Kada wa CHADEMA amwagiwa tindikali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kada wa CHADEMA amwagiwa tindikali

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by abdulahsaf, Apr 1, 2012.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  Apr 1, 2012
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  [TABLE]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE]
  [TR]
  [TD]


  na Mwandishi wetu


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #ffffff"][​IMG] [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][TABLE]
  [TR]
  [TD]Kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Zabron Yusuf, amemwagiwa tindikali na watu wanaoaminika kutumwa na chama kimoja cha siasa juzi usiku wakati akijaribu kumwokoa mwanachama mwenzake aliyekuwa ametekwa na watu hao.
  Katika tukio hilo ambalo viongozi wa CHADEMA wamelifungulia jalada la malalamiko kituo cha polisi Usa River, Yusuf amelazwa katika Hospitali ya Nkoaranga, huku ikielezwa kuwa hali yake sio njema.
  Akisimulia tukio hilo, Yusuf (28) alisema kuwa walipewa taarifa na Wasamaria wema kuwa kuna kijana mwenzao wa CHADEMA alikuwa ametekwa na watu waliodai kuwa ni wafuasi wa CCM na alikuwa akipigwa na kulazimishwa kushusha bendera za chama hicho na mabango ya mgombea wake, Joshua Nassari, ambayo yako sehemu mbalimbali hapo Leganga.
  “Tulipopewa taarifa hizo tukaondoka mimi na wenzangu kwenda kuangalia kuna kitu gani, tulipofika maeneo hayo tukawakuta wamefika mbele wanakaribia Rotterdam pale darajani, basi tukazidi kuwafuata, bahati nzuri pia wakaongezeka wenzetu wengine kina Mrema (John, Kamanda wa Operesheni Uchaguzi ).
  Alisema walifanikiwa kuwashika na kuwazingira watu hao ambao walikuwa sita na kuwaamuru wakae chini, lakini kukazuka vurumai kubwa kabla ya kuwadhibiti.
  “Walipoona tumewazidi nguvu wakapiga risasi, wenzangu wakakimbia lakini walipoona mimi bado nakabiliana nao hasa nimemshika na kumweka chini yule mmoja, wakarudi na ghafla wakanimwagia tindikali nyingi machoni na mwilini kama unavyoona,” alisema Yusuf.”
  Aliongeza kuwa watu hao walifanikiwa kukimbia hadi kituo cha polisi Usa River, huku wawili kati yao wakaingia kule nyuma kwenye matenti ya FFU, na mwingine kaunta ya polisi.
  “Cha ajabu ni kwamba tulipofika pale polisi walikataa kuwatoa wale walioingia kule kwenye matenti, hata yule aliyekimbilia kaunta bahati nzuri tu kuwa tulimkuta bado hawajamuingiza ndani, lakini walikataa katakata kuwa huyo hahusiki na tukio letu, kisha wakamwambia apite aende uani…tukawaambia sisi tunamjua ni yeye, basi nikiwa pale macho yakawa taaban na nikaishiwa nguvu nikaanguka ndipo wakanileta hapa hospitalini,” alisema Yusuf.
  Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha hakupatikana kuelezea tukio hili, naye mkurugenzi wa operesheni katika uchaguzi huo, Isaya Mngulu, alipotafutwa, simu yake ilipokelewa na msaidizi wake ambaye alisema kuwa bosi wake alikuwa kwenye kikao Chuo cha Polisi (CCP) Moshi.
  Mganga Mkuu wa Hospitali ya Nkoaranga, Julius Mollel, hakuweza kupatikana ofisini kwake kuthibitisha kimiminika alichomwagiwa Yusuf na wenzake.
  Mapema Julius alizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu ambapo alisema yuko ofisini lakini waandishi wa habari walipofika ofisini hapo hawakumkuta huku simu yake ikiwa haipatikani tena.
  Wiki mbili zilizopita watu wanaotajwa kuwa viongozi wa juu wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kilimanjaro, wanatuhumiwa kumteka na kumtesa mpaka kumharibu sehemu za siri, Mwenyekiti wa CHADEMA Tawi la Magadirisho.
  Polisi licha ya kupewa taarifa hizi na kutajwa kwa majina ya wanaodaiwa kuhusika na tukio hilo, hawajachukua hatua zozote, hali ambayo imelalamikiwa vikali na CHADEMA.
  Mbali na tukio hilo la kumwagiwa tindikali, mchana watu kadhaa wakiwa kwenye magari yaliyokuwa kwenye msafara wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ukitoka mkutanoni eneo la Kikatiti, walishuka na kuwavamia waendesha pikipiki mashabiki wa CHADEMA eneo la Leganga, ambapo kuliibuka vurumai kubwa, ambapo vijana hao walimteka mtu mmoja ambaye mpaka sasa haijulikani alikopelekwa.
  Baadhi ya watu waliohojiwa na Tanzania Daima, wamesema iwapo vyombo vya dola havitasimama imara na kuchukua hatua bila kubagua, matukio mabaya yakiwemo ya umwagaji damu yanaweza kutokea katika saa chache zilizobaki kabla ya uchaguzi wa kesho.


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. H

  HOJA YANGU Member

  #2
  Apr 1, 2012
  Joined: Jul 31, 2011
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Da! nampa pole huyo ndugu yetu. Mungu atamwinua na kumponya.
   
 3. l

  local king12 New Member

  #3
  Apr 1, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hakika hao jamaa wa ccm mwaka huu watakunya karanga
   
 4. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #4
  Apr 1, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Aisee!
   
 5. M

  Mhamashiru Member

  #5
  Apr 1, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Watawadhuru wangapi jamani!!! Cha ajabu ktk matukio yote(mwanza na Arumeru)sijasikia Kauli ya Mlinda usalama mkuu aigip!!!
   
 6. B

  Bweri Member

  #6
  Apr 1, 2012
  Joined: Aug 26, 2011
  Messages: 79
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  igp atasema nn wakati cheo cha zawadi,unataka anyang,anywe
   
 7. chumvichumvi

  chumvichumvi JF-Expert Member

  #7
  Apr 1, 2012
  Joined: May 6, 2010
  Messages: 1,050
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  yupo arusha anahakikisha ushindi wa hao mashetani
   
 8. chumvichumvi

  chumvichumvi JF-Expert Member

  #8
  Apr 1, 2012
  Joined: May 6, 2010
  Messages: 1,050
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  nani anaharibu amani ya nchi sasa nani anayetaka tufanye tofauti 2napenda amani ila hali ikiendeleea ivi serious 2015 inatakuwa ni mbali sana
   
 9. K

  Konya JF-Expert Member

  #9
  Apr 1, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 920
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  wanaohusika na uhalifu wa namna hii wengi wanatumwa na wanaowatuma wanajulikana na wengi wao ni vigogo thats why jeshi la polise hawana muda kufuatilia haya na wako tayari kuwalinda so tusitegemee jipya
   
Loading...