KADA wa CCM atoboa siri CCM mambo magumu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

KADA wa CCM atoboa siri CCM mambo magumu

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Lu-ma-ga, Oct 12, 2010.

 1. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #1
  Oct 12, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,840
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  Jana jioni nilibahatika kukutana na Rafiki yangu wa karibu ambaye ni kada wa siku nyingi wa CCM na pia ni askari jeshi mstaafu aliyepigana vita vya kagera akiwa Brigedi ya Mayunga a.k.a mti mkavu.
  Alikuwepo nyumbani kwangu tulipata chakula cha usiku a.k.a supper, wakati tunaangalia luninga kusikiliza taarifa ya habari za kitaifa alimuona kada mwenzake Kinana akimwaga sera za UMWAGAJI DAMU.Rafiki yangu huyu alikasilika sana akasema" Hivi CCM ndiyo imeishiwa hivi? hii si CCM ninayoijua mimi, sasa naanza kuamini kuwa mwaka huu hatushindi, labda tuibe sana kura, maana hata mitaani nimejaribu kupitia vijiweni nijaribu kuweka mada ya kutetea ccm napata watu 2 kati ya watu 10, yaanni rafiki yangu CCM hatuna asilimia 30 ya ushindi kama mambo yatakwenda sawa.Ila hatuko tayari kushindwa"
  Rafiki yangu huyo anapinga sana kitendo cha kutumia mtaji wa kumwaga damu, anakumbuka walivyoteseka kuikomboa Kagera toka mikono ya Nduli Idd Amin Dada, anasema anawaonea huruma watanzania, ila anapinga kuwa "sijawahi kumsikia SLAA akiongelea kumwaga damu ila sisi inaonekana hoja za kuwashawishi waajiri wetu(wapiga kura ) hatuna dalili ya kuanguka iko wazi sijui wenzangu CCM kama wameiona"

  Hayo ndiyo tuliyoongea na huyo rafiki yangu kada wa CCM,

  Fundisho:
  Kutokana na mazungumzo yetu nilichojifunza ni kwamba, chadema wanayo nafasi ya kuchukua dola wantakiwa waweke mikakati ya kulinda kura hasa tukizingatia statement ya colleague wangu ya kwamba"sasa naanza kuamini kuwa mwaka huu hatushindi, labda tuibe sana kura,"
   
 2. m

  masaiti Senior Member

  #2
  Oct 12, 2010
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 197
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Walianza na Chadema chama cha ukabila, wakashindwa, ooh Dr Slaa katumwa na kanisa Katoliki, wakashindwa, ooh ndoa yake, pia wakashindwa, sasa wanatishia kuwa amesema damu itamwagika, ambalo si la kweli lakini nalo pia watashindwa. Mungu akiwa upande wetu..........
   
 3. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #3
  Oct 12, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  ni kweli hata ccm wanajua mwenyekiti aliwaaaambia wanahali mbaya saaana! wajipange vizuri.
   
 4. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #4
  Oct 12, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Ni kweli wan a Hali mbaya san a ...nod maana iringa alipomaliza mkutano alikesha usiku kucha kuweka kikao na macadam wa chama....anajua kinachokuja
   
 5. W

  We know next JF-Expert Member

  #5
  Oct 12, 2010
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 664
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Jamani si wakubali tu yaishe? Hawa watu kwani hawajajifunza kweli toka kwa majirani zetu? mbona Tanzania tumezungukwa na nchi karibu zote ambazo wamepita ktk matatizo haya na tumeona matokeo? Mimi kwakweli si waelewi kabisa hawa watu. Sasa utawala Bora unaopigiwa kelele siku zote ndo uko wapi? I am fade up!
   
 6. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #6
  Oct 12, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,823
  Likes Received: 10,120
  Trophy Points: 280
  Wahenga walisema jamani...Ukiona Paka kakubali kulala chali...ujue .....
   
 7. Sir R

  Sir R JF-Expert Member

  #7
  Oct 12, 2010
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 2,177
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Ni wengi makada wa CCM wanaokiri hivyo kuwa hali ya CCM ni mbaya.
   
 8. J

  Jafar JF-Expert Member

  #8
  Oct 12, 2010
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 1,138
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Ili kukamilisha hayo hakikisha tarehe 31 October unachagua CHADEMA.

  Tusibwete CCM wana roho ya paka.
   
 9. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #9
  Oct 12, 2010
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Kakobe na waumini wake wanauzoefu wa kulinda na kukesha, vyama vya upinzani vyaweza wasiliana na kakobe wakapata mawakala waaminifu, wenye msimamo na uwezo wa kukesha na kutetea kile wanacholinda.
   
 10. Nyange

  Nyange JF-Expert Member

  #10
  Oct 12, 2010
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 2,180
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Leo nilikuwa kwenye usafiri wa dala dala Mwenge vs K/koo, kwenye radio ya Clauds, ikasoma habari ya Mgombea urai kupitia ccm amewahaidi wananchi wa nyasa kuwa akiingia madarakani, atawanunuliwa meli! Basi lote liliangua kicheko, huku baadhi wakisema huyu bwana upstair hapako sawa. Wakahoji , kwa sasa nani anamzui asinunue si ndiye Rais kwa sasa? HAKUNA HATA ALIYE TETEA HIYO AHADI.!
   
 11. B

  ByaseL JF-Expert Member

  #11
  Oct 12, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 2,223
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Pamoja na hayo mimi huwa sipendi kuchukulia observation au maoni ya mtu mmoja kama ndio hali halisi. Ni kweli mwaka huu CCM haikutegemea mambo yawe magumu lakini ili la kushindwa na Chadema bado silikubali moja kwa moja hata kama napenda upinzani hasa Chadema washinde. Huko vijijini tukubali tusikubali CCM bado ina nguvu sana kutokana na kuwa na mtandao wa utawala, umasikini mkubwa na elimu duni ya urahia. Tusisahau kama bado watu hapa mjini wanauza shahada za kupiga kura kwa elfu tano sembuse vijijini wakipewa khanga na kofia!! Maoni ya mwanajeshi tena mstaafu kwa mawazo yangu yanabaki kuwa mawazo tu.
   
 12. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #12
  Oct 12, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160

  Kwa sasa JK ametoa ahadi hata zingine hakumbuki tena!! Ameishiwa msikini, hajua afanye nini, mara Dubai ya Africa, Amsterdam ya Africa ,ma-california ya africa, mauwanja ya ndege, sijui nini, sjui nini, bado ahajasoma alama za nyakati kuwa ahadi sasa watu wamejua ni mchezo wa kuigiza!!!

  Kazi ni moja tu, 31/10/2010, dawa ni moja tu VOTE CCM OUT KWA KUCHAGUA CHADEMA!!!
   
 13. C

  CLAY KITUMBOY Senior Member

  #13
  Oct 12, 2010
  Joined: Sep 8, 2009
  Messages: 111
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Cha muhimu sio kuiba kura, wala mpiga kura,bali mtangaza matokeo ya kura.
   
 14. Mo-TOWN

  Mo-TOWN JF-Expert Member

  #14
  Oct 12, 2010
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,626
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 160
  Kazi kweli kweli! Eti wanataka kuingia Ikulu kwa kukanyaga maiti. Wanajukwaa kwanza niwaafahamishe mfahamu kuwa kile ambacho mtu anapenda sana kusema juu ya wenzake ndicho hasa anachopenda kufanya yeye. Hivi vyama vinavyotaka kushika dola vinaweze kuwaga damu kivipi wakati dola na machinery zote kamdamizi ziko na chama tawala? Haingii akilini hata kidogo. Hata kama mtu hajaenda shule anafahamu fika kuwa damu itaweza kumwagika tu kama chama kilichoko madarakani kinakuwa hakiko tayari kuondoka. Hii ni duniani kote. Na hii utokea kama kunakuwa na ubabaishaji kama kutumia nguvu kuwatisha wapigakura kama tunavyoona sasa.

  Swali kama Chama/Serikali iliyoko madarakani hawana hofu ya kushindwa kwanini waanze kuhusisha jeshi la Ulinzi (Labda jeshi la polisi limeshindwa kazi). Kwa nini kutumia taasisi kutoa maoni ya upigaji kura za Urais. Nashauri tu vyombo husika NEC/Returning Officers etc kufanya kazi yao ipasavyo, kura zihesabiwe katika vituo vya kupiga kura na matokea yabandikwe/kutangazwa vituoni. Ni Uwazi tu. Vilevile tunazingumzia swala la amani Tanzania napenda kuwafahamisha Jeshi la Ulinzi kuwa kuna maeneo mengi tu ambayo tunaishi na hatuma amani kutokana na Ujambazi/Uporaji/na dhuruma mbalimbali, Ombi langu kwenu ni kuwa muwe proactive kama manavyojitokeza sasa wakati wa uchaguzi.
   
 15. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #15
  Oct 12, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,373
  Likes Received: 3,134
  Trophy Points: 280
  Hatuko tayari kuendelkea kubabaishwa na ccm tumeshaichoka
   
 16. Mtende

  Mtende JF-Expert Member

  #16
  Oct 12, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 4,072
  Likes Received: 338
  Trophy Points: 180
  na cha muhimu pia ni ulinzi wa kura zisije kuchakachuliwa maana huku tunapoelekea sio pazuri kabisa
   
 17. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #17
  Oct 12, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Hili liko wazi kweli kweli Moja Wanamtandao walijisifu sana walipo shinda na JK akawa Rais na hawkujua wanaenda IKULU kufanya nini? Mwl.Nyerere "alisha wahi sema IKULU ni Mahali patakatifu Sio mahali pa kufanya Pango la Ulanguzi hata kidogo"

  Sasa Mlitegemea CCM ya wanamtandao itakuwa nzuri kweli? hebu angalieni kwanza wale watu maarufu wa CCM hawamo tena wamebakia wao tu na hii nikujifanya wao wanajua sana kuliongoza hili taifa na limewashinda na midomo yao ndio imewafikisha hapo pabaya kwa kukashifu sana ati mbona wao wakati wao walishindwa kufanya iweje leo ndio wanajifanya wanajua kurekebishaaa? Na matokeo yake sasa wao wanamtandao ndio wanajiahalibia kabisaaaaaaao

  Amini nawambieni UVCCM kama kweli nanyi mtafauata mienendo ya hao wana mtandao chini ya uongozi wa EL na mkarogwa tuu kukubaliana nae kweli 2015 UVCCM hamtokuwa na chenu amkeni sasa mkumbuke ile Miiko ya Uongozi ambayo Mwl.Nyerere aliitetea sana kwa maslahi ya nchi hii leo hawa wanamtandao wanawaharibieni Future yenu nini UVCCM mi naamini ndani yenu kwa muda huu uliobaki mwaweza kukigeuza chama CCM kama mtasimama na kuongea Lugha mmoja na Kauri ya pamoja mtakirudisha chama CCM uaminifu kwa watanzania wengi tu huko mijini na vijijini.

  Kama alivyo sema mwana JF mmoja"MO-Town" haiingi akilini Chama tawala kimeshika vyombo vyote vya dola na kina tuma watu wa propaganda kusema ukichagua upinzani kutavurukika amani sasa hili siwazi dhahili kuwa CCM wakishindwa waondio wataingia msituni sasa na kuanzisha dhahama nchini ??? Simwelewi Kinana kama manager Campaign wa CCM tena chama tawala kuruhusu upuuuzi huu wa hio propaganda kutolewa ni ujinga wa ajabu sana hivi umewaona watanzania ni mazezeta sana hawajaenda shule au? na ndio maana mwasema elimu haiwezi ikawa bure nini mkidhani ndio mtawafumba macho na masikio na akili wasijue lipi ni la haki na lipi sio la haki, Jamni tuache hizi siasa zisizo kuwa na kichwa wala miguuu a.k.a Majitaka politics, tumwage sera za kutupa maendeleo hapa

   
 18. N

  Nsesi JF-Expert Member

  #18
  Oct 12, 2010
  Joined: Nov 20, 2008
  Messages: 374
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nimefanikiwa kuzunguka na wagombea watatu, JK, Dr Slaa na Prof. Lipumba kwenye baadhi ya mikoa, ninachoweza kusema tu kwa ufupi ni kwamba iwapo ile mikusanyiko, maoni na hasira za wananchi ndizo zitakazowaongoza kwenye sanduku la kura okt 31, na uchaguzi ukawa ni huru na haki basi CCM kurudi madarakani ni ndoto.

  Kwa kipimo hicho cha mikusanyiko, maoni na hasira za watu dhidi ya CCM, mikoa ya Iringa, Mbeya, Rukwa na Katavi ni ya Dr Slaa. Rukwa ambao awali waliku CCM damdam, leo hii hawataki hata kuisikia, kwa mfano katika mkutano wa Sumbawanga mjini umati uliohudhuria unaelezwa na wenyeji haujawahi onekana tangu nchi hii ipate uhuru, ulikuwa mara tatu zaidi ya ule wa JK.

  Katika kukabiliana na nguvu ya Dr Slaa, CCM walikuwa wakiandaa vijana wa baiskeli, pikipiki na taxi, kwa kuwakodi, waliwapa fulana, kofia, scaff na bendera ili wawe wanazungka mjini muda wote siku mgombea huyo wa CHADEMA anapokuwa kwenye mji husika, ilifanyika Namanyere na Mpanda ndio ilikuwa balaa.

  Suala la kumwaga damu sijamsikia mgombea yeyote kati ya Dr Slaa na Prof. Lipumba, ni kauli ambayo amekuwa akiitumia JK kuwaghilibu wananchi kwa kuwahusisha wapinzania wake na umwagaji damu.

  CCM inapaswa kufahamu kuwa Watanzania wamebadilika sana, na safari hii wanachagua watu na sio chama
   
 19. JOYCE PAUL

  JOYCE PAUL JF-Expert Member

  #19
  Oct 12, 2010
  Joined: Jan 8, 2010
  Messages: 1,007
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Asa ndo tujue meja wa jeshi alikuja kwako?uhakika tutaupataje kama alizungumza hayo uyasemayo??
   
 20. Tonge

  Tonge JF-Expert Member

  #20
  Oct 12, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 696
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mwka huuu kweli kabisa watakao mwaga damu ni CCM wamejuaje kuwa kuna kumwaga damu kama hawajui jinsi ya kumwaga damu? Wamejiandaa kuchukua nchi kimaguvu ndio maana majeshi yamejipanga na kutoa vitisho.Sisi tunasema HATUDANGANYIKII.
   
Loading...