kilimasera
JF-Expert Member
- Dec 2, 2009
- 3,068
- 268
Ishu hiyo nimeisoma nikaona ni nzito sana basi kama mtu utaandika wosia ni muhimu pia kuandika kwamba ukifa uzikwe wapi na kwa dini ya dhehebu gani kwasababu hili ni tukio lapili nadhani kama unakumbuka miezi michache iliyopita kulikuwa na sakata kama hili lililosababisha kaka wa mke kufariki baada ya kudondoka pale mahakama ya kisutu!Nakubaliana na wazo la kujipanga kabla ya kufa,
ili kupunguza mifarakano baina ya ndugu utakawo waacha
Lakini mimi binafsi kila nikitaka kuandika wosia huwa naogopa sana
nahisi kama najitabiria kifo mapema ingawa sijui nitakufa lini.
Lakini kwa kesi hii, sidhani kama watoto wana haki ya kuuzika mwili kama wanavyotaka wao
kwani marehemu hadi anakufa inaonekana alikuwa katika dini yake mpya.
maane nakuunga mkono 100%hoja yako imepita man!Ndugu zanguni wosia ni muhimu hasa pale ambapo umefanya maamuzi makubwa kama haya ya kubadili dini. Hata kwa wale ambao wameoa mke mbali na mila na taratibu za kabila lake ni lazima afafanue wazi azikwe wapi maana imetokea mara nyingi kuwa ndugu wanataka ndugu yao azikwe kijijini kwao huku mke akitakwa azikikwe manispaa wanazoishi. Hii inaleta mzozo na kutokuelewana.
Kwa upande wa mali na pesa au mafao tunayoacha ndiyo kasheshe kabisa. Hebu tuamke kabisa na kuachana na kasumba kuwa ukiandika wosia eti unakaribisha kifo. Mbona wenzetu wazungu wanaandika wosia na ku-reviw kila jambo jipya au kuiongezeka/kupungua kwa rasilimali zake kwani wameshakufa? Wanaishi so many years na wosia copies kibao na ndipo ile latest ndiyo inatumika katika utaratibu wa urithi. Tuzinduke sasa!! Anza wewe!! Washauri wengine!!!
hivi ile ya kisutu ni upande gani ulishinda maana nilisikia tu kuwa kaka wa marehemu naye kafa ghafla.Ishu hiyo nimeisoma nikaona ni nzito sana basi kama mtu utaandika wosia ni muhimu pia kuandika kwamba ukifa uzikwe wapi na kwa dini ya dhehebu gani kwasababu hili ni tukio lapili nadhani kama unakumbuka miezi michache iliyopita kulikuwa na sakata kama hili lililosababisha kaka wa mke kufariki baada ya kudondoka pale mahakama ya kisutu!
MAHAKAMA ya Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam leo itatoa uamuzi ya sakata la kugombea kuzika mwili wa marehemu Salum Ngindo unaogombewa na mkewe anayetaka uzikwe Kiislamu huku watoto wa marehemu wakitaka azikwe kwa imani ya dini ya Kikristo.
Uamuzi huo ulitolewa jana na Hakimu Mkazi Afumwisye Kibona baada ya mke wa marehemu, Kudra Salum kufungua kesi ya madai dhidi ya watoto watano wa marehemu mumewe aliyefariki Februari 24, mwaka huu katika Hospitali ya Hindu Mandal wakidai kuuzika mwili wa baba yao Kikristo.
Watoto hao ni Matukuta Ngindo, Rose Ngindo, Nono Ngindo, Matukuta Ngindo na Gloria Ngindo.
Wakili wa upande wa Mashitaka, Mussa Roma alidai marehemu aliachana na mke wa kwanza ambaye ni mama wa watoto hao, miaka mingi iliyopita na kufunga ndoa ya Kiislamu na mke wa pili ambaye ni mlalamikaji.
Alidai awali marehemu alifahamika kwa jina la Gerard Ngindo, lakini baada ya kubadili dini alifahamika kwa jina la Salum Ngindo na kufunga ndoa ya Kiislamu na Kudra, Februari 10, 1994 na kuzaa naye watoto.
Alidai kuwa hata baada ya kuishi pamoja, baadaye marehemu aliugua na mlalamikaji ndiye aliyemuuguza kwa kipindi cha miaka sita na baada ya kufa, alitoa taarifa kwa ndugu na watoto wa marehemu kwa ajili ya msibani.
Alidai siku waliyopanga kwa ajili ya maziko, walikwenda katika Hospitali ya Hindu Mandal kuuchukua mwili, lakini baada ya kufika walikuta watoto hao wakiwa na kibali cha kuuchukua mwili kwa ajili ya kuuzika.
Naye Wakili wa utetezi Stephen Tonya alidai marehemu alitumia jina la Salum kama umaarufu, lakini alifahamika kwa jina la Gerard ambalo ni la Kikristo alilozaliwa nalo na hivyo ana wajibu wa kuzikwa Kikristo.
Wakili wa Mashitaka aliwasilisha cheti cha ndoa kati ya marehemu na mlalamikaji ambapo hakimu aliahirisha kesi hiyo hadi leo atakapotoa uamuzi wa kuzikwa kwa mwili huo.
Yaleyale..mijitu mingine sijui ni vp aisee.
Wosia ni kitu cha muhimu sana, kwani jamaa angekuwa kaandika wosia haya mambo yasingefika hapa yalipo. Tuache kuogopa kuandika wosia ili tutakapokufa tuwaache ndugu zetu waishi kwa amani.
Hapana wewe unasema tu ikitokea mungu akanipenda zaidi kuliko jamaa zangu basi mali zangu zitakuwa chini ya nani utazikwa wapi nk, huo ni mfano tu ila ukienda kwa wanasheria watakusaidia sanaHivi wosia huwa unaandikwa hata style ya maziko?
Nakubaliana na wazo la kujipanga kabla ya kufa,
ili kupunguza mifarakano baina ya ndugu utakawo waacha
Lakini mimi binafsi kila nikitaka kuandika wosia huwa naogopa sana
nahisi kama najitabiria kifo mapema ingawa sijui nitakufa lini.
Lakini kwa kesi hii, sidhani kama watoto wana haki ya kuuzika mwili kama wanavyotaka wao
kwani marehemu hadi anakufa inaonekana alikuwa katika dini yake mpya.
Nakubaliana na wazo la kujipanga kabla ya kufa,
ili kupunguza mifarakano baina ya ndugu utakawo waacha
Lakini mimi binafsi kila nikitaka kuandika wosia huwa naogopa sana
nahisi kama najitabiria kifo mapema ingawa sijui nitakufa lini.
Lakini kwa kesi hii, sidhani kama watoto wana haki ya kuuzika mwili kama wanavyotaka wao
kwani marehemu hadi anakufa inaonekana alikuwa katika dini yake mpya.
Kwa kawaida tunamzika mtu kwa imani aliyokuwa nayo kabla ya kufa..... to me azikwe kiislamu. Cheti cha ndoa hakitaji mtu azikwe vipi..sana sanakinataja dini tuuu...........Na hao watoto wanaodai baba yao azikwe kikristu.......walikuwa wapi kumshawishi baba yao arudi kwenye ukristu kabla ya kufa...??? NIKIONACHO NI KWAMBA HIZO PANDE MBILI INAONYESHA ZILIKUWA NA UGOMVI HATA KABLA HICHO KIFO........... tukio la kifo limetumika tu kukuza tofauti zao........MAHAKAMA ya Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam leo itatoa uamuzi ya sakata la kugombea kuzika mwili wa marehemu Salum Ngindo unaogombewa na mkewe anayetaka uzikwe Kiislamu huku watoto wa marehemu wakitaka azikwe kwa imani ya dini ya Kikristo.