Kabla sijampata,nilimdanganya mambo mengi,sasa kakuta mambo ni tofauti,anataka kuni..

Cruel mpole

JF-Expert Member
Jul 3, 2013
282
106
Habari zenu wana JF
Nimekuwa katika mahusiano na msichana mmoja,mrembo kwa takribani miezi mitatu sasa,katika mahusiano yetu,mimi peke ndo niliyekuwa najua makazi ya huyu binti,pasipo yeye kujua wapi ninaishi.Nimekuwa nikimdanganya mambo mengi sana mara tunapokutana nae.Nimekuwa nikijitutumua kama mtu mwenye maisha bora kumbe ni tofauti.

Sasa jana aling'ang'ania kuja kwangu nikajaribu kwa namna moja au nyingine,tufanye iwe siku nyingine apajue kwangu,lakini juhudi zikagonga mwamba,ikabidi nimpeleke kwangu,lakini moyoni najua kwamba naenda kuumbuka kwani yote niliyomwambia si kweli kwamba nimeshajijenga kimaisha,yaani having a complete house asset,frame za biashara n.k.For sure,my house is like a hole,no chairs,no tables no oven,lucking each and everything accomplishes a room.

Sasa jana kafikia kukaa kitandani,sebuleni kuna busati pekee,hakuna kitu kingine,I'm lucking even a buffer to play music and I have no the tv.

For sure my room is boring.You cant stay in it even for five minutes,its like a go-down.Leo asubuhi kaniambia yakwamba,ananipa siku tatu ninunue asset za nyumbani.

La si hivyo ataniacha na nisitegemee yeye kuja kwangu tena.Atakwenda kwa mwanaume anayejielewa ndo akae kwake,mm nitamsikia tu.

Sasa mimi niko njia panda,muda niliopewa ni mdogo,pesa niliyonayo hapa niyakukidhi mahitaji yangu yakila siku,sina bajeti yakununua vyombo na samani za ndani sasa.Nimeomba anivumilie,ndani yamiezi miwili nitakuwa nimefanya kile anachohitaji,lakini kanikazania kununua bidhaa hizi ndani yasiku tatu,kitu ambacho naona hakitawezekana.

Nina achwa jamani,naombeni ushauri bandugu,nisinyang'anywe tonge mdomoni.Kumbuka nampenda sana huyu binti,naye vilevile nahc ananipenda sana,ila kwa vile nilimdanganya sana,kanipa siku tatu tu,niwe nimetekeleza kile anachokitaka na mimi uwezo huo sina kwasasa.NIKAIBE?NIKAKOPE?AMA NIFANYE NINI ILI ASINITOKE.
 
mkuu huyo dada ulimpenda au ulimtamani? kwann umdanganye? kwanza una bahati coz ana mpango wa kuendelea na ww ingekuwa mwingine ndo byebye coz km uliweza kumdanganya kitu kidogo hvo je mengine?
 
Mkuu Pitisha mchango hapa jf

Gudi aidia! Hela nakusanya mimi jamani, tusimuache member mwezetu aachwe, ukitoa kidogo ulichonacho utapata zaidi mara kumi ya ulichokitoa! Afu apa hampotezi jamani, mtakikuta mbele ya haki!
...
Alietayari anipm nimtumie nö yangu aingize mijihela kwa tigo pesa, mpesa or kwa wale wailionje ya Tz watatumia bakileiz kufanikisha mchakato!
 
nenda I.T.V kajitangaze kuomba mchango kwa wananchi watakusaidia.

Mnaharibu uthamani wa jukwaa jaman acheni hzo ah!
 
Gudi aidia! Hela nakusanya mimi jamani, tusimuache member mwezetu aachwe, ukitoa kidogo ulichonacho utapata zaidi mara kumi ya ulichokitoa! Afu apa hampotezi jamani, mtakikuta mbele ya haki! ... Alietayari anipm nimtumie nö yangu aingize mijihela kwa tigo pesa, mpesa or kwa wale wailionje ya Tz watatumia bakileiz kufanikisha mchakato!
ha!ha!haaa naahid kumchangia sofa kochi seti moja mkuu! ili wifi asimwache kaka.
 
Njoo uoneshe kwangu kuwa ndo kwako, pale ulikuwa unamdanganya uone kama atakuacha, (material lady). Ila tuelewane kabisa utakuwa unanilipa kiasi gani kwa kila shoo utayopiga.
 
huo ukilaza mi siuwezi....ndo tatizo ya kuparamia visivyo levo zenu!
 
Leo asubuhi kaniambia yakwamba,ananipa siku tatu ninunue asset za nyumbani.
La si hivyo ataniacha na nisitegemee yeye kuja kwangu tena.Atakwenda kwa mwanaume anayejielewa ndo akae kwake,mm nitamsikia tu

mpenzi wako yupo sahihi sana! ni bora usalimu amri, usimtese huyo kiumbe.
 
Sema kweli,hii kitu inaandama mpaka sasa.Si story ya uongo,naombeni ushauri wenu,sio kunikandia.
 
Ndio uone athari ya uongo next time ukumbuke ukweli siku zote humuweka mtu huru..
Btw nipe namba yake nikusaidie jambo flani ili asikuponyoke.
 
Gudi aidia! Hela nakusanya mimi jamani, tusimuache member mwezetu aachwe, ukitoa kidogo ulichonacho utapata zaidi mara kumi ya ulichokitoa! Afu apa hampotezi jamani, mtakikuta mbele ya haki!
...
Alietayari anipm nimtumie nö yangu aingize mijihela kwa tigo pesa, mpesa or kwa wale wailionje ya Tz watatumia bakileiz kufanikisha mchakato!
Tuanze na wewe utachangia nini? sofa tayari tumepata.
 
Back
Top Bottom