mbadala.
Kuwa vyanzo vya ushuru wa forodha na Mapato ya Bandari yanafikia kiasi cha Trilioni 3.7 na gharama za uendeshaji wa serikali ndogo ya Muungano inakadiriwa kuwa Trioni 3.1 tu hivyo kwa chanzo hicho kimoja tu ,kinatosha kuifanya serikali ya muungano bila kutegemea michango ya serikali washirika.
Asante Kafulila kwa kutufungua macho watanzania.
CCM wanadai kuwa serikali tatu ni kuvunja muungano,Kafulila anadai kuwa hii ni Propaganda yenye lengo la kuwatia hofu watanzania kama watanzania walivyoogopeshwa vyama vingi vya siasa mwaka 1992 kuwa vitaleta vita.
Lkn ki msingi vyama vingi vimeimarisha demokrasia kama ambavyo serikali tatu itaimarisha kuaminiana kati ya Tanganyika na Zanzibar.Kafulila weeeeeeeeeeeeeee!
CCM wanadai kuwa serikali tatu zitaibua hisia kubwa kwa watanzania bara kuwa Tanganyika inachangia sana,hivyo kuukataa muungano mpaka wachangie kwa usawa.
Kafulila anasema waache unafiki,kwani kwa mfumo wa sasa wa serikali mbili nani anachangia kikubwa kati ya Tanganyika na Zanzibar? Kimsingi Tanganyika inachangia kikubwa kuliko Zanzibar na watanganyika wapo kimya,hivyo hakutakuwa na tofauti yoyote ndani ya serikali tatu na mfumo wa sasa.
Vijana tunapaswa kuwaiga vijana wenzetu wanaofanya vizuri katika mijadala ya kitaifa,tupende sana kujisomea japo magazeti na vitabu ili kujiongezea maarifa.
Natamani nimwone Zitto Kabwe akiwasilisha maoni ya wachache,Natamani nimwone James Mbatia akiwasilisha maoni ya wachache.
Natamani nimsikie Prof Lipumba akiwasilisha maoni ya wachache.Namtamani John Mnyika awasilishe maoni ya wachache,Natamani kumwona Julius Mtatiro akiwasilisha maoni ya wachache.
Natamani kumwona Ismali Jussa Ladhu akiwasilisha maoni ya wachache.
Muungano unaotokana na mawazo ya wananchi ndio muungano imara kuliko muungano unaotokana na matakwa ya watawala.
Mungu ibariki Tanzania.