Kabla ya kuangalia muvi ama series, pitia humu ujue inahusu nini

Chilojnr

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
302
1,306
CLICKBAIT

Series nyingine ya kiume hii hapa. Humu kuna jamaa anaitwa Brewer, siku ya birthday ya mama yake, kukatokea kaugomvi kadogo tu na mdogo ake, Pia, so dogo akasepa.

Kesho imefika, watu wanaangalia mtandaoni, wanamuona Brewer ameshika bango linalojieleza ana kosa la kumdhalilisha mwanamke, halafu na jingine kwa kufanya mauaji.

Pia hajui nini kinaendelea, anashtuka. Mbali na hilo bango, pia kuna bango jingine linasema hiyo video ikifikisha viewers milioni 5, basi jamaa anauawa, ili asiuawe, haitakiwi kufika 5M.

Hapo ndipo msala unapoanza. Polisi wanaingia kazini, wanachunguza na kuchunguza, muda unakwenda, viewers wanaongezeka hali inayowatisha ndugu wote akiwemo mkewe.

Unahisi nini? Viewers 5M walifika? Kama walifika, je, jamaa aliuawa? Na kama aliuawa, nani alimuua?

Okay! Tufanye hawakufika, nani alimteka? Lengo ni nini? Ukiiangalia, majibu ya maswali yote yapo humo.

Siku hizi hawataki kutuchosha, kuna episodes 8 tu mzigo wote.
Screenshot_20220109-201042_IMDb.jpg
 
SEE FOR ME

Humu kuna binti ni kipofu, kazi yake ni kulinda nyumba za watu. Yaani kama unataka kusafiri, unamuita, anakuja kukaa na nyumba mpaka unaporudi.

Sasa sometimes huwa anaiba. Inaibaje? Anapokuwa nyumbani kwako, anampigia simu rafiki kwa video call na kumwambia amuelekeze kuhusu nyumba hiyo. Kwa hiyo maelekezo ya jamaa huyo ndiyo macho yake.

Sasa alipoingia kwenye nyumba hii, aliingia mpaka kwenye chumba cha pombe, kulikuwa na pome za gharama, akataka kuondoka na moja, jamaa akamwambia ukiondoka nayo, siwezi kukusaidia. Mara simu ikakata.

Sasa bwana! Siku hiyohiyo akaamua kudownload App iitwayo See For Me. App hiyo ni kwa ajili ya kuwasaidia vipofu, yaani wewe unayeona kutumiwa kama macho yao.

Huko akakutana na msichana mmoja ambaye akaanza kumsaidia. Usiku wakati amelala. Wezi watatu wanaingia humo ndani, lengo lao ni kuiba pesa nyingi mno zilizokuwa kwenye safe.

Wakati wakiendelea na zoezi la kutoboa safe, mmoja anahisi humu ndani kuna mtu, anajaribu kumtafuta, ila hamuoni. Ni bonge moja la muvi, kuna mtifuano wa hatari sana.

Hii muvi ni kama Don’t Breath ila ukiiangalia kwa umakini utagundua ni kama ile ya Hush, sema mule kulikuwa na kiziwi, humu sasa kipofu.

Mwaka umeanza poa sana, naweza kusema nayo ipo upande wa muvi bora zitakazotoka mwaka huu. Kama hujaiona, itafute, hutojutia muda wako.
Screenshot_20220109-121417_IMDb.jpg
 
Kuna muvi huwa haziishi hamu. Sasa sikia! Humu kuna mzee alikuwa bilionea mkubwa, hakujawahi kutokea bilionea mkubwa kama yeye.

Nimependa namna mzee alivyokuwa anathamini sana pesa kuliko utu. Siku moja anapigiwa simu na kuambiwa mjukuu wake ametekwa na watekaji wanahitaji dola 17M kumuachia.

Mzee alipoambiwa atoe, akakataa, akasema ana wajukuu 14, akitoa hizo 17M kwa mjukuu mmoja, wajukuu wengine nao watatekwa, watekaji watahitaji pesa nyingi zaidi, hivyo akakaza.

Mama akaanza kuhangaika huku na kule, cha ajabu, mzee alikuwa ananunua michoro kwa bei kubwa, ila ishu ya mjukuu wake hakutaka kabisa kusikia.

Mwisho wa siku akakubali kutoa msaada, ila pesa atakazotoa, ni za mkopo, baadaye arudishiwe

Itafute hii. Ni muvi itakayokufundisha mambo mengi kuhusu umiliki wa pesa nyingi. Najua utaifurahia sana. Nilichopenda zaidi, ni jinsi mama alivyokuwa akipambana kwa ajili ya mtoto wake.
Screenshot_20220110-152159_Instagram.jpg
 
CLICKBAIT

Series nyingine ya kiume hii hapa. Humu kuna jamaa anaitwa Brewer, siku ya birthday ya mama yake, kukatokea kaugomvi kadogo tu na mdogo ake, Pia, so dogo akasepa.

Kesho imefika, watu wanaangalia mtandaoni, wanamuona Brewer ameshika bango linalojieleza ana kosa la kumdhalilisha mwanamke, halafu na jingine kwa kufanya mauaji.

Pia hajui nini kinaendelea, anashtuka. Mbali na hilo bango, pia kuna bango jingine linasema hiyo video ikifikisha viewers milioni 5, basi jamaa anauawa, ili asiuawe, haitakiwi kufika 5M.

Hapo ndipo msala unapoanza. Polisi wanaingia kazini, wanachunguza na kuchunguza, muda unakwenda, viewers wanaongezeka hali inayowatisha ndugu wote akiwemo mkewe.

Unahisi nini? Viewers 5M walifika? Kama walifika, je, jamaa aliuawa? Na kama aliuawa, nani alimuua?

Okay! Tufanye hawakufika, nani alimteka? Lengo ni nini? Ukiiangalia, majibu ya maswali yote yapo humo.

Siku hizi hawataki kutuchosha, kuna episodes 8 tu mzigo wote.View attachment 2075046
Endelea kutupa vitu mzee baba
 
Kuna muvi huwa haziishi hamu. Sasa sikia! Humu kuna mzee alikuwa bilionea mkubwa, hakujawahi kutokea bilionea mkubwa kama yeye.

Nimependa namna mzee alivyokuwa anathamini sana pesa kuliko utu. Siku moja anapigiwa simu na kuambiwa mjukuu wake ametekwa na watekaji wanahitaji dola 17M kumuachia.

Mzee alipoambiwa atoe, akakataa, akasema ana wajukuu 14, akitoa hizo 17M kwa mjukuu mmoja, wajukuu wengine nao watatekwa, watekaji watahitaji pesa nyingi zaidi, hivyo akakaza.

Mama akaanza kuhangaika huku na kule, cha ajabu, mzee alikuwa ananunua michoro kwa bei kubwa, ila ishu ya mjukuu wake hakutaka kabisa kusikia.

Mwisho wa siku akakubali kutoa msaada, ila pesa atakazotoa, ni za mkopo, baadaye arudishiwe

Itafute hii. Ni muvi itakayokufundisha mambo mengi kuhusu umiliki wa pesa nyingi. Najua utaifurahia sana. Nilichopenda zaidi, ni jinsi mama alivyokuwa akipambana kwa ajili ya mtoto wake.View attachment 2075951
Hii movie ni true story ya bilionea wa mwanzoni kabisa kuwekeza biashara ya mafuta uarabuni

na hicho kisa ni cha kweli kabisa
na hiyo MUSEUM ipo mpk leo nyumbani kwake ITALY huko imekuwa kivutio kikubwa cha utalii watu wanatoka pande zote za dunia kuangalia vitu vya kale

jamaa ukienda na kitu chochote cha kale akikielewa we sema bei yako unamuuzia
hvyo alikusanya makumbusho ya masalio ya tamaduni za pande zote duniani
 
CLICKBAIT

Series nyingine ya kiume hii hapa. Humu kuna jamaa anaitwa Brewer, siku ya birthday ya mama yake, kukatokea kaugomvi kadogo tu na mdogo ake, Pia, so dogo akasepa.

Kesho imefika, watu wanaangalia mtandaoni, wanamuona Brewer ameshika bango linalojieleza ana kosa la kumdhalilisha mwanamke, halafu na jingine kwa kufanya mauaji.

Pia hajui nini kinaendelea, anashtuka. Mbali na hilo bango, pia kuna bango jingine linasema hiyo video ikifikisha viewers milioni 5, basi jamaa anauawa, ili asiuawe, haitakiwi kufika 5M.

Hapo ndipo msala unapoanza. Polisi wanaingia kazini, wanachunguza na kuchunguza, muda unakwenda, viewers wanaongezeka hali inayowatisha ndugu wote akiwemo mkewe.

Unahisi nini? Viewers 5M walifika? Kama walifika, je, jamaa aliuawa? Na kama aliuawa, nani alimuua?

Okay! Tufanye hawakufika, nani alimteka? Lengo ni nini? Ukiiangalia, majibu ya maswali yote yapo humo.

Siku hizi hawataki kutuchosha, kuna episodes 8 tu mzigo wote.View attachment 2075046
Memories of the Midnight
 
Back
Top Bottom