Wonderful
JF-Expert Member
- Apr 8, 2015
- 7,347
- 5,986
Mshambuliaji Obrey Chirwa wa Yanga, yuko huru kucheza baada ya mechi kadi yake nyekundu kufutwa.
Kamati ya Saa 72 ya TFF iliyokaa, imepitisha uamuzi huo leo.
Chirwa alilambwa kadi nyekundu baada ya kupewa kadi ya pili ya njano katika mechi ya Yanga dhidi ya Ruvu Shooting.
Kadi yake ya kwanza ya njano ilikuwa ni baada ya yeye kufunga bao kwa kichwa, lakini mwamuzi akasema alikuwa ameshika na kumpa kadi ya njano.
Dakika chache baadaye aliupiga mpira chini na kulambwa kadi ya pili ya njano iliyozaa nyekundu.
Sasa Yanga wako huru kumtumia katika mechi yao dhidi ya Mtibwa Sugar mjini Morogoro, kesho.