Kada wa Chadema

mpiga domo

JF-Expert Member
Apr 30, 2013
852
1,505
Habari za Jumapili wakuu,

Kuna mwenzetu humu ndani anajiita Kada wa Chadema. Lakini kwa uchunguzi mdogo nilioufanya ni kwamba anatumia jina la Kada wa Chadema ila hana mahusiano yoyote ya kiitikadi na Chadema.

Ukitaka kulijua hili angalia post zake zote za nyuma ndo utagundua anatumia jina lake kama tool ya kujenga credibility kwa wataokurupuka kusoma mada zake. Na mara zote hoja zake zote zimejikita kwenye kuichafua Chadema.

Me naona ni kijana wa mrengo uleeeee, ambaye ana'abuse jina la chama kingine katika kutimiza malengo yake ya propaganda.

Ni sahihi ku'post kila unachoona wewe kina maana lakini usitumie jina la taasisi au mtu mwingine kutimiza malengo yako. Ni sawa sawa humu ndani mtu atumie jina Pope halafu awe ana post mada za uasherati humu ndani.

Naombe tuungane katika kuufichua unafiki huu kwani kutaleta content and true meaning katika post zinazowekwa humu ndani.
 
Yule ni kada wa ccm tena mfitini haswa..

Aliwahi kuja na mabandiko ya kuchafua wenzake kama kina Membe na wengine kibao!
 
ukiangalia story ya makada wa chadema wengi ni wale waliokuwa upande wa pili kama unataka kubisha tukuletee post za wema akiikandia chadema lakini sasa hivi ni kada wenu.Huyo ni kada msianze kumkana mwishowe mtamkana hadi lowasa
 
chadema nayo haitaki kukosolewa? akiikosoa chadema kosa lipo wapi? na umethibitishaje kuwa sio mwanachama wa chadema??
 
"Kada wa Chadema " njoo na kadi yako tumalize mjadala!
 
Kada Wa chadema, Msemaji ukweli, Lizaboni, Nibozali n.k. zote ni ID za mtu mmoja ambaye ni Lizaboni. Count me
 
Mpiga domo anatoka Chama Kimoja na Mlimbwende na Miss Tanzania wa Zamani mwny Kashfa kadhaa za Matumizi ya Mihadarati na ukahaba
 
Back
Top Bottom