Kabila lenye hali ya hewa bora kabisa nchini kwa uzalishaji wa mazao

Derspiegel

JF-Expert Member
May 30, 2016
285
242
Tanzania ni mojawapo ya nchi zinazoongoza barani Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara kwa kuwa na maeneo makubwa yenye hali mbaya ya hewa kwa uivishaji wa mazao ya chakula na kilimo. Yaani ni nchi ya pili tu nyuma ya Sudan Kusini kwa kuwa na meneo makubwa yanayopata mvua kidogo.

Kitaalamu, kiwango cha chini cha mvua kinachofaa kwa kuivisha vyema mazao yanayohimili ukame katika Ukanda wa Tropical ni mm 750, hivyo maeneo yote yanayopata mvua pungufu ya hizo, hayawezi kuwa na uhakika wa chakula kwa kuwa mvua ni kidogo sana.

Hata hivyo, hapa nchini, Wilaya yenye hali nzuri ya hewa kuzidi zote nchini (Bara) ni Wilaya ya BUKOBA. Baada ya hapo, inafuata Wilaya ya RUNGWE.

Hoja yangu haiko katika kuwa na hali ya hewa nzuri tu bali, HALI YA HEWA TOFAUTI TOFAUTI. Ni katika kigezo hiki, MAKABILA yafuatayo yanaongoza nchini kwani yameenea katika maeneo yenye aina mbalimbali za hali ya hewa ( yana maeneo yenye mvua nyingi, ya wastani na kidogo; joto jingi, la wastani na kidogo, pamoja; na unyevunyevu mwingi, wastani na kidogo).

La kwanza ni WACHAGGA, wanafuata WAHAYA, kisha WANYAKYUSA, kisha WASAMBAA, kisha WAMERU (na WAARUSHA).

Kundi la pili pia la makabila yenye hali nzuri ya hewa yenye utofauti tofauti ni WAMATENGO (na WANYASA), kisha WALUGULU, kisha WAKEREWE, kisha WAANGAZA, kisha WAKURYA, kisha WAHA, kisha WABONDEI, kisha WANDALI na kisha WANYIHA.
 
Watu wengi wamekuwa wakisumbuka kutafuta sababu za baadhi ya makabila kuwa juu kielimu. Lakini sababu kuu ndiyo hii - Makabila yote yaliyoendelea kielimu, yametapakaa katika ukanda wenye viwango tofauti vya mvua na joto tofauti tofauti.

Mfano wahaya wana maeneo yanayopata mvua zaidi ya mm 1900 (heavy rainfall) hadi yenye chini ya mm 800. Hivyo wana uwezo mkubwa wa kuzalisha vyakula vya kila aina.

Pia mitelemko ya Mlima Kilimanjaro ina mvua ya zaidi ya mm 1500 na kushuka hadi chini ya mm 700. Eneo hili la wachaga lina baridi kali, baridi ya kadri na joto jingi hasa mipakani na Kenya na wilaya ya Mwanga, na mkoa wa Arusha.

Rungwe ina mvua nyingi kuliko sehemu yoyote nchini na ina baridi kali lakini inapata faida kubwa ya hali tofauti kabisa ya hali ya hewa katika wilaya ya Kyela (kote ni WANGONDE - NYAKYUSA), ambako kuna joto kali na hivyo kuwezesha ulimaji wa mazao tofauti tofauti.

Ukerewe ina hali ya hewa tofauti kuanzia eneo lenye mvua mm 1600 hadi chini ya mm 900.

Hivyo kwa mifano hii michache, ni kwamba maeneo ambayo yana hali ya hewa tofauti sana ndiyo yenye uhakika wa chakula na chenye ubora zaidi.

Hivyo jamii zinazoishi ama kuzunguka maeneo ya namna hiyo, zilifanikiwa vizazi na vizazi kujenga akili zao kutokana na uhakika wa chakula kwa muda wote ndiyo maana they are among the brightest in Afrika.
 
Kuwa na unyevu si kweli kuwa na mazao mengi, Kondoa wanavuna sana mazao ya kila aina na si eneo lenye unyevu., Arusha hakuna hata ardhi kubwa ya kilimo watakuwa wanalima wapi mpaka wavune sana, migomba imebaki michache kahawa ndio historia kabisa.
 
Wewe kipimo cha eneo kivuna mazao mengi si kuyahesabu kuwa yako mangapi. Najua kuwa pamoja na ukame mkubwa wa wilaya ya Kondoa na Mkoa wa Dodoma kwa ujumla, wilaya hiyo ina udingo wenye rutuba ya kiasi cha kuivisha mazao kama ulivyo mkoa kame wa Simiyu.
Lakini jiulize, kuna mazao gani ya kudumu yanayolimwa eneo hilo. Mazao kama migomba, na yaliyoletwa na wakoloni kama chai na kahawa ni kiipimo pekee cha eneo husika kuwa na hali ya hewa. Aidha kustawi vyema kwa mpunga na matunda sehemu husika ni kipimo kikubwa kingine.
Katika posts za awali, sikutaja wilaya za Kilosa, Mvomero, Kilombero, Njombe, Hanang, Butiama, Karagwe, Misenyi, Kasulu, Kibondo na baadhi katika Nyanda za Juu kusini, lakini maeneo hayo ni bora kwa uzalishaji wa mazao ya aina mbalimbali kuliko Kondoa.
 
Tanzania ni mojawapo ya nchi zinazoongoza barani Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara kwa kuwa na maeneo makubwa yenye hali mbaya ya hewa kwa uivishaji wa mazao ya chakula na kilimo. Yaani ni nchi ya pili tu nyuma ya Sudan Kusini kwa kuwa na meneo makubwa yanayopata mvua kidogo.

Kitaalamu, kiwango cha chini cha mvua kinachofaa kwa kuivisha vyema mazao yanayohimili ukame katika Ukanda wa Tropical ni mm 750, hivyo maeneo yote yanayopata mvua pungufu ya hizo, hayawezi kuwa na uhakika wa chakula kwa kuwa mvua ni kidogo sana.

Hata hivyo, hapa nchini, Wilaya yenye hali nzuri ya hewa kuzidi zote nchini (Bara) ni Wilaya ya BUKOBA. Baada ya hapo, inafuata Wilaya ya RUNGWE.

Hoja yangu haiko katika kuwa na hali ya hewa nzuri tu bali, HALI YA HEWA TOFAUTI TOFAUTI. Ni katika kigezo hiki, MAKABILA yafuatayo yanaongoza nchini kwani yameenea katika maeneo yenye aina mbalimbali za hali ya hewa ( yana maeneo yenye mvua nyingi, ya wastani na kidogo; joto jingi, la wastani na kidogo, pamoja; na unyevunyevu mwingi, wastani na kidogo).

La kwanza ni WACHAGGA, wanafuata WAHAYA, kisha WANYAKYUSA, kisha WAKEREWE, kisha WASAMBAA, kisha WAMERU (na WAARUSHA) na WAANGAZA.

Kundi la pili pia la makabila yenye hali nzuri ya hewa yenye utofauti tofauti ni WAMATENGO (na WANYASA), kisha WALUGULU, kisha WAKURYA, kisha WAHA, kisha WABONDEI, kisha WANDALI na kisha WANYIHA.
Hakuna kabila la wa Arusha,hao wanaojiita hvyo ni ubishoo tu kwa kua waliwahi kuja mjini,wale wote ni wa Masai
 
Pamoja na kutaja maeneo yenye hali nzuri ya hewa lakini kutokana na mabadiliko ya tabia nchi (climate change), maeneo yaliyokuwa yakipata mvua nyingi sana aina ya conventional rainfall, yakiwemo ya Bukoba, Muleba na Ukerewe, yameathirika kwa kiwango kikubwa kutokana na kupungua kwa mvua katika ukanda huo wa Ziwa Victoria.
Japokuwa maeneo yote nchini yameathirika sana na mabadiliko ya tabia nchi, maeneo ya milimani yanayopata mvua ya aina ya relief (orographic), yakiwemo ya Rungwe na Kilimanjaro, hayajaathirika sana kama maeneo yasiyo ya milimani.
Ndiyo maana uzalishaji wa mazao yanayohitaji mvua nyingi Kanda ya Ziwa, hasa migomba katika Wilaya za Bukoba, Muleba, Ngara, Misenyi, Karagwe na Ukerewe, umepungua sana kutoka katika kuzalisha zaidi ya asilimia 70% ya ndizi nchi nzima hadi chini ya asilimia 40%.
 
Hakuna hatari kubwa kama hii ya kila mtu kujifanya nae ni mchambuzi!!! Hivi kwanini kila mara unapenda kuhusisha elimu na DINI na MAKABILA wakati ukweli upo wazi kwamba ubora wa elimu unatokana na uwekezaji kwenye sekta hiyo? Dar es salaam hapa kuna joto kweli kweli na kuna watoto kibao hata huko mikoani kunafananaje hawajui! Lakini pamoja na hayo, baadhi ya shule za Dar es salaam na maeneo ya jirani bado zinafanya vizuri kwavile tu kuna uwekezaji mkubwa kwenye hizo shule! Enzi zetu hapa Dar es salaam tulikuwa tunaburuzwa na Shule ya Mzizima! Over 90% ya wanafunzi wa Mzizima walikuwa Waasia huku majority wakiwa Wahindi! Na bado walikuwa wanapasua paper kweli kweli kv Mzizima kulikuwa na uwekezaji wa kutosha!

Juzi hapa ulizungumzia shule za kata... nikakupa mfano wa Mbeya na Kilimanjaro jinsi ambavyo shule za Kata zinazalisha mzigo wa Division Five bila kujali shule husika ipo wapi! Na hii ni kwa sababu shule za Kata hazina facilities za kutosha; kwahiyo haijalishi uwe Mkristo au Mwislam, Shule za Kata ni jipu kwa wote ingawaje hatupaswi kuzipuuza!

Hizo sehemu ulizotaja MSINGI sio makabila na hali ya hewa kwahiyo acha upotoshaji usio na maana. Kilimanjaro kwa mfano; ni vile tu Wakoloni wa Kizungu walifikia maeneo hayo na kujenga mashule kiasi cha kufanya wakazi wake kuwa na mwamko wa elimu tangu enzi za elimu! Na ingawaje kilichowavutia huko ni hali ya hewa, lakini haimaanishi endapo wangefikia maeneo yenye hali hewa tofauti na huko basi hata kama wangejenga mashule bado ingekuwa kazi bure!!

Sababu kuu ya tofauti za kielimu nchi hii ni sababu za Kihistoria and nothing else. Na ndio maana hata huko kwenye hali ya hewa mzuri, ni kule tu ambako Wakoloni wa Kizungu waliwekeza Kielimu ndiko kulikopiga hatua!
 
Hali ya hewa ya nchi ktk uzalishaji wa mazao ina uhusiano gani na kabila la mtu. Roho ya shetani ya ukabila na ukaburu ikutoke kwa jina ya yesu.
 
Hakuna kabila la wa Arusha,hao wanaojiita hvyo ni ubishoo tu kwa kua waliwahi kuja mjini,wale wote ni wa Masai
Wewe ndio hujui History, yuko sahihi kabisa waarusha na wamasai ni makabila mawili tofauti. Mwaarusha aliadopt culture ya wamasai but their origin is different...kasome historia ya makabila vizuri.
 
Hivi meru na wameru umeangalia wanaokaa USA na Tengeru au wapi unaijua kweli hali ya hewa ya Meru? Kuna upepo na baridi na vichaka vifupi vifupi kwa uzoefu wangu wa Meru jimbo la Nassari haya Ukerewe napo kweli umeishi kweli? Mahali hata maji hawana na wana ziwa miti ya mbao na jamii ya machungwa ndo yanakubali Ukerewe unayosemea labda ya miaka hiyo ila ya sasa haitofautiani na Musoma Wasambaa nakubali wengine sijui jui vizuri sijaishi uko ila Meru na Ukerewe hapana
 
Hakuna hatari kubwa kama hii ya kila mtu kujifanya nae ni mchambuzi!!! Hivi kwanini kila mara unapenda kuhusisha elimu na DINI na MAKABILA wakati ukweli upo wazi kwamba ubora wa elimu unatokana na uwekezaji kwenye sekta hiyo? Dar es salaam hapa kuna joto kweli kweli na kuna watoto kibao hata huko mikoani kunafananaje hawajui! Lakini pamoja na hayo, baadhi ya shule za Dar es salaam na maeneo ya jirani bado zinafanya vizuri kwavile tu kuna uwekezaji mkubwa kwenye hizo shule! Enzi zetu hapa Dar es salaam tulikuwa tunaburuzwa na Shule ya Mzizima! Over 90% ya wanafunzi wa Mzizima walikuwa Waasia huku majority wakiwa Wahindi! Na bado walikuwa wanapasua paper kweli kweli kv Mzizima kulikuwa na uwekezaji wa kutosha!

Juzi hapa ulizungumzia shule za kata... nikakupa mfano wa Mbeya na Kilimanjaro jinsi ambavyo shule za Kata zinazalisha mzigo wa Division Five bila kujali shule husika ipo wapi! Na hii ni kwa sababu shule za Kata hazina facilities za kutosha; kwahiyo haijalishi uwe Mkristo au Mwislam, Shule za Kata ni jipu kwa wote ingawaje hatupaswi kuzipuuza!

Hizo sehemu ulizotaja MSINGI sio makabila na hali ya hewa kwahiyo acha upotoshaji usio na maana. Kilimanjaro kwa mfano; ni vile tu Wakoloni wa Kizungu walifikia maeneo hayo na kujenga mashule kiasi cha kufanya wakazi wake kuwa na mwamko wa elimu tangu enzi za elimu! Na ingawaje kilichowavutia huko ni hali ya hewa, lakini haimaanishi endapo wangefikia maeneo yenye hali hewa tofauti na huko basi hata kama wangejenga mashule bado ingekuwa kazi bure!!

Sababu kuu ya tofauti za kielimu nchi hii ni sababu za Kihistoria and nothing else. Na ndio maana hata huko kwenye hali ya hewa mzuri, ni kule tu ambako Wakoloni wa Kizungu waliwekeza Kielimu ndiko kulikopiga hatua!
Sijajifanya mchambuzi, maana unaweza ukijiita mchambuzi lakini unaowachambulia wsikuone ulewachambulia. Hakuna haja ya kunishambulia wewe jaribu kunijibu kwa hoja pekee tu inatosha.
Unakimbilia kusema kuwa utofauti wa kielimu unatokana na uwepo wa wazungu katika eneo husika. NA KWA TAARIFA YAKO, HILI KOSA LAKO NDILO KIINI CHA HASA POSTS ZANGU - KUCHUKULIA MAENDELEO YA SEHEMU NA UWEPO WA WAZUNGU.
Fuatilia idadi ya wazungu waliokuwa wakiishi Bukoba, Muleba, Karagwe, Ngara, Misenyi, Ukerewe, Tarime na Kasulu, halafu linganisha idadi ya wazungu waliokuwa wakiishi Dar.
Au jiulize kati ya Bagamoyo na Dar dhidi ya Nyanda za Juu Kusini ni wapi wazungu waliwekeza sana kipindi cha ukoloni.
 
Hivi kati ya Brazil na Argentina dhidi ya nchi za Ulaya nani wana miundombinu bora ya kukuza soka? Au kati ya China na Brazil nani ana academies bora za soka? Utapata jibu tu ukiwa na nia ya kuelewa.
Angalia uwezo balaa wa wakimbiaji wa mbio ndefu (marathon) wa Kenya na Ethiopia, unadhani wanatokea maeneo gani ya nchi hizo? Ulishasumbuka kujua why?
There is something more hidden that we human beings are intentionally or accidentally ignoring it at the expense of scapegoats (kwamba kulikuwepo upendeleo wa wazungu kujenga miundombinu ya elimu).
Kwani shule zilizojengwa na wakoloni ni ngapi hizo jamani kiasi cha kukataa ukweli?
 
Hadi mwaka 1994, hakukuwepo shule yoyote ya sekondari ya umma katika Wilaya ya Ukerewe (ukiacha shule za sekondari za binafsi - Murutunguru na Kagunguli, ambazo hata hivyo zilikuwa zinachukua zaidi watoto wa wenye hela zao waliofeli hasa kutoka nje ya Ukerewe).
Sasa fuatilia vichwa vya huko jinsi vilivyotapakaa kwenye maofisi nchi nzima. Utajiuliza mbona hawakuwa na shule lakini wamekuwa juu kielimu.
 
Thread yako inachochea ukabila kwa mbali.
Kwanini kwenye neno "kabila" usingeweka neno "sehemu" au "mikoa"
 
Hali ya hewa ya nchi ktk uzalishaji wa mazao ina uhusiano gani na kabila la mtu. Roho ya shetani ya ukabila na ukaburu ikutoke kwa jina ya yesu.

Haufahamu sababu za kuwepo makabila tofauti tofauti ndiyo maana. Unafahamu kuwa makabila karibu yote ya Tanzania ni ya asili ya kibantu, isipokuwa baadhi ya makabila yaliyoko mikoa ya Mara, Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Dodoma na Tanga. Sasa kwa nini kuna makabila hayo yenye asili ya kibantu, kwa nini wasingekuwa wanaongea lugha hiyo moja waliyoanza nayo huko Cameroon miaka 2000 bc iliyopita?
Hivyo ujifunze kuwa kuna tofauti (mara nyingi) kubwa ya hali ya hewa kati ya kabila na kabila hasa yale yasiyo na uhusiano wa karibu. Fikiria kabila la Wairaq (wambulu) lililoko mkoani Manyara. Eneo lao la asili lina hali nzuri ya hewa huko Hanang na Mbulu lakini makabila yote yanayolizunguka yana ukame mkubwa - wasanzu, wamasai, watatoga, wambungwe, wagorowa, wanyaturu na wasandawe. Nyie ndio mko msitari wa mbele kuwa mama mja mzito akila vyakula vizuri anasaidia mtoto kuwa na akili na hadi leo kuna sijui unga wa lishe kwa watoto - je eneo la Hanang ungelilinganisha na eneo la waisanzu ama wagorowa, ni lipi vyakula vilikuwa vinapatikana vya kutosha, je trend hiyo ikiendelea haitasababisha baadhi ya jamii kuwa na akili (za darasani) kuliko nyingine kutokana na utofauti huu wa hali ya hewa?
 
Hebu angalieni utofauti mkubwa wa hali ya hewa kati ya kabila la waangaza na wasubi (na washubi) wa wilaya ya Ngara, ambako kwa waangaza kuna hali nzuri ya hewa tofauti na wasubi. Hivi kwenye hali kama hiyo kwa nini wale waangaza wasiwe ahead kwa wasubi kutokana na upatikanaji mkubwa wa vyakula wa miaka mingi?
 
napata ugumu kuhusisha kabila na hali ya hewa au uoto wa eneo fulani. Kila mtanzania kabila lolote anaweza kukaa eneo lolote TZ; unasemaje kabila fulani lina hali ya hewa nzuri??? Si useme eneo fulani lina hali ya hewa nzuri badala ya kutaja kabila? Mfano unaweza sema Lushoto kuna hali ya hewa nzuri na si Wasambaa wana hali ya hewa nzuri! Lol
 
Back
Top Bottom